Nauchukia zaidi ufisadi kuliko ninavyoichukia CCM

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,223
Katika Tanzania nauogopa na kuuchukia sana ufisadi kuliko ninavyoichukia CCM na Serikali yake. Na kiukweli kabisa chuki yangu kwa CCM ilikuja baada ya kugundua kwamba chama hicho kimeugeuza ufisadi kama ndiyo mfumo wake rasmi wa kuendesha mambo. Lakini ukweli wa mambo unaoonyesha kwa kukaa kwake muda mrefu kwenye madaraka, CCM imeambukiza ufisadi kwa watz wengi sana.

Niliwahi kumsaidia mama mmoja kuhudhuria semina pale Giraffe Hotel. Alipotoka kwenye semina na laki tano zake za posho (Per diem) aling'ang'aniza anipe "asante" hata baada ya kumwambia kwamba kuhudhuria kwake kwenye semina ile kulitokana na yeye kuwa na sifa za kuhudhuria semina na wala si upendeleo kutoka kwangu. Niliikataa asante yake!!

Huo ni mfano mmoja tu wa hali halisi kwenye jamii yetu. Tuna watu wangapi tunaowajua wanatumia vyeti vya kughushi kupata ajira, tumetoa taarifa polisi? Ndugu zetu ambao ni Traffic Police na wanamiliki mali tofauti na mishahara yao tumewahi kuwakemea? Ni wangapi kati yetu tunafanya biashara au kupangisha nyumba bila ya kulipa kodi, huo nao siyo ufisadi?

Kwenye NGOs tunazofanyia kazi tumeghushi risiti ngapi na ni fedha kiasi gani tulizokwapua na kwenda kujengea nyumba au kununulia magari badala kufanya kazi zilizokusudiwa. Ufisadi kama huu ni lazima ufanywe na Lowassa ndiyo tuupige kelele?

Ili kuirekebisha nchi yetu ni lazima tuupige vita ufisadi hata bila ya kujali kama umo CCM, CUF, CHADEMA, msikitini ,kanisani, kwa jirani au ndani ya nyumba zetu. Kwa maana kuna watu humu jamvini wanataka tuamini ufisadi ni matendo mabaya ya wanasiasa peke yao ila matendo hayo hayo yakifanywa na watu wa kawaida tunatafuta sababu za kuyatetea na kuyahalalisha maovu hayo. Ufisadi ni ufisadi tuu hata kama unatendwa na baba yako mzazi au mkweo.

Ufisadi Tanzania umo madarasani, umejaa kwenye mabweni, umejikita kwenye mithani, umeota mzizi kwenye matokeo, haushikiki kwenye usaili, umetamalaki kwenye ajira, upo kwenye mishahara, ndiyo alama ya mafanikio,na ni chanzo cha mbwembwe kwenye maisha yetu ya kila siku mtaani. Kwa hakika UFISADI ndiyo NGUZO ya MAISHA ya kila SIKU kwa WATANZANIA wengi.

Wewe ukifumba macho haimaanishi wenzio wote nao pia hawaoni.
 

MwanaCBE

JF-Expert Member
Sep 23, 2009
1,773
800
Sijakuelewa mwandishi. Unamaanisha kuna tofauti kati ya CCM na UFISADI?? Naomba unieleweshe tafadhali, mi huwa sioni tofauti hapo.
 

kiloni

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
575
75
Katika Tanzania nauogopa na kuuchukia sana ufisadi kuliko ninavyoichukia CCM na Serikali yake. Na kiukweli kabisa chuki yangu kwa CCM ilikuja baada ya kugundua kwamba chama hicho kimeugeuza ufisadi kama ndiyo mfumo wake rasmi wa kuendesha mambo. Lakini ukweli wa mambo unaoonyesha kwa kukaa kwake muda mrefu kwenye madaraka, CCM imeambukiza ufisadi kwa watz wengi sana.

Niliwahi kumsaidia mama mmoja kuhudhuria semina pale Giraffe Hotel. Alipotoka kwenye semina na laki tano zake za posho (Per diem) aling'ang'aniza anipe "asante" hata baada ya kumwambia kwamba kuhudhuria kwake kwenye semina ile kulitokana na yeye kuwa na sifa za kuhudhuria semina na wala si upendeleo kutoka kwangu. Niliikataa asante yake!! Huu ni mfano mmoja tu wa hali halisi kwenye jamii yetu. Tuna watu wangapi tunaowajua wanatumia vyeti vya kughushi kupata ajira, tumetoa taarifa polisi?

