Nauza suzuki escudo 5 doors sh. 8.2 ml

POLITIBURO

Member
Apr 21, 2012
41
6
Wana JF nawasalimu. Ninauza gari Suzuki Escudo milango 5 kwa Sh. 8,200,000/=. Gari liko Dar, lina hali nzuri na linatembea. Kwa mwenye kuhitaji tuwasiliane.
 
Toa particulars zilizoenda shule mkuu, kutembea kwa gari sio issue kwani hata kwenye mtelemko linaweza kutembea hata kama injini haipo.
 
Yaani hapo tangazo ndo limekwisha? Watu wanauliza maswali, majibu hakuna, mwe! Kibiashara bado tuko mbali na tuendako.
 
Gari ni AUTOMATIC, lina CC 1990, limetembea km 49,000 na ni la mwaka 1995. Kwa mwenye kulihitaji tafadhari ni pm tupeane details zaidi. Asanteni
 
Wana JF nawasalimu. Ninauza gari Suzuki Escudo milango 5 kwa Sh. 8,200,000/=. Gari liko Dar, lina hali nzuri na linatembea. Kwa mwenye kuhitaji tuwasiliane.

Gari ni AUTOMATIC, lina CC 1990, limetembea km 49,000 na ni la mwaka 1995. Kwa mwenye kulihitaji tafadhari ni pm tupeane details zaidi. Asanteni
Mzee,
Biashara yako hii inatia mashaka, si uwasikilize wateja watarajiwa wanachoomba hapo juu?
 
Weka picha. Unaogopa nini?
Hata kama hutaki namba zionekane unaweza kuziba eneo la number plate.

Kwa maelezo uliyoyaweka, bado hayamshawishi mtu kuwa mteja wako.
 
Gari ni AUTOMATIC, lina CC 1990, limetembea km 49,000 na ni la mwaka 1995. Kwa mwenye kulihitaji tafadhari ni pm tupeane details zaidi. Asanteni
hii gar inawezekana ilikuwa yadi au gereji kwa mda mrefu sana.
gari ina umri wa miaka kama 17
Imetembea km elf 49, kila mwaka inatembe km 2,800 tu

(Inawezekana imetembea km 149,000 Nashawishika)
 
hii gar inawezekana ilikuwa yadi au gereji kwa mda mrefu sana.
gari ina umri wa miaka kama 17
Imetembea km elf 49, kila mwaka inatembe km 2,800 tu

(Inawezekana imetembea km 149,000 Nashawishika)
Umeongea fikra zangu zote, huyu bwana anasumbua akili za watu humu jamvini, nimeona hapo juu wana JF wameshauri alete picha hataki, badala yake analeta uongo wa "odometer" readings kama huo akifikiri humu ndani kuna malimbukeni wa magari kama yeye.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom