Teh fanya basi kunilipa kwa gazeti langu.
There is absolutely no justification for cheating on someone . Mkeo akikosea/ kujisahau ndo ukacheat? Muwe na hofu ya Mungu, punguzeni tamaa za ngono na kuwe na mawasiliano kati wa wanandoa inapotokea tu kuna kitu hakijakaa sawa
Shem kwanza Nikuhakikishie Kitu kimoja ambacho labda bado hujakijua.. Mimi ni muislam safi ninaye Amini, kuheshimu na kufuata matendo yote mema likiwemo Hilo la Hofu ya Mungu. Kwahiyo Kuhusu Hilo nakuomba Utoe Shaka.
Pili lazima tukubali kuwa mahusiano ya kimapenzi na hata kindoa hugubikwa na mitafaruku na migongano isiyo na mwisho. Unapoamua kwa Moyo Wako kuwa unahitaji au Unaingia katika mahusiano ni kwamba yule Unayeingia naye kwenye ndoa ni kwamba Umempenda na Kumchagua Yeye Katika Wote uliyowahi kukutana nao.
Pia Umeangalia na kuchunguza kuwa huyu ni Mke au Mume bora na katika kuchunguza hivyo vitu ni kwamba umejaribu Kushirikisha Akili na Moyo wako katika kufanya Maamuzi ambayo Kwako Uliamini kuwa ni maamuzi sahihi.
Ikiwa ni Hivyo na Wote mkakubaliana Hapa sioni Sababu ya mume kucheat au mke kusaliti katika ndoa kwa kuwa wakati wakufanya Chaguo Wote mliridhiana kuwa mko tayari katika Hilo. Kwahiyo kama mmoja atakuwa msaliti basi huhesabiwa ni tamaa au wakati wa ndoa na muhusiano mmoja hakuvutiwa na mwingine isipokuwa alipenda sababu labda ya tamaa au kwasababu ya Pesa (kama wengine wanavyoshadadia)
Kuhusu kuwahisisha kwangu wanawake na Usaliti, pointi yangu ni kwamba Wanawake wengi wanapoolewa Huwa Wanajisahau na kusahau majukumu Yao kama wamama wa nyumbani na hata kile ambacho kiliongeza kachumbali mpaka kusababisha mwanaume kutangaza ndoa nacho kinaachwa kwa kuwa tayari yupo ndani ya ndoa.Siku zote mwanamke lazima atambue na kuelewa kuwa ndani Ya ndoa ndio kunahitaji ubunifu na Upya, ukiwa mbunifu na mpya kwenye ndoa kila siku itaongeza mahaba na mapenzi kwa mumeo na Kumfanya Akuwaze kila Wakati.
Na kingine ni lazima uwe na Kauli njema na Heshima kwa mumeo.. Usipojirekebisha Utaachwa na Kusalitiwa kila siku. Mume Anahitaji kubembelezwa sio kultewa kisirani.
NB HATA WEWE USIPOKUWA MBUNIFU UTAACHWA TU KWAHIYO UMAKINI UNAHITAJIKA KATIKA KUILINDA NDOA NA MAHUSIANO YAKO.