Naumwa sana na kichwa

Ushirombo

JF-Expert Member
Jan 22, 2013
3,557
2,692
Jamani mi nasumbuliwa na kichwa kinauma sana tena frequently kinaweza kuacha kwa mud a tu, shida iko hivi nikitembea juani kwa dakika 25 nitaumwa kichwa sana,pili nikiwasha computer hasa kama chumba kinagiza kwa dakika 45 tayari kichwa kinachemka,misuli inasimama kinauma mbaya.

Na pia unaweza kujikuta pua kama haivuti hewa ya kutosha yaani mfano ninapolala chali pua inakuwa kama imeziba, so naanza kupumua kama kwa shida hali hyo pia hunifanya kichwa kuuma sana.

Tiba nilizojaribu so far nilienda CCBRT wakanipa miwani yakupunguza miale ya jua transition, lakini shida iko pale pale, kuhusu pua kama kuziba huwa nikipigà chafya napatà nafuu kwani naona mfumo wa upumuaji unaachia na kichwaà kinapoa,au nameza panadol pain killer na kutafuna PK.

Nahitaji ushauri wenu.
 
Pole sana mkuu jitahidi unywe maji kwa wingi. Kama bado jaribu na upande wa pili (sawa za kienyeji), kama wewe ni mlokole ama msabatho basi kapinge kambi kwa mchungaji maana hamna namna tena.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom