Nawanyoshea kidole wanawake msitafute mchawi.

Nawanyoshea kidole wanawake msitafute mchawi.

Judgement

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2011
Posts
10,326
Reaction score
4,787
Hapa Jamvi haipiti wiki hujaona umeshushwa uzi kidole kaelekezewa Mwanaume.
Kidole cha lawama na mashambulizi makalimakali, maneno kama :
> Wanaume hawaridhiki.
> Wanaume wengi baadhi yao hawatosheki.
> Wanaume wengi baadhi yao malaya. N.k
Husikika maneno kama haya with releated matter ! Nachukua fursa hii kukubali lawama hizo na nitoe mifano michache visababishi vya hayo yanayolalamikiwa.
1. Mume amerudi kunako kazi/mihangaiko ana mfuko wa mazagazaga mkononi huamki kumpokea wala nini.
2. Anakusalim "habari za hapa" unajibu "nzuri" umemaliza, huku domo umelivuta kutoka hapo ulipokaa kwenye kochi hadi linakaribia kugusa screen ya Tv, kisa umeomba akufanyie safari uwende kwenu kwenye harusi ya mdogo wako ukaambiwa haitowezekana kwa kua financial mambo sio January iko mbele shughuli za kifedha zitakua nyingi.
3. Kufuatia visirani kuongezeka kinachofata ni unaanza kumjibu majibu ya dry yanayomtia mwanaume hasira na mnaanza kutupiana maneno yanayozaa bifu kamili.
4. Kinachofata ni kutogusana kitandani. Ambapo Biological organs hazitambui bifu lenu.
5. Kinachofata mwanaume ni kuangalia atakapopata utulivu! Anaanza ku'cheat .
6. Kama inavyokua wanawake wanaobahatika kuangukiwa na waume wa wenyewe hujituma isivyo kawaida ufundi atakaoupata kule hujikuta kwako haupati.
Anaanza kulowea hadi mke unajua.
Hapa nani mchawi ? Kama sio wanawake wenyewe ?
 
mule mule, mfumo dume
bora kucheza mdumange
 
Si unaona hawana majibu ya kutoa.Umewagusa mwana.Wanawake wa cku hz wana mapenz ya kimagumashi
 
Si unaona hawana majibu ya kutoa.Umewagusa mwana.Wanawake wa cku hz wana mapenz ya kimagumashi

Niliwahi kuwathikia wadhungu wakithema Silency means Yes ! Ok Doyi nisalimie Kulwa.
 
ukiona hvyo mna li ugomvi lenu linafukuta, haiwezekani akununie na kukunyima bila sababu
 
ila kweli wanawake visirani vinatuponza kwenye nyumba. ilo sina upinzani cz kila kitu kina ukweli.
 
ukiona hvyo mna li ugomvi lenu linafukuta, haiwezekani akununie na kukunyima bila sababu
ofcourse sometimes kunakuwaga na sababu za msingi ila sa nyingine ni visirani vyetu tu na kukomoana.
 
ofcourse sometimes kunakuwaga na sababu za msingi ila sa nyingine ni visirani vyetu tu na kukomoana.
Huu ndo uungwana, hongera kwa kuwa mkweli Sister! Natamani ningekupa zawadi ya x-mass kwa uungwana wako, natumaini ni funzo kwetu sote.
 
Nijuavyo mm mwanamke aliyempenda mmewe mpaka kuolewa nawe na mwanamke muelewa anayeijua thaman ya ndoa yake hawezi from no where akanza vituko km hivyo,lzm kuna chanzo cha tatizo,watu tunatofautiana km mwanaume umeshajua mapungufu ya mkeo tafuta namna kumweka sawa mapema na kuwa na mawasiliano mazuri na kuwa mnamaliza tofauti ndogo ndogo zinazotokea kabla hayajawa makubwa na kumpelekea kuanza vituko na mwanaume kuchiti km suluhisho!wanawake huwa hawafanyi jambo bila sababu!
 
Kweli kbs canta, mwanamke kama mwanamke haanzi kununa wala madharau ndan ya nyumba bila sababu, chunguza tu utakuja kugundua source, na nyie wanaume sln si kucheat jaman jarib kutambua source ya hayo yote na mrekebishane frm there. kweli nawaambia mwanamke habadili frm nowhere! there must b a reason.
 
Nijuavyo mimi matatizo yapo pande zote japokua yanatofautiana,so hakuna wa kumfunga mwengine kengele hapa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom