Natoa ushauri wa bure kwa CHADEMA ili ki-survive hadi 2025

KooZito

JF-Expert Member
Dec 14, 2020
396
1,377
Hatuwezi tukabishana hadi kuku warudi bandani kwamba Chadema bado ni chama Kikuu Cha Upinzani Tanzania hata kama hakina kinara wa upinzani. Hata hivyo lazima Chadema kitafakari kwa kina na mapana kitawezaje kuishi kama chama kuelekea 2025?

Mambo kadhaa yanapaswa yafuatwe kama bado Mbowe anataka abaki sokoni. Otherwise, huu unaweza kuwa tamati ya Chadema na kuinuka kwa ACT-Wazalendo katika kuendeleza utaratibu wa "rise and fall" ya vyama vya Upinzani.

(1). Chadema iseti ajenda mahsusi wanayohubiri asubuhi, mchana, jioni na usiku. Iwe ndio wimbo wao kama ilivyo "Hapa Kazi Tu" ya watani zao.

Napendekeza kwao ajenda hiyo iwe ni Katiba Mpya ya Warioba pamoja na Tume Huru ya Uchaguzi.

(2). Wabunge wao Bungeni wakiongozwa na Halima Mdee wasipokonywe uanachama na hivyo wasiondolewe Bungeni. Pamoja na uchache wao Bungeni lakini wawe na ajenda. Hata kama wangekuwa wawili tu. Bunge ni jukwaa zuri sana la "kuamsha dude". Waliamshe dude kwelikweli. Hata kama watafukuzwa Bungeni mara mia moja lakini waoneshe kuwa wanayo ajenda.

Wanapoliamsha Bungeni, huku nje Mbowe na Lissu nao wanaliamsha. Hivyo kelele za Katiba Mpya na Tume Huru zitasambaa na kufika masafa marefu. Hata mwenye pamba sikioni atazibuka.

(3). Wabunge 19 wajenge hoja Bungeni ya kutaka Tume ya Kibunge iundwe kuchunguza ni nini hasa kilitokea Uchaguzi wa 2020? Hili suala la "tumeibiwa kura" isiachwe ipite hivi hivi. Uchunguzi ufanyike kwa maslahi mapana ya nchi. Chadema iachane na maauala ya pesa sijui mishahara ya Wabunge kama Lissu anavyofikiria. Hayo ni Mambo madogo sana kwa wanasiasa wenye visheni kali.

(4). Kwa mambo ambayo ni kwa maslahi ya nchi, Chadema imuunge mkono Rais Magufuli kuyatekeleza maana nchi ni yetu sote. Tusipinge kila kitu.

Nawasilisha.
 
Cdm haina wabunge ndani ya bunge hili. Katiba mpya inaweza kudaiwa sio lazima iwe ndani ya hilo bunge kibogoyo. Ongea na wabunge wa ACT wadai hiyo katiba mpya huko bungeni maana kwa mujibu wa maelezo yako, wao ndio watapanda kwenye hiyo principle ya rise and fall ya vyama vya upinzani.

Unataka Magufuli aungwe mkono na cdm, yeye Magufuli amewahi kuunga mkono ajenda gani ya cdm ili tujue na yeye hapingi kila kitu?
 
Unataka Chadema ichukue huu ushauri wako unaotetea "wabunge" 19 kwenda bungeni bila kufuata taratibu?

Watu waliojiamulia kwa mapenzi yao kujipeleka bungeni simply because Chadema ilikuwa na nafasi 19 za wabunge wa viti maalum bila kufuata makubaliano waliyokubaliana kwenye KK ya chama chao, hicho kwangu ni kikundi cha wahuni tu.
 
CCM yenyewe inajua imechokwa na wananchi, ndo maana wakiambiwa Mambo ya katiba mpya au utawala wa kisheria, Tume huru ya uchaguzi hawawezi kutoa majibu yanayoeleweka
 
Wamekusikia akija mwenye visheni yake kutoka Dubai watamueleza wale ambao hawamuogopi japo nasikia wengi wao wanamuogopa hawawezi kumwambia chochote kinachohusu ukweli wa chama chao.
 
Back
Top Bottom