Navunja ndoa ya mtu!!!!

Navunja ndoa ya mtu!!!!

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2009
Posts
6,157
Reaction score
4,454
Wadau mwenzenu nipo kwenye wakati mgumu sana psychologicaly, kuna dada anataka kuachika kwasababu yangu ilihali hana kosa lolote....Ishu iko hivi Kuna dada(mke wa mtu) nipo naye karibu sana kikazi, siku asipokuwepo ofisini kuna baadhi ya kazi zake hunachia nimsaidie namimi nisipokuwepo ofisini naye hunipa ushirikiano wa hivyo kutokana na nature ya kazi zetu kufanana sana.

Kutokana na ukaribu huu mmewe alianza kuwa na wasiwasi namimi, kwasababu kuna siku nilimpigia simu mkewe akapokea yeye bila hata kujibu salamu yangu akaniuliza shida yangu ni nini? mimi nikamueleza kwamba shida yangu ni ya kikazi nataka kuongea na mkewe,..... kumbe alikuwa naye jirani akampatia nikaongea naye, yalikuwa ni masuala ya kikazi tu yaliyohitaji ufafnuzi wa sekunde chache tu alafu zilikuwa ni saa za kazi, ishu ni kwamba huyu dada na mmewe walikuwa likizo.

Hivi majuzi huyu dada aliwahi kidogo kutoka ofisini kwasababu alikuwa anawahi kumpokea mmewe Airport alikuwa ametokea nje ya nchi kusimamia matibabu ya ndugu yake, all the way kwenda airpot na kuelekea nyumbani kwao tukawa tunawasiliana na huyu dada kuhusiana na vikazi alivyoniachia pale kazini nimsaidie mpaka nilipomaliza mida ya saa2 usiku.

Nikiwa nyumbani mida ya saa4 usiku mwanangu wa miaka3 alichukua simu yangu ikiwa chumbani mimi nikiwa sebureni akawa anaichezea, kwa bahati mbaya akapiga simu kwenda kwa yule dada ikapokelewa na mmewe kila akiongea simu yangu ilikuwa kimya maana alikuwa anaichea mtoto na hakujua kama kapiga simu. baadaye kidogo akapiga yeye, mwanangu akaniletea simu nilipoipokea kumbe ni yule bwana anapiga akaniambia maneno machache tu "HAJAKWAMBIA KWAMBA NIMERUDI? KUANZIA SASA NIMEKUACHIA" nilipojaribu kutaka kujua zaidi nini kinaendelea akanikatia simu, kila nikipiga simu ikawa haipokelewi, kwenye mida ya saa6 usiku akapiga yule dada akiwa amepigwa na kahifadhiwa kwa jirani ndipo nilipogundua nini kilitokea, nimejaribu kumuomba huyu jamaa tuonane tuongee ameniambia nikae mbali naye.

Wadau naombeni ushauri nimsaidieje huyu dada ili kuokoa ndoa yake maana jana amerudi nyumbani kwake lakini mmewe hamsemeshi kitu chochote, akijaribu kumuelewesha anamuambia aje kwangu yeye hataki kuishi naye, najisikia vibaya sana kwasababu mimi ndiyo chanzo na naofia maisha yangu kujisogeza kwenda kunusuru hii ndoa.
 
Wivu jamani sio mzuri kabisa kwa hizi ndoa zetu. sasa jamaa anaweza kuvunja ndoa hivi hivi na mke hajafanya baya lolote.
 
mmmmh ndugu pole haya mambo yapo sana na bora kubadili line na uwaache wenyewe wayamalize usithubutu kusuluhisha wala kuulizia na kuanzia leo usipige tena simu ya huyo dada muwasiliane akiwa job akishaondoka subiri kesho au hata pata msaada wa mfanyakazi mwingine. Ni ushauri wangu tuu kama ulivoomba.
 
mme wake mjinga,achana nae,huna kosa.Mwanaume unazira?!!!!

Huyu jamaa anampenda sana mkewe kiasi kwamba anakuwa na wivu wa kijinga, na tunaomfahamu huyu dada hapa ofisini hana tabia anazomzania labda huko mtaani kwao...mimi kinachoniuma ni huyu dada ikivunjika ndoa yake ilihali hana kwasababu yangu na akiwa hana uhusiano wowote na mimi
 
mmmmh ndugu pole haya mambo yapo sana na bora kubadili line na uwaache wenyewe wayamalize usithubutu kusuluhisha wala kuulizia na kuanzia leo usipige tena simu ya huyo dada muwasiliane akiwa job akishaondoka subiri kesho au hata pata msaada wa mfanyakazi mwingine. Ni ushauri wangu tuu kama ulivoomba.
Ila inaniumiza sana, nimejifunza kitu kikubwa sana hya mambo ya wivu
 
Mshikaji hiyo ngoma nzito.
watu wa namna hiyo ambao hawataki kujua ukweli, wanakuwa na maamuzi mabaya sana dhidi ya mkewe na huyo "mchafuzi" (sikutuhumu).
Mwandikie sms ueleze ukweli wote na kama vipi mshirikishe padri/mchungaji/sheikh (sijui yeye ni dini gani) wake ili huo ukweli udhibitshwe mbele ya huyo kiongozi.
Kuvunja ndoa ya mtu ni hatari sana. jamaa hatoweza kusahau maishani mwake. anaweza kutaka kulipiza kisasi kwa namna usiyotarajia.
Pole sana mkuu.
 
