Nawakumbusho: MAGUFULI DAY ni kesho

Nawakumbusho: MAGUFULI DAY ni kesho

Aendelee kupumzika mahali panapo mstahili, kipindi chake wafanyakazi wa ofisi za uma walikua na adabu hata kama ilikua ya uoga wananchi tulikua tunapata ushirikiano wa kutosha kabisa kutoka kwao lakini utawala wa bibi chaudele yamekua yale yale za zamani, alikua na mabaya yake mengi lakini mazuri yake machache yameshindwa kufikiwa na bibi wanaemwita mwema
 
Hakuna mtu mwenye akili timamu atamkumbuka huyu Bedui.
Hujitambui wewe.

Rais ambaye tatizo la umeme lilikwisha, watu wakavuta nguzo za umeme kwa 27000/= , Rais aliyewashughulikia ipasavyo mafisadi, Rais aliyewabana watumishi wakawajibika, Rais aliyejenga miundombinu mikubwa ya barabara, madaraja na bwawa la umeme, Rais aliyekuwa anafanya kazi usiku na mchana, Rais aliyebana matumizi kwa kutosafiri nje ya nchi na Rais aliyejali maisha ya Watanzania kwa kudhibiti mfumko wa bei. Wakati wake hakukuwa na uhaba wa sukari wala bei kupanda, bei ya usafiri haikupanda kihuni huni wala bei ya mafuta haikupanda.

Unataka nimchukie kisa nini?????

Utakuwa na akili kweli wewe????
Wakati wake hakukuwa na tozo wala kukopa kopa, unataka achukiwe? Pooole ndugu.
 
Kiongozi pekee aliyenitoa chozi la kamasi baada ya kifo chake.
Hii ilikuwa ni siku ya ijumaa alipokuwa anazikwa chato.
Nililia kama mtoto wakati ni mtu mzima

REST IN PEACE MAGUFULI.
 
Back
Top Bottom