Nawaona walipaji wa mafao wakiingia Kisutu siku za mbeleni

MWITONGO MAARIFA

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
276
1,428
Sheria ya mafao ilitungwa na kupitishwa na Bunge na kanuni zikatungwa na Waziri mwenye dhamana zikiwa zinaeleza namna mafao yatakavyolipwa hapa nchini.

Rais aliyesaini mswada kuwa Sheria akaja kutangaza kuwa Sheria na kanuni hizo zisitumike hadi 2023 na kwamba Sheria za zamani zitumike.

Kauli ya Rais yaweza kuwa Sheria lakini kauli ya Rais katika mazingira Kama haya yanayohusu maslahi ya watu ilipaswa kuendana na maelekezo ya Sheria gani itumike na hata kumwelekeza Waziri mwenye dhamana kufuta kanuni zilizotungwa na pia Bunge kuifuta Sheria mpya ndipo turudi kwenye Sheria mpya.

Mituko hii ilikuwa na upigaji mwingi na mashimo ya upigaji yalifukiwa na Sheria mpya, Leo mifuko muflisi inaambiwa ilipe mafao wakati hata watendaji wake hawapo Tena, Je mlipaji atatoa wapi fedha na mifuko iliyovunjwa itajiunganisha vipi upya?

Namwonea huruma Sana msimamizi wa mifuko hii, Kama atashindwa kurudi kwa Waziri na hata Mhe.Rais kumwomba atoe maelekezo mbalimbali kufanikisha mchakato wa malipo basi ipo shida huko mbele hasa kwenye ukaguzi. Anaweza asiwe mwizi lakini akaambiwa ametumia vibaya madaraka.

Anachotendewa Tido Mhando leo kinaweza kumpata mwingine yeyote hapa nchini pale anapopokea maelekezo kutoka Juu na kuyafanyia kazi. Bora uishi kwa buku kuliko milioni tano zitakazokufedheesha siku za mbaleni.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom