Naunga Mkono Bunge Kutoonyeshwa Live

Naunga Mkono Bunge Kutoonyeshwa Live

Sasa ni bora ikawa live ili kama ni matusiJ
Sasa ni bora ikawa wazi ili kama ni matusi na upumbavu mwingine usikike ili tujue kabisa nani mpumbavu na nani anajielewa kuficha ujinga sio kuutatua Bali ni kuulea na anayefucha ni mpumbavu zaidi ya yule anayefuchwa hawa wabunge watajuja kugimbea urais baadae sasa ni bora tukaijua hali halisi ya tabia zao
 
Naunga mkono hatamie
Hawa wabunge wetu wengi wanapenda kuonwa wakifanya mambo ya hovyo bungeni
Inakuwa kama mtaji wao kisiasa
Na mawaziri wanaozunguka na vyombo vya habari je?? Hadi mtu anafunga geti asubuhi na vyombo ya habari..!
 
Mambo ya hovyo yanakuwaje mtaji wa kisiasa? Pumbaf sana
Wanawaonyesha wazazi wetu wakiwa wameuchapa usingizi bungeni mpaka wajukuu wanawaona wanaanza kusema babu alikuwa amelala kule kwenye ile nyumba ya Dodoma.

Tumeamua kufuta Live show
 
Kama government inaokoa millions of TZSh kwa kupunguza muda wa kurusha live matangazo toka bungeni .Ni jambo zuri ,hizo pesa zinaweza zikatumika kwenye masuala mengine muhimu kama kujenga madarasa ya shule zetu . Suala la kurusha porojo za bungeni kwa kutumia kodi zetu sikubaliani nalo.
 
kwa hili sikubaliani na wewe kamwe. yaani rais aoneshwe live halafu wawakilishi wa wananchi wasioneshwe live. kamwe....
 
kwa hili sikubaliani na wewe kamwe. yaani rais aoneshwe live halafu wawakilishi wa wananchi wasioneshwe live. kamwe....
Lazima ujue tofauti kati täya Rais na wawakilishi then upinge unachokipinga. Coverage ya Rais niya some minutes lakini ya bunge ni zaidi ya masaa tisa kwa siku . So wewe mwenywe unaweza chambua
 
Sasa ni bora ikawa wazi ili kama ni matusi na upumbavu mwingine usikike ili tujue kabisa nani mpumbavu na nani anajielewa kuficha ujinga sio kuutatua Bali ni kuulea na anayefucha ni mpumbavu zaidi ya yule anayefuchwa hawa wabunge watajuja kugimbea urais baadae sasa ni bora tukaijua hali halisi ya tabia zao

TCRA na sheria za utangazaji haziruhusu kurusha matusi hewani yawe ya bunge nk.Kuthibiti hilo hatua mojawapo ni ya kutorusha live wabunge wakijadili.Chombo kikirusha tu matusi chaweza fungiwa.Sasa akiwapo mbunge anayetaka chombo cha habari kifungwe aweza poromosha matusi bungeni makusudi ili chombo kinachorusha live kidakwe kifungiwe.

Kuzuia kurusha Live ni pamoja na kudhibiti wabunge warusha matusi wasiviletee shida vyombo vya habari.

Lakini pia matusi yanaharibu Jamii hasa watoto.Bunge linatazamwa na watu wa rika zote sasa ukiachia Live wakaanza wengine kuporomosha matusi humo bungeni wanaharibu jamii na ustaarabu wa watu.Kudhibiti hilo pia ndio maana inatakiwa kuhariri kwanza na kurusha baadaye yale tu yenye maaadili kwa nchi.
 
vp kuhusu mwenge..? ambao kiukweli hauna faida ..haujawahi kuwa na faida na hautakuja kuwa na faida kwa taifa ...nao mnasemaje?
 
Watz tunapoteza zaidi ya sh. bilioni 400 kwa ajili ya foleni Dar. Ongeza thamani ya masaa kazi yanayopotea kwa kuangalia bunge live nchini kote, inasikitisha. Uamuzi wa kujenga flyovers na kutoonyesha bunge live naamini una tija kwa uchumi wetu. Watz tuwe kikazi zaidi, tuache blah blah. Hapa kazi tu.
 
WE KILAZA KWELI,, SO WE UTAJUAJE KM MBUGE WAKO ANATETEA MAENDELEO JIMBONI KWAKO BILA KUANGALIA BUNGE.
Mkuu si utaona mabadiliko jimboni kwako?barabara zikijengwa, umeme ukiwekwa,maji yakiwekwa n.k.

Wabunge kwa utaratibu wa kwetu sio wawakilishi tu bali pia wanapaswa wawe na uwezo wa kulobby kuleta mipango ya serikali majumbani.Hatutaki wale wanaoishia kupiga domo tu na matokeo hayaonekani.Hawa ndio wataumia kwenye utaratibu huu.
 
Kuna wabunge hawawezi kazi kabisa ila wanajua kupangilia maneno kweli. Wanaishi tu kwenye siasa za live bungeni kwakuzungumza mambo mazito kweli kweli na baadhi ni mahodari wa kudandia Hoja za wenzao.

Ukienda Jimboni kwake wananchi wake wanaishi kwenye dimbwi la umasikini, Hawa wabunge hawajitumi kabisa.

Hawaanzishi vikoba, Hawaanzishi miradi ya manufaa kwa wananchi wao,wana diplomatic passport lakini hwatafuti wafadhiri. Hebu tuwadhibiti kabisa waanze kufanya kazi Majimboni.

Napeeeeee futiilia mbali mbali mambo live wabunge wawe wanashinda kwa wananchi wakiwahudumia.
Hoja yako ni dhaifu hata mwanangu wa darasa la tano anakushinda. Hivi unafahamu kazi za bunge wewe zuzu? Hivi bunge kutokuwa live ni nani anafaidika ? Kuwa na watanzania wewe ni biashara ya watumwa ingerudi tungekubalisha hata shanga.
 
Hoja yako ni dhaifu hata mwanangu wa darasa la tano anakushinda. Hivi unafahamu kazi za bunge wewe zuzu? Hivi bunge kutokuwa live ni nani anafaidika ? Kuwa na watanzania wewe ni biashara ya watumwa ingerudi tungekubalisha hata shanga.

Kama ni hili la kwako basi kuna wabunge hawajui kazi zao. Hasa marehemu Deo Filikunjombe na wabunge wengi tu kama Mkono pia hawajui majukumu yao ya kibunge.
 
Hapa kazi Tu.!
de8ca0fed9fc7c76bbdc0a3140de6de2.jpg
 
Watuonyeshe tu wenye nafasi waangalie wakazini wahadithiwe na chokochoko zipate sehemu ya kutolewa. Bila kukubali kukosoana hadharani madhara yake ni kujenga ugaidi wa chinichini tukakosa maendeleo. Kwani mipango ya serikali iwe hadharani au kificho ikosolewe au isikosolewe nchi inakwenda. Bado sisi ni wachanga tunahitaji kujifunza kwa walioendelea.
 
Wewe jamaa ni kilaza, unajua kazi za mbunge wako?hilo ni jukumu la serikali, bunge kazi yake ni kuhakikisha serikali inayatekeleza haya, sasa kama Bunge likiminywa na kushindwa kuibana serikali maumivu ni kwa wananchi
Mkuu huyo kulingana na post yake anaishi dunia nyingine,dunia ya kusadikika akisha jidunga ng'ada tayari anajiona yuko kwa malkia au kwa obama!
 
Back
Top Bottom