Ninavyoona mimi hapo, huyo mwanamume alikua anatafuta sababu tu ya kutengana na mkewe. Kama anatambua nature ya kazi ya mkewe hakupaswa kufura kwa hasira hivyo, kwani mtu anayeiba mke wa mtu hawezi piga simu in late hours.
 
i hate men who are so abusive!!! kama anamwona mkewe si mwaminifu si amwache?? vipigo vya nn?? angejua ukweli wa story yote si kukimbilia kumpiga mwanamke eti kwakuwa ni weak na hawezi pigana naye....wat a coward.....
 
Nimekwisha mtumia Sms na nataka kutoa taarifa polisi, in case of anything wawe na mahala pa kuanzia.
 
upendo gani wa kujeruhiana?? ni mshamba tu na udhaifu unamsumbua, pia hajiamini
Huyu jamaa anampenda sana mkewe kiasi kwamba anakuwa na wivu wa kijinga, na tunaomfahamu huyu dada hapa ofisini hana tabia anazomzania labda huko mtaani kwao...mimi kinachoniuma ni huyu dada ikivunjika ndoa yake ilihali hana kwasababu yangu na akiwa hana uhusiano wowote na mimi
 
Ninavyoona mimi hapo, huyo mwanamume alikua anatafuta sababu tu ya kutengana na mkewe. Kama anatambua nature ya kazi ya mkewe hakupaswa kufura kwa hasira hivyo, kwani mtu anayeiba mke wa mtu hawezi piga simu in late hours.

Angekuwa ni mtu mwenye busara angekubari nionane naye tuzungumze, nijuavyo mimi mtu anaweza akakumegea na hata ukimgundua anaendeleza jeuri hilo hajalifahamu, labda anasababu zake zingine
 
Huyu jamaa anampenda sana mkewe kiasi kwamba anakuwa na wivu wa kijinga, na tunaomfahamu huyu dada hapa ofisini hana tabia anazomzania labda huko mtaani kwao...mimi kinachoniuma ni huyu dada ikivunjika ndoa yake ilihali hana kwasababu yangu na akiwa hana uhusiano wowote na mimi
Kaka huyu dada ndoa yake ikivunjika hatakulaumu wwmatamlaumu mumewe,coz kwa maelezo hayo,kosa lako liko wap?na dada naye angekuambia kuwa usiwe unampigia simu nyumbani kwao!
 
Tatizo wanaume wazinzi ndo wanakuwa na wivu wa kiivyo, anazani anavyofanya yeye kwa wake wa wenzie ndiyo yanafanyika kwa mkewe!
 
i hate men who are so abusive!!! kama anamwona mkewe si mwaminifu si amwache?? vipigo vya nn?? angejua ukweli wa story yote si kukimbilia kumpiga mwanamke eti kwakuwa ni weak na hawezi pigana naye....wat a coward.....

Kwa gentleman makini asingekataa mimi kuonana naye face to face
 
Mimi nadhani hutakiwi kukaa kimya, cha msingi waendee au watafute wazazi wa mume na uwaeleze ishu imekaaje na wao wakusaidie kuzumngumza na mtoto wao. Kama si hao anaweza akawa shangazi yake au ndugu yeyote anayemuheshimu. Wakati unayafanya haya hakikisha mke wako anajuwa unachofanya na mwisho wa siku mkutanishwe wewe, mkeo, jamaa na mkewe pamoja na ndugu wa mume alitakayehusika kuanza kuongea na huyo jamaa
 
Ila inaniumiza sana, nimejifunza kitu kikubwa sana hya mambo ya wivu

kawaida ya watu wenye hasira hivi hujirudi baada ya hasira kuisha hata baada ya siku 3 wewe cha kufanya hata kama huyu dada anakuja kazini wacha kudiscuss nae na kama mlikuwa mnaenda wote lunch acha kuanzia leo yaani sio uwe adui yake ila ikilazimu muongozane na mtu mwingine zaidi yenu 2 yaani msiwe wawili tuu kikazi maana anaweza anza uchunguzi wa kumfatilia mkewe kazini na akijua mnakuwa bennet muda wa kazi atakonclud kingione ambacho siyo.
Najua ofisini kuna utani mwingi sana watu wanataniana ila kaa nae mbali kwani ushamjua mumewe ni mtu wa aina gani. Kuwa nae kikazi zaidi, socia muachie mume wake.
 
