Nawapenda Sana Wazenji, Soma hapa!

Nawapenda Sana Wazenji, Soma hapa!

sekulu

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2011
Posts
988
Reaction score
158
Katika pita pita zangu nikadondokea hapa Zanzibarwebsite

Kuna Story moja nimeipenda sana Naomba Kushea na Nyie(Nahisi hii ni forum Yao)

Mada: JEEE HILI HALITALETA MATATIZOO?.....



HIVI WANA UKUMBI WENZANGU MUNASEMAJE KUHUSUU,KUMUONESHA MWENZA WAKOO KAMA UMEOZA KWAKEE,YANII HUJIWEZII UTAABANI KWAKE... AU NI BORAA KUTOMUONESHA HIYO HALI? NAOMBA MICHANGO YENUU JUU YA HILII WANAUKUMBII

Michango ilikua kama ifuatavyo:

Majibu ya Mjadala huu

BABENGWA
Hatari iliopo kumnadi kwa kumtangaza - muhibu.Na kuonesha kwa kiasi gani umesalitika kwake ni kwamba unaamsha ari zilizolala na wengine kujikuta mnaoza pamoja kwani wataingia katika foleni - It makes to be high traffic jam .
Hapo sijui unanielewa ? Mpenzi au mapenzi yanataka privancy( faragha ya roho) yanapoanikwa huwa kama uchuro au ushamba..wa mambo.
Nakusihi, kufa kiofisa - Bushako UKIVUNA ULIE KIVULINI BILA YA JOTO LA WAJASIRI WA MALI.

Haahahaaa! ukisema nitasema simalizi hapo..

Permalink Imejibiwa na Spider on May 31, 2011 at 6:53pm Ahsante mtoa mada, mimi nitoe mchango kwa kuanza kusema "Penzi ni kikohozi kulificha hamuwezi" ikiwa kweli munapendana hata ujidai kuficha namna gani basi mambo yatajidhihirisha yenyewe kama yanavyokwenda. hiyo ni kwa upande mmoja lakinui kwa upande wa pili kwanini usimuoneshe unaempenda kuwa umeoza kwake, muoneshe mwenza wako kuwa unampenda, unamjali na unamthamini kufanya hivyo kutajenga misingi imara ya pendo lenu.


Permalink Imejibiwa na BABENGWA on June 1, 2011 at 7:52am Niwakumbusheni kulikuwa na Raisi mmoja jina nimemsahau.Akipanda kwenye jukwaa huwambia wananchi na wafuasi wa chama chake" jee nnang'ara !! nnapendeza !! basi -hii ni kazi ya mamaenu ndie aning'arishae nvi moja ikitoka yeye ananidondoa " HATIMAE wenye nguvu kama yeye leo hanae tena wamemnyanganya
Nasisitiza ukianza kuonesha na kulia pendo kwa upatu mjomba na kuonesha hisia kama umeoza hujifai kwa bibi amini wengine watakusaidia kujaribu bahati nasibu zao .
Naamini, hakuna yeyote asiyesemezeka juu ya mapenzi ukimkosa wewe umemkosea njia au mtego wako mekuwa dhaifu lakini aligundua mtego anamnasa kumtia mikononi.
SHAIRI LAKE NITAKUJA PUNDE WACHE NIINGIE MAABARA NICHANGANYE MADAWA..... hahaahaa!


Imejibiwa na bushako on June 1, 2011 at 9:29am
hali zenuu?ahsanteni babengwa na spider kwa michango yenuu.ila binafsi nayakubali yote lakini kwa spider tabiya ya wenzetu mara nyingi akigunduwaa upo hali hiyoo anaanza kukudenguliya kisa hujiwezi kwakee.mifano ipoo hatimayee inakuwa bora penzi na sio penzi boraa...
- ima kwa babengwaa usemayo ni sahihi na pengine kutomuonesha ndio sahihi ,lakini wanasema wahenga (penzi loisilinadi halinogii!!..) na na pia nachelea ule usemi usemao (harufu ya waridi ,huleta ufisadii.)ningependa tuwe wawazi zaidi kuhusu hilii jee bora lipi? natowa hojaa ........


Permalink Imejibiwa na BABENGWA
Apendwae Akijua Haachi kujizuzua
Uso ataubedua Na pozi kukufanyia
Hilo sipo angalia Wazimu utajitia
UNGEPENDA BORA MOYO-KULIKO KUJIHASHUA
Bora kipimo tumia Vipi yalivyoanzia
Kuliko kufikiria Pendo kukuelemea
Maneno kujisemea Pendo lisije kuua
UNGEPENDA BORA MOYO-KULIKO KUJIHASHUA

Mara ngapi ushapima Hisia wapi zendapo
Ushafikisha kalima Tamko la upendapo
Bure isiwe walima Huna mbegu upandapo
UNGEPENDA BORA MOYO-KULIKO KUJIHASHUA

Hebu fanya kaka hima Sema isiwe hayupo
Woga si silaha njema Sema popote alipo
Huwa hawezi simama Afa kwako si penginepo
UNGEPENDA BORA MOYO-KULIKO KUJIHASHUA

Haaahaaa!! NDIO Nilichovumbua MAABARA YANGU( laboratory) .
Hivi niona uchukua hatua ya kukabiliana nae huyo 'KIPUSA' isiwe wapenda maneno hayajafika au bora tufafanulie hatua za msingi ulizochukua ili tuone wazi wazi ,pana PENDO hapo au ni babaisha *****.
ENDELEA....!


Imejibiwa na Zulfikar Makamba Jana Mapenzi hayafichiki,yakimea yanamea,Ya kweli hayana mikiki,huwezi kuyapangia,Ukipenda hubanduki,na huwezi jisifia,Ya dhati hayapangiwi,yakikanywa yanazidi.

bushako

ahsanteni wana ukumbi kwa nasaha zenuu na nasema hiviii:-....

babengwa nimekusikia, maneno uliyonambia.
kwa kweli huu ni usiaa, tausamba kwa wanachama.
na siwezi kuupuziaaa, akilini umeniingiaaa.

nilijiona nafaidiiiiiiiiiiiiiii, mfalme ndio mimi.
nikamfanyia uhabibiiii, sikutambuwaa maskini.
ila sasa nataqidiiiiiiiiiiii, mkaidii hakika hafaidii.

kwa hakika niliozaaa, kwa mtoto wa kipemba.
nikalishwa mauzauza, nahisi ndio yaliyonipozaa.
hadi sasa najiuguzaa, muathirika yupo nyumaa.

babengwa nikulizeee, na wala usinificheee.
wewe ni mara ya nane, unapelekwa mpute mpute.
wala usikasirikeeeeee, ulipocheza kibafuteee.

ushauri nilioupataaaa, kwa sasa natamkaa.
mpenzi mpya nikipata, sitafanya lebenekaa.
hata akinipakataaaaa, nisiwe bushako niwe nimeokotwa.

yailahii ya rabbanaa, dua tukubalieee.
utujalie uzimaaaaaa, nyumba zetu usilinde.
tusiwe twapiganaaa, kila mwenye mke atulie.


Nimeipenda kwani watu wako Deep Mbaya Mpaka Wanawekeana Mashairi humo ndani, Sio Mchezo
 
Back
Top Bottom