Natonesha vidonda.... **** ya kale yananuka!

Kwanza - Kidonda kikipona huwa kovu ambalo haliumi hata likipakwa pilipili. Lakini kidonda sugu huendelea kuuma kila kikitoneshwa hadi hapo dawa itakapopatikana. Leo nimekusudia kutonesha vidonda, mchangiji endelea kutonesha vidonda zaidi.

Pili - wahenga walisema mavi ya kale hayanuki. Nadhani walimaanisha yale ya vichakani na si haya tunayoyashusha kwenye vyoo vya kizungu wakati hakuna maji ya kuyasukuma.

Tatu - watanzania tunakosa mfumo wa kufuatilia nyeti za kale na haraka huwa na tabia ya kushabikia mambo mapya. (Kuna waziri mmoja marekani ya obama, alijiuzulu hata kabla ya kuapa kwa kosa la kukwepa kodi ya vijisenti zaidi ya miaka 10 nyuma; nakapenda haka kautaratibu)

  • mavi ya kale = Dr. Hussein Mwinyi na kidonda cha Gongo la Mboto
  • mavi ya kale = Andrew Chenge na kidonda ni rada
  • mavi ya kale = Zombe na vidonda mnavijua
  • mavi ya kale = Karamagi, Lowassa, Rostam na vidonda ndugu richmond, dowans, na kidonda kipya
  • mavi ya kale = Mgodi wa North Mara na vidonda ni vifo kutokana na maji ya sumu
  • mavi ya kale = JK na kidonda ni IPTL

Dege la waarabu kupark KIA na kupakia twigabila bugudha, mavi kabisa, usalama wa taifa mavi kunuka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom