Andrew Nyerere
JF-Expert Member
- Nov 10, 2008
- 3,007
- 2,469
..nimepitia JKT na sikuona faida yake.
..ilikuwa ni sawa na mwaka mzima wa kukaa kijiweni tu.
..binafsi ningependekeza iwe ni suala la HIARI ya mhusika kujiunga na JKT.
..anayeona atafadika ajiunge na JKT, asiyefahamu manufaa yake aachwe aendelee na maisha yake.
Wananchi, National Service hatukuanzisha sisi. Mataifa mengi duniani yana National Service. Taifa linawaambia vijana wake; tunataka vijana mlitumikie Taifa lenu. Taifa linadai utumishi toka kwa vijana. Linadai huduma kwa vijana. Na vijana wanaitika wito huo kwenda kulihudumia Taifa kwa kazi yo yote ambayo Taifa linahitaji ifanywe. Kwa desturi National Service au huduma wanayoitiwa vijana hawa wa mataifa haya mengine duniani, ni huduma ya kivita. Wanaitwa vijana wafundishwe kazi ya kivita. Ikiwa kesho na kesho kutwa hapana budi, basi waende wakapigane . Hiyo ndiyo National Service ya kawaida kwa mataifa mengine duniani Na sisi, wananchi, tumeanzisha National Service hapa. Tofauti ya kweli baina ya National Service yetu na zingine ni nini. Kwanza, ya kwetu si ya kivita; ni ya UJENZI. tumewaita vijana waingie katika National Service, na kazi tutakayowapa ni ya UJENZI KATIKA NCHI.
Watanzania wenzangu.
... wale wa kutoka Sokoine University of Kilimo watakwenda mashambani etc. kwa wanafunzi wanaweza kwa kweli kuunganisha mara tu wakimaliza shule na wale wengine ambao wako makazini ndio watakalazimia kupewa muda ndani ya miaka mitatu. kukamilisha hii requirement (a bill may be passed through national assembly)
Mtanzania huyu atatakiwa kwa wakati atakao taka yeye ndani ya hiyo miaka mitatu atoe huduma hiyo na akishamaliza atapatiwa cheti cha kitaifa.
Pendekezo hili litatatua kwa kiasi kikubwa sana uhaba wa walimu, madaktari etc. Na pia kurudisha uzalendo uliopotea etc.
Endeeleni kujadili...
Hivi kuna tofauti gani kwa wale walioenda JKT na ambao hawakwenda? JKT was a waste of time kwa vijana wengi na ni chombo cha propaganda tuu za CCM na serikali yake kuharibu watu akili na sera zao za ujamaa uchwara,ndio maana mpaka leo nchi imejaa mafisadi na wababaishaji.
Kasheshe,
..Ghana wao wanachukua vijana waliomaliza vyuo vikuu na kuwapa kazi ktk maidara ya serikali kwa kipindi cha mwaka mmoja. vijana hao huwa wanalipwa allowance ndogo na siyo mishahara.
..JKT hii ya miaka nenda rudi ibakie kuwa "chekeche" la vijana wanaotaka kujiunga na JWTZ,POLISI,na MAGEREZA, kama NCOs [Non Commisioned Officers].
Exactly this my point, tutumikie taifa kwa skills zetu mbalimbali na tuone fahari kutumia elimu yako ya historia kwenda kufundisha shule x.
Hatuna tatizo la pesa...ni tatizo la strategies and priorities zetu kuhusu yale yanayotuzunguka.Kwani tatizo letu ni pesa? Mbona nyingi tu wanatumia kubembea na kuwapa wengine wajiridhishe mfano EPA, IPTL, Richmonduli, RA., Loliondo, Ndulu na hekalu lake, etc etc.
Au kuna wa kulipwa na wengine wasio wa kulipwa?
Hatuna tatizo la pesa...ni tatizo la strategies and priorities zetu kuhusu yale yanayotuzunguka.
Kuna vitu vingap ambavyo havina lolote la kuongeza na kila siku tunapangia hela za matumizi huko?