Nawaomba radhi Watanzania kwa kushiriki kumuweka Madarakani Malinzi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,165
217,107
Nilikuwa mmoja wa wadau wa soka tuliopambana kufa na kupona kuhakikisha kwamba Jamal Malinzi anashinda urais wa TFF , Tulipambana kwa udi na uvumba , Kwa hali na mali hadi tukafanikiwa .

Lakini kwa madudu yaliyotokea kwenye uongozi wake , nimeona nijitokeze mbele yenu ndugu zangu kuwaombeni sana radhi kwa hujuma hii tuliolifanyia soka la Tanzania , mtoto akinyea mkono usiukate , Naahidi sitorudia tena kufanya madudu ya kumbeba mtu yeyote asiye na uwezo kwa vile tu ni Mfanyabiashara mwenzangu .

Wito wangu kwa wadau wa soka wa Tanzania , hakikisheni mnachagua mtu mwenye uwezo wa kuongoza , na mwenye kuzijua hasa changamoto za soka la nchi hii.

Niko tayari kusaidia upande wowote wa kambi ya mgombea yeyote mwenye weledi na mwenye maono ya kusukuma soka la Tanzania mbele zaidi.

Mungu ibariki TFF .
 
Nyamaza, mbona haisaidii!
 
Naomba kuyafahamu japo kwa uchache mazuri yaliyofanywa na Malinzi .
Msingi wa soka ni timu za vijana Malinzi kajitahidi sana kwa hili kukuza na kuweka misingi mizuri kwa soka la vijana na matokeo yake hayataonekana kwa muda mfupi huu,soka la wanawake kajitaidi mpaka kulifufua hili ambalo lilikuwa lishakufa,timu ya Taifa kajitahidi kila awezalo ikiwa ni pamoja na kuleta makocha wa nje na ndani,kugharamia kambi ya timu nje na ndani pamoja kutoa posho stahiki ambapo jambo hili huko nyuma lilikuwa na mshike mshike mpaka bakuli litembezwe. Pia amejitahidi sana kupunguza migogoro ya vilabu na vyama vya soka mikoani ikiwemo TTF yenyewe. Ligi kuu kuonyeshwa live,kutafuta wadhamini kila kona kusaidia vilabu na timu ya Taifa. Kufanikiwa kutupatia nafasi ya kuwa mwenyeji wa u17, kufanya maboresho mbalimbali ya ligi na baadhi ya viwanja. Hayo ni machache tuu yapo mengi.

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
 
Tatizo la watanzania tunataka output ionekane hapo hapo bila kujua kuwa kila kitu kinahitaji good foundation kwa maana ya kuwa sisi tunachokitaka kukiona ni Taifa Stars iwe inashinda kila match bila kusahau kuwa hatuna msingi mzuri wa timu za Watoto na vijana ambapo sasa Malinzi ndio amejikita huko.

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
 
Wewe ni muungwana, tofauti na CCM. CCM wanapitisha vimeo wenyewe huku wakishangilia. Siku wanufaika wa vimeo wakishughulikiwa, CCM wanashangilia tena kana kwamba sio wao waliopitisha vimeo. CCM nao wanapaswa kutuomba radhi kwa sababu ya IPTL na Madini.
 
Back
Top Bottom