Sikulaumu na pia sikutetei....kuna mambo ambayo tunapaswa kuyawekea tahadhari toka mwanzo hasa tunapokuwa tunawasiliana na wake/waume za watu ..Na wewe inaonyesha uli-mess up from the day go..mfano hata wewe ukijiweka kwenye nafasi ya huyo jamaa ..afu mtu unayemhisi ampigie simu mkeo ..asiongeee..lolz..nahsi utaona ambavyo ni ngumu sana kuaminika kirahisirahisi...

La kwanza jifunze namna bora ya kuishi na mke wa mtu hata kama mnafanya kazi pamoja (distancing)...La pili, kuhusu hili jambo kama una mke mshirikishe kwanza ili ajue kilichokutokea na hata likitokea la kutokea akupe support (manake unaweza kupoteza huku na kule)..Then, usifanye mawasiliano yeyote na huyu dada..hell no...naaamini kama hamkuwa na kitu chochote the truth will set you free..........................
 
Wadau mwenzenu nipo kwenye wakati mgumu sana psychologicaly, kuna dada anataka kuachika kwasababu yangu ilihali hana kosa lolote....Ishu iko hivi Kuna dada(mke wa mtu) nipo naye karibu sana kikazi, siku asipokuwepo ofisini kuna baadhi ya kazi zake hunachia nimsaidie namimi nisipokuwepo ofisini naye hunipa ushirikiano wa hivyo kutokana na nature ya kazi zetu kufanana sana.

Kutokana na ukaribu huu mmewe alianza kuwa na wasiwasi namimi, kwasababu kuna siku nilimpigia simu mkewe akapokea yeye bila hata kujibu salamu yangu akaniuliza shida yangu ni nini? mimi nikamueleza kwamba shida yangu ni ya kikazi nataka kuongea na mkewe,..... kumbe alikuwa naye jirani akampatia nikaongea naye, yalikuwa ni masuala ya kikazi tu yaliyohitaji ufafnuzi wa sekunde chache tu alafu zilikuwa ni saa za kazi, ishu ni kwamba huyu dada na mmewe walikuwa likizo.

Hivi majuzi huyu dada aliwahi kidogo kutoka ofisini kwasababu alikuwa anawahi kumpokea mmewe Airport alikuwa ametokea nje ya nchi kusimamia matibabu ya ndugu yake, all the way kwenda airpot na kuelekea nyumbani kwao tukawa tunawasiliana na huyu dada kuhusiana na vikazi alivyoniachia pale kazini nimsaidie mpaka nilipomaliza mida ya saa2 usiku.

Nikiwa nyumbani mida ya saa4 usiku mwanangu wa miaka3 alichukua simu yangu ikiwa chumbani mimi nikiwa sebureni akawa anaichezea, kwa bahati mbaya akapiga simu kwenda kwa yule dada ikapokelewa na mmewe kila akiongea simu yangu ilikuwa kimya maana alikuwa anaichea mtoto na hakujua kama kapiga simu. baadaye kidogo akapiga yeye, mwanangu akaniletea simu nilipoipokea kumbe ni yule bwana anapiga akaniambia maneno machache tu "HAJAKWAMBIA KWAMBA NIMERUDI? KUANZIA SASA NIMEKUACHIA" nilipojaribu kutaka kujua zaidi nini kinaendelea akanikatia simu, kila nikipiga simu ikawa haipokelewi, kwenye mida ya saa6 usiku akapiga yule dada akiwa amepigwa na kahifadhiwa kwa jirani ndipo nilipogundua nini kilitokea, nimejaribu kumuomba huyu jamaa tuonane tuongee ameniambia nikae mbali naye.

Wadau naombeni ushauri nimsaidieje huyu dada ili kuokoa ndoa yake maana jana amerudi nyumbani kwake lakini mmewe hamsemeshi kitu chochote, akijaribu kumuelewesha anamuambia aje kwangu yeye hataki kuishi naye, najisikia vibaya sana kwasababu mimi ndiyo chanzo na naofia maisha yangu kujisogeza kwenda kunusuru hii ndoa.

Tafuta watu wazima 2, anaweza kuwa mchungaji wako au boss wako wa kazini. Nenda kaongee na huyo Bwana uso kwa uso kwa lengo la kunusuru ndoa ya huyo DADA.

Sio wanaume wote wana busara, kumbuka hadithi ya Nabal na Abigail vs Daudi.
 
Back
Top Bottom