Ndugu zetu ambao ni Traffic Police na wanamiliki mali tofauti na mishahara yao tumewahi kuwakemea? Ni wangapi kati yetu tunafanya biashara au kupangisha nyumba bila ya kulipa kodi, huu nao siyo ufisadi? Kwenye NGOs tunazofanyia kazi tumeghushi risiti ngapi na ni fedha kiasi gani tulizokwapua na kwenda kujengea nyumba au kununulia magari badala kufanya kazi zilizokusudiwa. Ufisadi kama huu ni lazima ufanywe na Lowassa ndiyo tupige kelele?Ili kuirekebisha nchi yetu ni lazima tuupige vita ufisadi hata bila ya kujali kama umo CCM, CUF, CHADEMA, msikitini ,kanisani, kwa jirani au ndani ya nyumba zetu. Kwa maana kuna watu humu jamvini wanataka tuamini ufisadi ni matendo mabaya ya wanasiasa peke yao ila matendo hayo hayo yakifanywa na watu wa kawaida tunatafuta sababu za kuyatetea na kuyahalalisha maovu hayo.

Ufisadi ni ufisadi tuu hata kama unatendwa na baba yako mzazi au mkweo. Ufisadi Tanzania umo madarasani, umejaa kwenye mabweni, umejikita kwenye mithani, umeota mzizi kwenye matokeo, haushikiki kwenye usaili, umetamalaki kwenye ajira, upo kwenye mishahara, ndiyo alama ya mafanikio,na ni chanzo cha mbwembwe kwenye maisha yetu ya kila siku mtaani. Kwa hakika UFISADI ndiyo NGUZO ya MAISHA ya kila SIKU kwa WATANZANIA wengi. Wewe ukifumba macho haimaanishi wenzio wote nao pia hawaoni.
Nimekuelewa na kwa kifupi unamaanisha ufisadi ni taasisi.
Tunataka kuingoa hiyo taasisi tuanzie wapi?
Ni nani mwenye uwezo wa kuvunja taasisi yoyote TZ?
Ninakubali kuwa ni issue ya mindset je tuanzie wapi?
Tunataka tupigane na mizizi ya kutaasisisha ufisadi tufanye nini?
tuepuke hoja nyepesi tujadili kwa mapana hapa. Tatizo la kimfumo linahitaji utatuzi wa kimfumo vile vile!
 

Mwita25

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
3,836
1,164
Kwahiyo unataka kumaanisha kuwa tunaweza kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi hata kama bado CCM ipo madarakani? Nadhani ni uchambuzi mzuri sana ambao umewahi kuingia JF. Ni kweli kabisa kwasababu watu wengi wamekuwa wakiitupia lawama CCM na kuilaumu kuwa ni chanzo cha ufisadi bila hata kuchunguza kuwa ufisadi ulianzia wapi. Sasa utafumbua macho baadhi ya wapinzani wa JK.
 

kiroba

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
324
114
Hapa mkuu umenena. Wajua wengi sana wameshindwa kujua hiki chama tawala kilivyoanzisha kampeni ya kufukuzana kwenye chama ikiwa na kauli mbiu ya kujivua gamba. Hapa kwa uelewa wangu walikuwa hawana shida sana na ufisadi bali ni watu wanaotajwa kuwa ni mafisadi.

Ukiangalia unagundua vita hii ni kata ya mtu na mtu au kikundi fulani baina ya mtu mmoja au kikundi cha watu. Hapa my comrade NAPE aliingia kichwa kichwa hakujua maana halisi ya wimbo huo wa kujivua gamba. Ni kweli ufisadi ni tatizo kubwa sana kwa maendeleo ya taifa letu lenye rasilimali lukuki.

Mwenyewe binafsi nachukia sana ufisadi kuliko kuchukia chama. Ninasema chama kwa kuwa kila chama kina mabaya yake japokuwa vinatofautiana kwa hayo mabaya.

Ushauri kwa comrade NAPE MNAUYE, achana na hao viongozi wa CCM kwa sasa kwani wao hawana nia thabiti ya kupinga ufisadi bali wana vita wanayoijua wao lakini wewe wanakutumia kama chambo na hata watakapokuwa wamemalizana basi wewe tena utakuwa huna maana tena.
 

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,869
9,820
Ufisadi ni Ufisadi tu!! Ufisadi unaanzia kwenye kwa wahudumu wa ofisi hadi viongozi serikalini. Tofauti ni access tu kwamba mhudumu wa chai ana access na majani ya chai na sukari; anafanya ufisadi wa kuiba sukari na majani ya chai. Mtu kama huyo angekuwa na access ya mamilioni naye angefanya ufisadi tu wa kiasi kikubwa. Tusiangalie ufisadi kwa tarakimu tu tuangalie ufisadi kwa asilimia. Lowasa ni fisadi sawa; na mhudumu wa chai naye ni fisadi vilevile na anayeuza magari chakavu ni fisadi pia. SUALA LA UFISADI NI MTAMBUKA
 

Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
931
Yap umenena,
Ufisadi uko pia chadema

Ufisadi wa kutoa viti maalum vya ubunge kwa ndugu au jamaa wa nasaba za viongozi wakuu na hata kanda

ufisadi upo pia katika kupokonya ndoa za watu hali kuna wanawake kibao mitaani

Uadilifu utasimamiwa na mtu moja moja wala si chama wala taasisi
 

MwanaCBE

JF-Expert Member
Sep 23, 2009
1,773
800
Ufisadi ni Ufisadi tu!! Ufisadi unaanzia kwenye kwa wahudumu wa ofisi hadi viongozi serikalini. Tofauti ni access tu kwamba mhudumu wa chai ana access na majani ya chai na sukari; anafanya ufisadi wa kuiba sukari na majani ya chai. SUALA LA UFISADI NI MTAMBUKA
UNAMAANISHA UFISADI NI WIZI?? Kweli tunatofautiana..!!
 

