Natadhaharisha tu watu hii saloon ni nzuri kweli kama inavyoonekana ila napata mashaka kidogo maana Saloon ikuingizie uhakika wa 60,000 per day uhakika hiyo halafu uiuze??? nawasi wasi Muuzaji utakua ulipewa kama MSIMAMIZI wa saloon na wala saloon sio yako.
Ndio mana hata KODI hajaimalizia anataka aiuze halafu akimbie,siku mwenye saloon akija Ndio balaa litakapoanza upya,na kwa kusoma soma tu Mwenye saloon ndio huyo jamaa mwenye safari za nnje anaepiga mi dollar so huyu msimamaizi TAMAA imemwingia au ametibuana na boss wake ameamua kuiuza saloon.
Kwa mnunuaji kama ndugu yetu
Saint Ivuga nakushauri ukitaka hiyo saloon inunue ila usifanyie biashara kwenye hiyo frem,ONDOKA na vitu vyako KODI iliyobaki tafuta mpangaji pangisha kula kodi yako.
Muuza saloon huyu nina mashaka sana kama ndio mmiliki halali wa hii saloon...Kuna kibosile huko hajui kama biashara yake huku inapigwa mnada..yeyote atakae itaka hii saloon AENDE NA TAHADHARI 100% Andikishianeni hadi vitana na powder. mbele ya serikali ya mtaa team nzima OTHERWISE akija huko BOSS mwenye saloon ambae hatumjui Unaweza jikuta wewe mnunuaji unalala sero bila kujua.
Watu wanatafuta hela kwa shida ndugu zangu,arudi alafu akukute umwambie kirahisi tu NIMEUZIWA SALOON HIII bwana bwana waulizeni TISS walichofanywa na ZACHARIA walipomfata ofisini kwake.