Nauza Strawberry

Nauza Strawberry

mzalendo-wa-tz

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2014
Posts
404
Reaction score
187
Nina shamba langu la strawberry na mbogamboga zingine Morogoro. Kama upo tayari tuwasiliane nikuuzie Strawberries kwa jumla nawe upate faida ya kuendeleza mipango yako ya maisha.

NB: Kwa sasa Strawberry ni zao adhimu na kama utafanikiwa kupata soko la uhakika ndani ya mwaka mmoja utakuwa umepiga hatua si haba.

Bei ya rejareja kwa wastani (Soko la kisutu n.k) 1kg huuzwa Tshs. 5000. Mimi nitakuuzia kwa 4000 kwa KG na kama utanunua zaidi ya 100 ninaweza kukupunguzia kiasi fulani. Karibu sana tuendeleze fursa za kilimo
Emmanuel Fidelis Mgimwa (+255 765 452 928 (Whatsapp) au +255 713769013)
 
swali tafadhali, hivi hizo huwa zinadumu kwa muda gani pasipo kuharibika? je nikichukua zikachelewa kuisha,

hazitaharibika? na je nikitaka kg 25 tu ili nianzie kwanza utanipa? vp kuhusu usafiri? imekaaje? mi nipo Dar nahitaji ila

nipate majibu ya hayo maswali kwanza. please nipo serious ndugu.
 
Kama ukiwa na fridge zinaweza kudumu kwa siku 2 hadi 3 au zaidi (naamini huwezi kaa nazo muda wote huu bila kuuza) lakini kama hauna fridge zinaweza dumu kwa siku moja hadi mbili kutegemeana na uhifadhi (handling). Kama ukizingandisha kwa ukavu ( dry frozing) zinaweza dumu muda mrefu zaidi.
Usijali utapata hizo kgs unazohitaji, kuhusu usafiri mimi nitakuletea mzigo mpaka Dar (ulipo) ambapo baada ya kukabidhiana tutafanya malipo.
 
asante, sasa mimi nazitaka mwisho wa mwezi huu, bila shaka kwa hizo kilo kg ni Tsh. 100,000, kwa mujibu wa

maelezo yako. ila tu nahitaji kwenda kuongea na wafanyabiashara hapo Kisutu na K/koo ili niwe na uhakika wa kuuza,

we ukileta tu mi nauza moja kwa moja.

jibu nitakupa nimechukua hiyo namba hapo juu.
 
Usijali mkuu, tuwasiliane ukiwa tayari,
 
Nina shamba langu la strawberry na mbogamboga zingine Morogoro. Kama upo tayari tuwasiliane nikuuzie Strawberries kwa jumla nawe upate faida ya kuendeleza mipango yako ya maisha.

NB; kwa sasa Strawberry ni zao adhimu na kama utafanikiwa kupata soko la uhakika ndani ya mwaka mmoja utakuwa umepiga hatua si haba. Bei ya rejareja kwa wastani (soko la kisutu n.k) 1kg huuzwa Tshs. 5000. Mimi nitakuuzia kwa 4000 kwa kg na kama utanunua zaidi ya 100 ninaweza kukupunguzia kiasi fulani. Karibu sana tuendeleze fursa za kilimo
Emmanuel Fidelis Mgimwa (+255 765452928 (whatsapp) au +255 713769013)

Kumbe Ni Strawberry Tunda Mimi Nilidhani Ni Nanihiiiiiiiiuuuuuuuu...................!
 
aiseee ni zao zuri ila uhakika wa kuliuza au kupata masoko yake ndo shida

hizo zao linafaaa kutengeneza juice? linatumikaje maana wengine hatuwawahi kula
 
aiseee ni zao zuri ila uhakika wa kuliuza au kupata masoko yake ndo shida

hizo zao linafaaa kutengeneza juice? linatumikaje maana wengine hatuwawahi kula

Keki nyingi za gharama kubwa hupambwa kwa strawberry .... fruit salad kwenye mahoteli makubwa huwekwa tunda la strawberry .... ice cream nyingi kwenye ice cream parlour and shops huwekwa tunda la strawberry .... vinywaji vingi ikiwemo maziwa fresh na mtindi huwekwa ladha halisi ya strawberry .... kama ulivyouliza tunda hili hutengeneza juice nzuri sana kwa kuchanganywa na tikiti maji (strawberry and water melon juice blend) .... hivyo basis utaona umuhimu Wa zao hili .... ni tunda kama matunda mengine

wahindi wanayapenda sana ..... Kwasababu gani mmi sijui
 
aiseee ni zao zuri ila uhakika wa kuliuza au kupata masoko yake ndo shida

hizo zao linafaaa kutengeneza juice? linatumikaje maana wengine hatuwawahi kula

Ni kweli, ila ukipata soko ni zao zuri. Strawberry unaweza tengeneza juice (ni tamu sana) lakini pia unaweza tengenezea jam na hata kuifanya kama kiungo cha salad.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom