kijana wa leo
JF-Expert Member
- Nov 28, 2011
- 2,916
- 7,164
Ndugu zangu Watanzania,
Unajua sio kila jambo ni la kulalamika, serikali zote Duniani zinahitaji uungwaji mkono na kukubalika kwa wananchi wake mbele ya mataifa mengine. Sasa kwa sisi Tanzania tumejijengea kautaribu ka kulalamika kila siku bila kutimiza wajibu wetu kisheria na kikatiba.
Leo taongelea zaidi swala la kujiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi wa seeikali za mitaa, asilimia yetu kubwa hatujajiandikisha kwa makusudi tu tena bila hata sababu yoyote ya msingi, na wengine waandikishaji walikua mbele ya nyumba zao lakini walishindwa kujiandikisha bila sababu yoyote.
Kwa uelewa wangu, moja ya vitu vinavyochangia maendeleo na ustawi wa uchumi ni pamoja na chaguzi zinapoenesha raia wengi kushiriki katika hizo chaguzi, hiyo inavutia mataifa mengi na wawekezaji, sasa kwa serikali yoyote ile yenye nia ya kuleta maendeleo ya kweli ni lazima itahakikisha hii taswira haipotei mbele ya uso wa Dunia.
Hivyo kama ni kweli serikali imeongeza majina hewa ili kufanya idadi iwe kubwa, mimi naunga mkono huo mpango kwa asilimia 💯 mana una nia njema kwa ajili ya maendeleo yetu na kujenga imani kimataifa.
Kama sisi wenyewe hatutaki kujiandikisha bila sababu yoyote ya msingi, tunailaumu vipi serikali kuongeza watu? Kuna wajinga watasema sababu ni uchaguzi kutokua wa haki, tuongee ukweli, Tanzania kuna chama chochote cha siasa chenye miundombinu na rasilimali watu wa kuongoza nchi?
Mfano majimbo mengi ya uchaguzi vyama vingine vimekosa hata wagombea, sasa chama kinachokosa hata wagombea kitawezaje kuongoza nchi?