Japo sio lazima ila ngoja nikushauri ki utu uzima, kama demu hataki kuwa nawe kimahusiano ya mapenzi, usimlazimishe, tena ni vizuri amekua wazi kwako na anapenda mshirikiane ki elimu, ni jambo jema sana, ili usiumie endelea kumpenda na nakushirikiana naye kwenye masomo, na uwe na faraja moyoni mwako kwa kuwa anakuja kwako kwa ajili ya masomo maana anakuamini.
Huna sababu ya kumchunia na kutomsaidia, sio lazima muwe wapenzi, lakini mwaweza kuwa marafiki wazuri na wenye kufaana baadae hata baada ya kumaliza masomo yenu.
Niliwahi mtaka msichana fulani chuoni lakini yeye hakuwa tayari kuwa nami kimapenzi bali kimasomo, lakini nikuelewa inagawa nilijaribu kumshawishi mara nyingi bila mafanikio sikumchunia wala kumchukia nilimfurahia tu, nikaridhika kuwa naye karibu kimasomo, na baada ya chuo aliolewa na mtu mwingine, na ikapita kipindi kirefu karibu miaka sita, akanitafuta kunipa mchongo wa ajira, tena alinipigania kwa dhati nipate ajira hiyo ili niwe vizuri kimaisha...
Nadhani utajifunza kitu hapo.