Nauli za Daladala.

Nauli za Daladala.

uporoto01

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2008
Posts
4,698
Reaction score
1,429
Kwa wakazi wa Dar msisahau kuwa nauli za daladala zimepanda kuanzia leo ile safari ya 250/- sasa ni 300/- na safari ndefu zaidi pia zimepanda.
 
bado kidogo leo nimtoe konda jicho!! kumbe nauli zimepandaa!!

Mkwere utatumalizaaa wenzio wakati ww na familia yako mnakula bure, mnatumia usafiri kupitia kodi zetu!! mnaenda loliondo kwa mafuta ya yalionunuliwa kupitia kodi za mlalahoi!!

aaaaaaahhhhhhhh!! Bwana Yesu utarudi lini????????
 
bado kidogo leo nimtoe konda jicho!! kumbe nauli zimepandaa!!

Mkwere utatumalizaaa wenzio wakati ww na familia yako mnakula bure, mnatumia usafiri kupitia kodi zetu!! mnaenda loliondo kwa mafuta ya yalionunuliwa kupitia kodi za mlalahoi!!

aaaaaaahhhhhhhh!! Bwana Yesu utarudi lini????????

susy, unataka umtoe konda jicho gani tena?yeye si sumatra au si aliyeongeza nauli,teh teh teh...hyo ndiyo bongo na watu wake wanaish kwa bongo, fanya mishemishe upate zile pikipiki zilizotoka sauzi ,ooooh!shauri lako,
 
hahahaaaaaaaaaaaaa uwwiiiiiiii mbavu zangu nziriye!!!

sinilisahau kama nauli imepanda best???

ss hizo pikipiki sijui nitazipataje?? hembu nitonye nziriye!!
 
We wa wapi nauli zimepanda kote.inavyoonekana sio mtumiaji san wa hiv vyombo vya moto.
 
hata hivyo nauli ya 300 kutoka ubungo mpaka posta ni kiasi kidogo umbali wa km zaidi ya 15, wakati kigali kuingia city umbali chini ya km 15 nauli yake kwa pesa yetu inafika TSH1000. Halafu hivi hujui kama mafuta yamepanda bei? unajua pipa la mfuta limetoka dola 90 mpaka 120 unategemea nini?
Watanzania tuache kumlaumu mkuu wa nchi, kuna watu wanahusika na isue za mfumuko wa bei. yaani Raisi ndio atupangie bei ya bidhaa.Hivi unajua kuna BOT. Tujiulize huyo Prof.ndulu anafanya kazi gani ama kutengeneza noti. hayo ndio majukumu yake kuzuia mfumuko wa bei. la sivyo tuandamane ili ndulu ajiuzulu kwa sababu ameshinwa kutekeleza majukumu yake.
Halafu watanzania wanalia na mfumuko wa bei ya vyakula wakati kulima hamtaki, nani awalimie nyie mle. kila mtu anataka kuishi dar wakati huku kwetu kilosa moro mabonde yanalalia mapori hakuna watu wa kulima. hapa kjjn kwetu zinalimwa ekari 200 tu kati ya 500 za umwagiliaji.
 
yani nipo ndani ya dala dala konda anatangaza nauli mia tatu naingia jf nimehakiki kweli jambo ukilikosa jf ujue alijatokea mana hapa mpaka tetesi zinapatikana ila mkwere utokwepa lawama we ndio mkulu wa nchi
 
Na bado maisha yatazidi kuwa magumu, hii itatufanya watanzani tuamke na tufanye vitu kwa umakini sana....pole kwa walalahoi wenzangu..mmmhhhhhuuu? Maisha bora kwa kila mtanzania!
 
dah.sasa kwa yule anayependa toka mapipa hadi mwembechai je?naye alipe mia300?its nt fair..hii ki2 nimekutana nayo leo,mimi ckulipa mia300.nilikuwa naelekea posta.nililipa 250 ila i had utata na konda.
 
wewe fire posta.sh 300?dah tunapoelekea ni pabaya..life becomes more hard n pesa ye2 inashuka thamani 2.
 
hata hivyo ukilinganisha nauli zetu na miji kama nairobi nauli bado iko chini sana,,,, na zingeweza kuwa chini zaidi ya hapo kama serikali ingekuwa inatoa vipaumbele kwa sekta zingine ambazo zingeweza kuingiza mapato na si kila bajeti ni kuongeza kodi kwenye mafuta..
 
dah! Tanzania kaz ipo na tabu 2pu yan kilaki2 yan cjui 2nakwenda wap
 
Tunapoyaona hayo, binafsi naona tusilaumu kupita kiasi, ila tufikirie zaidi, tufanye kazi kwa bidii zaidi, tuzalishe zaidi ili tupate zaidi.

Lawama sio nzuri sana, hata Mungu hapendi kulaumu laumu kila kitu. Hebu tufikirie na kutenda zaidi ya kulaumu laumu!!!
 
Mtu anakaa bunju anafanya kazi mbagala itakuaje?
Bunju mpaka mwenge tsh 500
mwenge mbagala3 tsh 500
total tsh 1000
hivyo kwenda na kurudi ( 1000 x 2) = 2,000
nauli kwa mwezi ( 2000 x 30 ) = 60,000

huyu mtu analipwa kima cha chini tsh 80,000

baki kwa ajili ya familia ( tsh 80,000 - tsh 60,000 ) = 20,000!

askari mshahara tsh 160,000 kwa mwezi
toa nauli ( tsh 160,000 - tsh 60,000) = tsh 100,000

nb; kweli rushwa itaisha!
 
Inabidi kutafuta baiskeli au kutembea kwa miguu tu ndugu zangu!
 
Mtu anakaa bunju anafanya kazi mbagala itakuaje?
Bunju mpaka mwenge tsh 500
mwenge mbagala3 tsh 500
total tsh 1000
hivyo kwenda na kurudi ( 1000 x 2) = 2,000
nauli kwa mwezi ( 2000 x 30 ) = 60,000

huyu mtu analipwa kima cha chini tsh 80,000

baki kwa ajili ya familia ( tsh 80,000 - tsh 60,000 ) = 20,000!

askari mshahara tsh 160,000 kwa mwezi
toa nauli ( tsh 160,000 - tsh 60,000) = tsh 100,000

nb; kweli rushwa itaisha!
Angalizo: Askari wanapokuwa katika sare zao hawalipi nauli, hupanda dala dala bure.
 
Back
Top Bottom