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,223
Nimekuelewa na kwa kifupi unamaanisha ufisadi ni taasisi.
Tunataka kuingoa hiyo taasisi tuanzie wapi?
Ni nani mwenye uwezo wa kuvunja taasisi yoyote TZ?
Ninakubali kuwa ni issue ya mindset je tuanzie wapi?
Tunataka tupigane na mizizi ya kutaasisisha ufisadi tufanye nini?
tuepuke hoja nyepesi tujadili kwa mapana hapa. Tatizo la kimfumo linahitaji utatuzi wa kimfumo vile vile!

Tuanzie kwenye familia ambayo ndiyo taasisi inayounda taasisi nyingine zote.

Hivi umewahi kujiuliza kwamba kanuni ya baba kula mapaja na sehemu nyingine nzuri nzuri kuku anapochinjwa na kuwaachia watoto vipapatio na shingo ni Ufisadi? Impact ya tukio hili mtoto akiwa mkubwa unalijua? Mtoto huyu akikua ni lazima aamini kwamba wakubwa (viongozi) wana haki ya kula vizuri hata kama wadogo wanaambulia "vipapatio"

Kwa maoni yangu tuanze kusafisha ufisadi kwenye familia zetu kwanza.
 

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,223
Sijakuelewa mwandishi. Unamaanisha kuna tofauti kati ya CCM na UFISADI?? Naomba unieleweshe tafadhali, mi huwa sioni tofauti hapo.

CCM ni taasisi na ufisadi ni tabia,lakini kwa bahati mbaya sana tabia ya ufisadi imekuwa ndiyo nguzo ya kupata madaraka ndani ya CCM. CCM siyo kila mwanachama wa CCM ni CCM, CCM ni Kamati Kuu ya CCM. Kama ndani ya Kamati Kuu asilimia kubwa ya wajumbe wa kamati hiyo wana tabia ya Ufisadi basi ni lazima tuseme CCM ni mafisadi.

Kuna wanachama wa CCM ambao ni walokole kabisa lakini wao si "CCM" kwani hawana madaraka ya kuamua jambo ndani ya CCM. Kwa hiyo ikifika mahali hawa wana CCM Decent wakifanya mapinduzi na kuchukua madaraka CCM itakuwa si ya mafisadi tena. Lakini kwa hali ya mambo ndani ya CCM haielekei hawa wana CCM decent wataweza kuimiliki CCM bila ya CCM kuondolewa madarakani.

Ufisadi ndani ya CCM ni kama kitendawili cha glasi na maji nusu au maji nusu na glasi. Kwa sasa Ufisadi ni CCM na CCM ni ufisadi
 

Laface77

JF-Expert Member
Jul 9, 2008
2,117
2,845
Kwahiyo unataka kumaanisha kuwa tunaweza kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi hata kama bado CCM ipo madarakani? Nadhani ni uchambuzi mzuri sana ambao umewahi kuingia JF. Ni kweli kabisa kwasababu watu wengi wamekuwa wakiitupia lawama CCM na kuilaumu kuwa ni chanzo cha ufisadi bila hata kuchunguza kuwa ufisadi ulianzia wapi. Sasa utafumbua macho baadhi ya wapinzani wa JK.
Mwita25, Ufisadi na CCM ni maneno mawili tofauti lakini yenye maana moja!Tukitaka kuondoa ufisadi Tanzania lazima CCM izikwe. Ufisadi na CCM=Synonyms.
 

Laface77

JF-Expert Member
Jul 9, 2008
2,117
2,845
Kwahiyo unataka kumaanisha kuwa tunaweza kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi hata kama bado CCM ipo madarakani? Nadhani ni uchambuzi mzuri sana ambao umewahi kuingia JF. Ni kweli kabisa kwasababu watu wengi wamekuwa wakiitupia lawama CCM na kuilaumu kuwa ni chanzo cha ufisadi bila hata kuchunguza kuwa ufisadi ulianzia wapi. Sasa utafumbua macho baadhi ya wapinzani wa JK.
Mwita25, Ufisadi na CCM ni maneno mawili tofauti lakini yenye maana moja (Synonyms)!Tukitaka kuondoa ufisadi Tanzania lazima CCM izikwe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

3 Reactions
Reply
Top Bottom