NATO wakataa ombi la Ukraine

NATO wakataa ombi la Ukraine

Raisi wa ukraine tunasema alidanganywa lakini kiuhalisia alishindwa kung'amua kelele za USA na hii ni kutokana na kuwa mgeni wa siasa za nchi za magharibi akajikuta ameingia na miguu miwili. hii vita hakuna wa kumsaidia kijeshi atafute tu namna yoyote ya kuzungumza moja kwa moja na putin au otherwise anyooshe mikono juu kusurrender

Sent using Jamii Forums mobile app
Si unaona alivyofura na kuwakashifu NATO kwa kukataa kulinda anga lake.
Ni tabia ya 'vijana wadogo' kuanzisha pambano huku wakitegemea nguvu toka kwa kaka zao.
 
Ukraine asingeingia vitani Kama angejua atakuwa peke yake Urusi nguvu yake ya kijeshi Ni kubwa Sana labda alihaidiwa atapata msaada na sivinginevyo.
Waliowashauri wamewaharibia sana. Kwa miaka minane tokea 2014 Ukraine wamekataa kutekeleza mkataba wa amani ulisimamiwa na umoja wa mataifa na kutiwa saini huko Minsk Belarus. Wangetekeleza yale makubaliano hii vita isingekuwepo kabisa badala yake wakajaa kiburi cha NATO. pamoja na kwamba wanapenyezewa silaha kwa sasa lakini watapoteza zaidi majimbo na uharibifu mkubwa zaidi kuliko wangekubali mkataba wa minsk
 
Chief, mambo ya udukuaji hayaangalii nchi mzee.. ni uwezo na capacity tu.. kuna machalii tu toka taiwan huko wanadukua hawafai, je Taiwani ni taifa la maana sana duniani?
Ndio wakubali wamezidiwa uwezo na Dunia ya sasa information is everything.
Siku moja Putin aliwahi kusema anaijua mipango ya US na NATO kwa zaidi ya miaka 15 ijayo, na akaeleza moja ya mipango yao kuibomoa Russia. Aliyasema hayo kipindi cha mgogolo wa Edo Snowden 2012.
 
NATO wamekataa ombi la Ukraine la kuziomba nchi za NATO kuweka "the no fly zone" nchini Ukraine.

No fly zone ikimaanisha mpango wa kujilinda katika upande wa anga huku ikimaanisha Kama Ukraine wangekubaliwa ndege za Urusi zingeshambuliwa pale tu zinapoingia katika anga la UKRAINE.

Jambo ambalo halijaungwa mkono na NATO huku wakiweka wazi Kama wakifanya hivyo watakuwa wameruhusu vita ya Nuclear rasmi jambo ambalo siyo mpango wao.

Mwaka 2001 US na washirika wake waliweka no fly zone kule Iraq, 1992 Bosnia na 2011 Libya.

Je Raisi wa Ukraine Mr Zelensky alidanganywa kwa kuhakikishiwa msaada na NATO?? Au alijihakikishia mwenyewe.
Tuendelee kuwa watazamaji.
Na leo pande zote mbili zimekubaliana kusimamisha vita kwa muda kuruhusu watu wanaotaka kuondoka hapo UKRAINE,unadhani watu wakiondoka hapo Russia hatakuwa na huruma na mtu. Acha wachezee kichapo
 
NATO wanataka vipigo vya chini chini...

Za juu juu wanajua shughuli yake pevu...
 
Mchawi vita hii ni huyu commedian Rais wa Ukraine mwenyewe.
Alijua atapata support ya EU, US au NATO.

Sidhani kama alikuwa wise enough...kupima mambo kisiasa, Hasa ktk nafasi ya president.

Ni nafasi ya kufujinza kuwaingiza watu kimhemuko ktk majukumu serious.....kisa tu ni mtu maarufu ( msanii).
 
Na leo pande zote mbili zimekubaliana kusimamisha vita kwa muda kuruhusu watu wanaotaka kuondoka hapo UKRAINE,unadhani watu wakiondoka hapo Russia hatakuwa na huruma na mtu. Acha wachezee kichapo
Wameshaanza kui violate mkuu
 
Back
Top Bottom