Nauli za Mwisho na Mwanzo wa Mwaka

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Hali halisi ya upandishaji nauli za abiria kinyume na bei elekezi ya serikali; vipindi vya mwisho na mwanzo wa mwaka ninachelea kusema isipodhibitiwa inaenda kuzua biashara ya ulanguzi na magendo ambayo haya yataathiri uchumi wa taifa.

Ninachoona kinaenda kutokea mbeleni ni hichi:-

Wanaenda kuzuka watu ambao hawamiliki mabasi lakini wanaenda kununua siti zote za basi kwa bei anayotaka mmiliki alafu analipa ela zote na kumwambia mmiliki kuwa sasa viti ni vyangu mimi ndiyo naviuza (navikatia tiketi) kwa bei yangu ambayo hiyo anaweka kiwango cha juu ya kiwango alichomlipa mmiliki ili yeye mlanguzi apate faida.

Nauli ya mizigo iwe ya dereva na konda lakini kwa bei atayopanga mlanguzi ili asijekwamishiwa abiria.

Konda, tingo, fundi na dereva wanabaki kuwa kwenye utaratibu wa mmiliki siyo mlanguzi huyu.

Service na matengenezo yanaendelea kuwa ya mmiliki kama kawaida.

Sina hakika kama nimebuni mbinu hii ambayo watu wataidaka na kuifanyia kazi.

Tujiandae.
 
Back
Top Bottom