Naumia sana; nifanyeje?

Pole sana jamani umeandika kwa uchungu sana.
Karibu chama la mabachelor.
Hivo vya kawaida sana within time mambo yatakua sawa.

Ila msiwe mabachelor sugu tuu!
 

1) Sijawahi kusikia mwanamke anakubali kuwa yeye ana michepuko.
2) Unakutana na mwanaume mwingine mtu mzima(hence sugardaddy) akupe pesa tena sehemu ya kunywakunywa? baba ako huyo?
3)Kama kulikuwa hakuna kinachoendelea nyuma ya pazia kati yako wewe na huyo named sugardaddy, kwa nini useme ni bahati mbaya kuna mtu wa karibu na bf wako alikuona?
4)Alikupenda sana na ulimuumiza sana ulipokuwa nae, sasa na yeye anajaribu kukufanya na wewe uumie. Hii inanipa picha kwamba wewe ulikuwa ni mtu wa michepuko na ma-sugardaddy au na wanaume ambao hawawezi kukuoa, pengine ulikuwa unanufaika na hiyo michepuko kwa hali au mali, halafu huyo bf wako ulikuwa unadhani umemu-handle vizuri hivyo hawezi kukuacha.
5) Uliumia sana baada ya kusikia kuwa anaoa kwa sababu wewe ndio chanzo cha sababu ya uhusiano wenu kuvunjika.
6)Uliweza kumsubiri arudi kwako huo muda wote wa mwaka mmoja na nusu kwa sababu ulikuwa na uhakika kuwa jamaa hana pa kwenda lazima atarudi kwako tuu kwako na ulikuwa unaendelea na wanaume wengine kama kawaida(unless utuambie ulikuwa hubanduliwi muda wote huo), na inawezekana ulishamfanyia vituko mara kadhaa akawa anaondoka halafu anarudi, hivyo ukawa unaamini lazima atarudi.

Hakuna mwanaume ambaye atahimili kirahisi kuona/kusikia demu/mchumba wake amekutana kisirisiri na jamaa ili achukue hela labda huyo mwanaume awe Marioo. Iwe fundisho ujue jinsi ya kuishi vizuri na utakayemchagua next.

HATA HIVYO POLE MWAYEGO.
 

Ehh ndugu nashukuru kwa kuchukua muda kuandaa thread hii. Kweli kabisa upande wa pili hauwezi kuona hilo swala kuwa genuine.
Kuhusu kukutana naye huyu mtu sijakataa na tena huwa nimekutana naye mara nyingi huko nyuma na hata sasa. Sio sugadaddy wangu na hajawahi kuwa michepuo. Hili ndio lilinitatiza sababu nilisikiza hoja za mwenzangu akiwa na hasira nikaona kwa upande wake zilikua zinaleta maana. Japo ilinibidi kuomba msamaha la kwenda mahali pale bila kutoa taarifa.

Yeah nilisubiri na sijawahi kuwa na mtu sababu sex was never a priority kwangu. Ndio hivyo haikuwa bahati yangu. Najua ni mimi nilichangia zaidi kwenye kuachika kwangu ila ukweli ni kwamba naumia na nahitaji kusahau tena kwa upesi.
 
kwanza pole saana, mimi nilichoelewa hapo huyo uliyekuwa naye hakuwa chaguo sahihi kwako/kwake
nadhani ni kama alikuwa anatafuta sababu tu ya kukuacha na alikuwa na wewe kama kimada (bila ya malengo)

ushauri wangu ni kujaribu kusahau tu!!

Huwezi amini hata mimi Nimepewa taarifa na aliyekuwa mpenzi wangu kuwa anaolewa mwezi wa 7 mwaka huu hata mwezi haujapita!! nimekubali matokeo na kujitahidi kujisahaulisha tu!!
 
Ulifanya kosa kutomuomba msamaha before. Ila ndo ishatokea ucumie xna cha msingi usiende kwenye hyo harusi/ndoa. Cha msingi kuwa busy na mambo yako utasahau na kama upo na imani basi piga maombi ya nguvu utapata faraja yako. pole xana ndugu.
 

Du.! hii nafikiri nenda kule kwenye love connect. kweli we ni kichwa, jinsi ulivyotengeneza story na ulivyozunguka , kwani ungesema unatafuta mchumba ingekua kuna tatizo.
 
Ulifanya kosa kutomuomba msamaha before. Ila ndo ishatokea ucumie xna cha msingi usiende kwenye hyo harusi/ndoa. Cha msingi kuwa busy na mambo yako utasahau na kama upo na imani basi piga maombi ya nguvu utapata faraja yako. pole xana ndugu.

Asante ndugu.
 
Pole sana!I know how it feels,
Just learn to let go,Jipende zaidi
 
Grieving stages
1 disbelief
2 Anger
3 bargaining
4 depression
5 acceptance
Depending on your personality and ability to handle difficult situations, you cant skip any stage but ca go through faster...face it feel it accept in your mind you have lost someone you loved...cry...grief eventually you will go through ...some days in the future you will look back n smile...n thats life
 
Yani umsubiri mtu mlieachana kwa zaidi ya mwaka na nusu? Kwamba atarudi tu kwako? Wewe unauzuri gani? Wanawake wengine hakuna?!......Wewe unaumia kwa sababu umri umeenda na wa kukuoa hakuna. Hicho ndo kinakuuma.
 

sex was never a priority?????mnaambiwa the way to a man's heart is through food and sex i.e ujue kupika and u must be a freak in bed...inaonekana hata wakati wa uhusihano hukuwa unamridhisha jamaa sasa ukiongeza hayo na ya kuonwa usiku na mwanaume jamaa akaamua kukutosa.ushauri wangu kwako learn how to please a man and always toa taarifa when the unexpected happens kama vile kuchelewa n.k..ni kitu kidogo but kinajenga uaminifu
 
"Binti amka acha huzunika,
Binti amka acha sikitika,
Binti amka jikaze anza mwendo,
Binti u mrembo na bado wang'ara

"Unasema eti huwezi kuishi bila yeye...
Miaka ilopita hukumjua ni nani yeye...
Mbona uliishi na umekuwa mkubwa sasa...
Iweje akuchezee ili maisha yakuchanganye... wewe"

Rudia chorus

====Lady Jaydee====
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…