Nawachukia sana Polisi

Nawachukia sana Polisi

Ubuyu mchafu

New Member
Joined
Nov 26, 2022
Posts
4
Reaction score
41
Kwa nilipofikia Acha niwachukie tuu hawa viumbe wanaojiita polisi, sio polisi wa kwenye muvi namaanisha hawa polisi wetu wa Tz, yaani nawachukia sana.

Wamesababisha nianze kuishi Maisha ya kimaskini, sina hatia yoyote lakini walinikamata na kuning'ang'ania.

Hawakutaka kuniachia, hawakutaka kunipa dhamana, waliendelea kunishikilia wakinituhumu kwa mambo mazito ambayo sihusiki nayo.

Wameniachia muda ukiwa umeenda sana, wameniachia ni baada ya ndg zangu kuhangaika sana, Wameniachia kwa kunipeleka mahakamani na kunibambika kesi isiyo yangu

Nina maumivu makali sana juu ya uonezi walionifanyia polisi hawa...
 
Wapo humu wengi tu, lakini tatizo ni mfumo wetu kuwa mbovu sana, sheria za hovyo. Kutuhumiwa sio shida ila tatizo ni upande wa waendesha mashitaka (serikali) kuokoteza ushahidi wanaweza kuchukua muda mrefu sana halafu dakika ya mwisho wanafuta kesi. #katibampya
 
Inasikitisha mno kuwa tunaishi kwenye nchi ambayo sensitive issue kama hii inaishia kulalama humu JF, wananchi wa nchi nyingine wanafanikiwa wapi ambapo watanzania wanashindwa?,push backs zitaanza vipi na lini?,Hamza (rip)alionyesha njia baada ya kudhulumiwa ?,tuendelee kula mtori mifupa tutakutana nayo chini.
 
Inasikitisha mno kuwa tunaishi kwenye nchi ambayo sensitive issue kama hii inaishia kulalama humu JF, wananchi wa nchi nyingine wanafanikiwa wapi ambapo watanzania wanashindwa?,push backs zitaanza vipi na lini?,Hamza (rip)alionyesha njia baada ya kudhulumiwa ?,tuendelee kula mtori mifupa tutakutana nayo chini.
Inasikitisha sana mkuu
 
wanasheria wenu wa iliyokuwa TLS juzi wamechambwa kwa kuegemea harakati na kuacha jukumu la msingi la taasisi husika,mambo kama haya yanatesa sana watu masikini,wasio na watu,wala ramank hapa nchini.

mimi nikushauri kama umeonewa na polisi na haki iko upande wako,nenda karoge,kafunge novena au kasone albadir,usimwache dhurumati akaishi.

ila hakikisha 100% hukuhusika na kosa,wala hujawahi dhurumu mtu maana yanaweza kukurudia tu.halafu usiwe kama mtoto wa kike kuita wanaume wote mbwa.
komaa sawa sawa na jamaa aliyekuingiza kwenye matatizo,huo ni upuuzi wake yeye.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom