Mimi nishaitupa line yangu ya Airtel wiki mbili zilizopita,sababu kila nikijaribu kujiunga Airtel tosha inaniambia huduma hii haipatikani kwa sasa jaribu tena baadae,kupiga simu Huduma kwa Wateja wakanijibu kuwa kuna baadhi ya line zina tatizo hili,nikasema ngoja nisubiri labda tatizo litaisha,kaa mwezi mzima hakuna mabadiliko. Kilichonifanya niitupe line ni pale unapoweka salio,mfano buku,ukipiga simu Airtel to Airtel dk mbili haziishi hela imeisha na ukilogwa ulaze salio kwenye simu umeliwa.
Nilichogundua ni kuwa zile line zote zilizoanza kutumia huduma hii ya Tosha katika hatua za mwanzo kabisa ndizo hizo zilizofungiwa,sasa sielewi hawa watu wana maana gani kutoa promotion biased namna hii.