Nauza chumba cha kufanyia biashara Katoro-Geita

Jack_tshirt_point

New Member
Mar 11, 2024
4
1
Leo nimewaletea uzi kuhusu biashara ya nguo hasa za kiume,hii ni biashara nzuri sana endapo utaifanya kwa umakini na ina faida kubwa. Mimi nimefanya hii biashara nafkri ni zaid ya miaka 10 sasa kwahy nina uzoefu mkubwa sana,mambo kadhaa kufahamu kabla hujaanza kufanya biashara hii ni;

1. lazima ufahamu vizuri wapi utapata mzgo yaani kujua utakapo pata mzigo mzuri na bei nzuri,hasa kariakoo bila kuijua vizuri utajikuta unanunu kwa machinga ambao nao wanakaba humo humo afu nawao wanauza,kwahy bila kuwa mkini utajikuta unadhani umenunua jumla kumbe umenunua rejareja umepigwa matokea yake wewe unapoenda kuuza hutapata faida nzuri,kwahy kabla hujaanza biashara jitahidi ufanye research vizuri wapi ntapata mzigo.

2. Ni Location, sehemu yakuweka biashara hapa inabidi utulize kichwa vizuri,wengi huwa wanaogopa kutoa pesa nyingi kununua site (Chumba cha biashara) huwa wanaogopa kutoa ela nyingi na badala yake huwa wanakimbilia kwenda kwenye site ambazo zina bei ndogo, kupata site inategemea na maeneo kuna maeneo mengine kupata site hadi umtoe mtu yaan umnunue ndo akupishe au maeneo mengine utapata kwa kulipa kodi tu kwa mwenye site,sasa inatakiwa uhakikishe umefanya research vizuri kabla hujachukua chumba cha biashara maana hapa ndo wengi huwa wanafeli hata kama unamtaji kiasi gani ukichemka hapo mtaji wote utafia hapo.

3. Ni kufanya research ya aina ya watu walio karbu na biashara yako,mfano unaweza kuweka duka la nguo labda ni ushahilini afu ukawa unawapelekea nguo ambazo ni za watu wa maofisini hutapata wateja, inatakiwa upeleke nguo kulingana na watu wengi ni wa aina gani.

4. Hii ndo ya mwisho ni mtaji jamani mtaji haunaga kiwango ni kulingana na mtu unataka kufanya kwa ukubwa gani, ila kwa kukusaidia kama unaanza biashara ya nguo kwa kiwango cha kati syo cha juu sana wala siyo cha chini sana, ukiwa na milioni 5 unaanza hapo utaigawa vizuri, na ukiwa umeifanyia kazi point namba 3 utakua ushajua aina ya watu walio kuzunguuka mfano kama ni vijana lazma ujikite zaidi kwenye jinsi,tshirt na utaweka kidogo vitu vya watu wa maofisini mfano kadeti kidogo shati milioni 5 inatosha.

Jamani kwa yoyote anaehitaji ushauri asisite kuuliza, pia kwa anae hitaji chumba cha biashara kipo nakiuza hiki changu kipo katoro mkoa wa geita kipo sehemu nzuri sana unauza jumla. Katoro ni sehemu nzuri sana ya kujitafuta kwahyo napauza mimi nataka niende huko kariakoo nikapambane na matajiri.nichek kwa namba 0678295060
 
Back
Top Bottom