Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,814
- 218,474
Naomba kuyafahamu japo kwa uchache mazuri yaliyofanywa na Malinzi .Wewe kaa pembeni na tunashukuru sana kwa msaada wako kipindi kile,kwa sasa tupo wengine tuliojitolea kumuweka tena ili amalizie yale mazuri aliyoyaanzisha japokuwa wewe huyaoni.
Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
Nyamaza, mbona haisaidii!Nilikuwa mmoja wa wadau wa soka tuliopambana kufa na kupona kuhakikisha kwamba Jamal Malinzi anashinda urais wa TFF , Tulipambana kwa udi na uvumba , Kwa hali na mali hadi tukafanikiwa .
Lakini kwa madudu yaliyotokea kwenye uongozi wake , nimeona nijitokeze mbele yenu ndugu zangu kuwaombeni sana radhi kwa hujuma hii tuliolifanyia soka la Tanzania , mtoto akinyea mkono usiukate , Naahidi sitorudia tena kufanya madudu ya kumbeba mtu yeyote asiye na uwezo kwa vile tu ni Mfanyabiashara mwenzangu .
Wito wangu kwa wadau wa soka wa Tanzania , hakikisheni mnachagua mtu mwenye uwezo wa kuongoza , na mwenye kuzijua hasa changamoto za soka la nchi hii.
Niko tayari kusaidia upande wowote wa kambi ya mgombea yeyote mwenye weledi na mwenye maono ya kusukuma soka la Tanzania mbele zaidi.
Mungu ibariki TFF .
Msingi wa soka ni timu za vijana Malinzi kajitahidi sana kwa hili kukuza na kuweka misingi mizuri kwa soka la vijana na matokeo yake hayataonekana kwa muda mfupi huu,soka la wanawake kajitaidi mpaka kulifufua hili ambalo lilikuwa lishakufa,timu ya Taifa kajitahidi kila awezalo ikiwa ni pamoja na kuleta makocha wa nje na ndani,kugharamia kambi ya timu nje na ndani pamoja kutoa posho stahiki ambapo jambo hili huko nyuma lilikuwa na mshike mshike mpaka bakuli litembezwe. Pia amejitahidi sana kupunguza migogoro ya vilabu na vyama vya soka mikoani ikiwemo TTF yenyewe. Ligi kuu kuonyeshwa live,kutafuta wadhamini kila kona kusaidia vilabu na timu ya Taifa. Kufanikiwa kutupatia nafasi ya kuwa mwenyeji wa u17, kufanya maboresho mbalimbali ya ligi na baadhi ya viwanja. Hayo ni machache tuu yapo mengi.Naomba kuyafahamu japo kwa uchache mazuri yaliyofanywa na Malinzi .
Wewe kaa pembeni na tunashukuru sana kwa msaada wako kipindi kile,kwa sasa tupo wengine tuliojitolea kumuweka tena ili amalizie yale mazuri aliyoyaanzisha japokuwa wewe huyaoni.
Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
Na wewe unalihitaji hili dili?Naona umepata dili la kumtetea uku JF. Hongera sana,endelea kula pesa za TFF.
Basi endelea kusubiri pesa safi.Hapana,siitaji pesa chafu.
Wanjiru hataki .[HASHTAG]#malinziout[/HASHTAG] 2017