Bando ya voda ilivyobadilishwa haimjali mteja na sijui kama huyo jamaa aliyetoa wazo hili ameliweka kiushindani au anataka kufanya nn.Nilikua naona kwamba haya makampuni ya simu yalikua yanarahisisha mawasiliano ila kwa upande mwingine naona lengo kubwa ni kutengeneza faida na hapa ndio naona Serikali kupitia Kale kajamaa TCRA wanatakiwa waseme kitu
wadau mnaonaje?
Wakuu mwenzenu tangu voda itibue hiyo cheka bombastic Yao nakuweka wizi wao hadi Leo sijanunua vocha ya voda, niko zangu airtel yatoaha vifurushi vya wiki vunanipa dakika za kutosha tu kupiga mitandao yoote, akizingua huyu nahamia kwa mwingine as simple as that
Mie najiandaa kuhama Tigo. Usipojiunga na zile bando zao, ukaacha pesa yako ina-hang; inakua halali yao. Hutajua imekwisha vipi. Tatizo niliwaamini kupitiliza, ina all official contacts. Mitandao hii imeharibika sana nowdays; labda Airtel; so far wananpa nafuu ya maisha na 'hakatwi mtu hapa'. Siku hizi hawafanyi mawasiliano; wanatutumia kufanya biashara zao za bahati nasibu, ring tones n.k.
Hawa voda huu ni wizi wa mchana kweupe.narudia tigo yangu.nimegundua niliingia chaka kumbe.wamefanya kimya kimya mno inabidi niwashawishi washikaji wangu tusepe
Mimi nineshaitupilia mbali line ya voda na kampun kwa ujumla hawamjali mteja kwangu ni kero sana wanataka kuchuma na sio kutusaidia hawana maana tena mpaka watakapojirekebisha viwango vya mitandao vipo juu sana gharama wewe unangoja nn kuhama?
Kwa mtazamo wangu huu wizi unachangiwa na tcra ambao wana thamana ya kusimamia makampuni ya mawasiliano hapa Tz kwa mwezi wa Aprili 2013 walipitisha kiwango cha kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mtandao mwingine kuwa tsh 35/dakika na tunachokiona sasa hivi ni ngonjera ya kujirusha ,kabaang na babalao .Tcra tunaomba majibu kwa hili.
Pumbafu kabisa voda, nimewapigia customer care nikawatukana mbaya, wamelewa umaarufu sasa inakula kwao, eti wanaweka voda kwenda voda masekunde kibao alafu voda mitandao mingine sec 45, inalazimisha tuwapigie watu wa voda tu, pumbafu, sasa tunangoa vi voda vyao.:frusty: