Natumaini SIFA HIZI NDIZO wanazo VIONGOZI WETU akianzia Rais

LGMJAMII

Member
Nov 5, 2010
44
0
Ni kweli kuna kiongozi yeyote mwenye sifa kama hizi?

1. Ana hofu ya MUNGU
2. Anaweka maslahi ya umma mbele kuliko yake ya binafsi au ya chama chake.
3. Mtetezi wa haki za wanyonge.
4. Hatoi wala kupokea rushwa.
5. Mkweli na muwazi
6. Mwaminifu.
7. Anafanya maamuzi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo.
8. Anazingatia matumizi sahihi ya taarifa.
9. Yuko tayari kukoselewa.
10. Mwajibikaji
 

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,170
1,500
Ni kweli kuna kiongozi yeyote mwenye sifa kama hizi?

1. Ana hofu ya MUNGU
2. Anaweka maslahi ya umma mbele kuliko yake ya binafsi au ya chama chake.
3. Mtetezi wa haki za wanyonge.
4. Hatoi wala kupokea rushwa.
5. Mkweli na muwazi
6. Mwaminifu.
7. Anafanya maamuzi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo.
8. Anazingatia matumizi sahihi ya taarifa.
9. Yuko tayari kukoselewa.
10. Mwajibikaji

Mkuu kwenye hizi sifa ulizozitaja unaweza usimpate hata mmoja ambaye yuko madarakani, kwa mfumo uliopo ukiwa na sifa hizi unaenguliwa kugombea nafasi ya udiwani, ubunge na hata urais
 

kiloni

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
575
0
Mkuu Kinyume chake ndiyo sifa za viongozi wetu ukianzia na JK.
1. Hakuna hofu ya Mungu- Hofu na imani kuu vipo kwa jamaa wa mlingotini nk
2. Maslahi ya uma nyuma ya maslahi binafsi, familia, vimada na marafiki. Mfano kuliko JK amtupe Lowasa au Rostam gerezania afadhali nchi yote ifilisike na wafe wote.
3. Wanyonge watanyongwa tu. Wakipiga kelele wataitwa WADINI, WAHUNI, WAKOROFI, WAHAINI. kuna vilaza wanyonge wenzetu wanaamini hivi hasa UDINI siku hizi
4. Ulaji wa Rushwa ni imani ya viongozi.
5. Uwongo mpya, ahadi mpya za uwongo, hasa kila baada ya kuchakachua matokeo ya uchaguzi mkuu.
6. Uwe mwanaminifu kwa mafisadi wenzio na usifichue sera ya UFISADI kwa wanyonge.
7. Maamuzi ni lazima yatokane na Matakwa ya Mkuu wa Mafisadi.
8. Taarifa za kusifia Mafisadi na maamuzi ya kifisadi zidumishwe
9. Kukosoana ni UHAINI na UDINI
10. Awe anawajibika kwa mafisadi waliomweka madarakani bila kujali vyeo vyao.
 

Questt

JF-Expert Member
Oct 8, 2009
3,010
1,195
HAKUNA Hata mmoja.....Si TZ tu Dunia nzima.....................
 

andrewk

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
3,102
1,500
HAKUNA Hata mmoja.....Si TZ tu Dunia nzima.....................

jamani kati ya watanzania million 40 wapo, tatizo tunadhani watapatikana CCM, haiwezekani! 1993 mwalimu Nyerere alisema CCM ni kama dodoki ukiliweka mwenye maji litabena na uchafu, kwa miaka 40 sasam limebeba uchafu mwingi mpaka halisafishiki tena. Chama ni matendo wala sio sera,..nchi makini zina written interest za nchi ambazo wote wanatakiwa kuzitimiza wawapo madarakani, angalia katiba ya yetu ya 1997 tunadhani ni bora! kesho unauliza nani anaturoka kwa kukosa maendeleo? Kikwete alisimania uandda wa foreign policy ya Tanzania miaka ya 1990, kwenye hotuba yake bungeni anazungumzia kuendele kupata misaanda toka nje!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom