Naunga mkono zoezi la Bomoabomoa

kISAIRO

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,796
654
Ndugu zangu,

Kumekuwa na kilio kikubwa kuhusiana na bomoabomoa inayoendelea hapa nchini, kilio ni kutoka kwa walalahoi mpaka kwa wemye nacho.Mimi kwa maoni yangu naunga mkomo asilimia 100 na bomoabomoa zinazoendelea.

Nchi ili iendelee ni lazima tuheshimu, kutii na kufuata sheria, nchi haiwezi kundeshwa kwa kelele, hivyo basi ni vizuri bomoabomoa ikaendelea na tena kwa kasi na ari ya kiwango cha juu sana.

Ili tuendelee lazima tufuate sheria.
 
Last edited by a moderator:
Wahi na tingatinga Jangwani, mradi wa Dart umewekwa xx.
Toa msisitizo ili sharia iheshimiwe pia.
 
Kama ni suala la kuvunja sheria si hao wanavunjiwa pekee ndio waliovunja sheria. Wakati hizo nyumba zinajengwa mamlaka husika zilikuwepo na hazikuchukua hatua yoyote kwa hiyo huo ni uzembe wa wahusika kushindwa kusimamia sheria. ilitakiwa hawa watu nao wabomolewe kwanza, hapo ndio tungeona kweli sheria zinafuatwa.
 
Wanasheria wanasema kutokujua Sheria hakuhalalishi kosa, unajenga kwenye Mikoko unategemea nini?unajenga open space unategemea nini?kuoneana aibu Ndio kunakotukwamisha
 
Kama ni suala la kuvunja sheria si hao wanavunjiwa pekee ndio waliovunja sheria. Wakati hizo nyumba zinajengwa mamlaka husika zilikuwepo na hazikuchukua hatua yoyote kwa hiyo huo ni uzembe wa wahusika kushindwa kusimamia sheria. ilitakiwa hawa watu nao wabomolewe kwanza, hapo ndio tungeona kweli sheria zinafuatwa.
Umejenga eneo la wazi kuna mjadala hapo?
 
nilifundishwa na mama yangu nisifurahie matatizo ya mwingine
 
Back
Top Bottom