Naunga mkono hoja ya kuimarisha mifumo ya nchi

Naunga mkono hoja ya kuimarisha mifumo ya nchi

Escrowseal1

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2014
Posts
4,795
Reaction score
4,849
Mtindo wa sasa wa mambo miradi inayofanyika inategemea maamuzi ya mkuu wa nchi ni hatari Sana na inatujengea utamaduni mbaya kama nchi.

Kuna maeneo ya nchi hii kama Rais Hana mzuka nayo inakuwa bahati mbaya Sana kwao. Nitatoa mfano mmoja Kwa sasa mkuu anapenda kuona Jimbo lake linapaa na Kwa sababu hiyo baadhi ya majimbo yana hasa majirani zake yana suffer comparative disadvantage .

Juzi tulishuhudia utiaji saini mradi wa mgodi mkubwa wa mabilioni ya pesa Ila Kwa kuwa ni ngumu ku balance ama kuwa fair Kwa ajili ya priority Kwa kila eneo bali matakwa, walibebwa wananchi kadhaa sijui Kwa kigezo gani kwenda kushuhudia utiaji saini ati makao makuu ya mkoa. Jimbo uliko mradi halieleweki eleweki japo si mbali na Jimbo linalofanywa la mkakati Kwa kuwa anatoka mkuu wa nchi. Ila kiuhalisia nalo Kwa umuhimu wake lina umkakati wake kama likipata kiongozi atakaelitambua kwani.

1. Liko mpakani mwa nchi mbili
2. Lina mgodi mkubwa uliozinduliwa
Kwa majirani
3. Ni kati ya majimbo kongwe tangu enzi za mkoloni hadi mkoloni
Kuandika kitabu kinacholihusu. The lost mandate East Africa

So, kila eneo Kwa utetezi wake kama linae mtu wa kulitetea ni strategic. Watanzania hatuwezi kuwa tunarundika resources sehemu moja Kwa kigezo cha kuwa mkakati. We need to balance ili wote twende Sawa. Jimbo halina maji, barabara na ambayo inasafirisha mizigo kwenda nje ya nchi inatia aibu sehemu ya mwendo wa Saa itachukua masaa matatu yet hata kampeni mkuu hakukanyaga Bali alibeba wajumbe kwenda makao makuu ya mkoa. Makao makuu kilometer lukuki. sababu katibu mkuu anatoka huko, unfair dealing ina impact mbaya kabisa for generation.

Tanzania ijikite kujenga mifumo imara
1. Mifumo itakayohakikisha wizi wa rasilimali unakoma na kuwa historia na ambayo haitegemei mkuu wa nchi kuwa mkali ndo wizi ukome.

2. Mifumo itakayohakikisha rasilimali zinakuwa shared kutokana na uwezo Ila pia na uhitaji na si mpaka Rais atamke hiki na kiwe ndo kinakuwa

3. Mifumo itakayohakikisha makusanyo yanafanyika bila nguvu ya mtu mmoja kwani hatujue kesho atakuwa nani anaamua.

Mwisho haamini bandiko linalohusu kuhawana keki ya Taifa kwa usawa bila utashi wa mtu langu si la Kwanza na itambulike ufukapo Moshi basi Pana Moto.
 
Back
Top Bottom