National Intelligence and State Intelligence

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,985
20,263
Kwenye nchi yoyote ile duniani katika mambo ya utawala na uongozi, kuna kitu kinaitwa National Intelligence na kingine kinaitwa State Intelligence.

National Intelligence huwa ipo kisheria (Legal), na State Intelligence huwa haipo kisheria (illegal). Wanaweza kufanya kazi moja, mahali pamoja, nk Tofauti yao nikuwa kimoja Natinal Intelligence kinafanya kazi chini ya miiko na taratibu za kisheria kwa nchi husika, na State Intelligence hakitambuliwi na sheria yoyote zaidi ya (decree) na mara nyingi huwa hakifahamiki na wengi katika serikali, huenda katika nchi kikafahamika na watu watano au sita tu. Baadhi ya nchi, kila rais au Waziri Mkuu wa nchi huiingia madarakani na watu wake wa State Intel, Katika nchi za kiafrika si lazima wote wawe wamepata mafunzo ya kijasusi, wanaweza kuwa ndugu zaidi, wafanyabiashara, marafiki zaidi nk, ilimradi wanakuwa wapambe wa kiongozi husika.

Nchini Marekani ndani ya shirika la ujasusi la CIA, kuna kikosi kinaitwa Special Activites Division (SAD), Hiki huendesha shughuli zenye maslahi ya rais, chafu, mbaya na pia dhalili zenye maslahi kwa nchi na muda mwingine kwa maslahi ya wakuu katika nchi au katika vikosi husika. Uwepo wacho hautambuliwi na katiba wala sheria yoyote.

Nchini Israel, serikali ya Tel Aviv chini ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu ina kikosi cha siri kiitwacho Kidon, au kwa lugha ya kiswahili kinaitwa ncha ya mkuki, hiki ni kikosi kisichotambuliwa na sheria yoyote ndani ya Israel, na hata utambulisho wa maafisa wake hakuna aujuae. Sehemu kubwa ya shughuli zake ni mauaji na hujuma kwa yeyote anayepinga au kuukosoa utawala wa Tel Aviv, awe wa ndani au wa nje ya Israel. Kikosi hiki kimefanikiwa kuzima harakati zote za kiarabu na makundi yote ya kiislamu yenye msimamo mkali kwakuua mmoja baada ya mwingine.

Nchini Urusi nako ikulu ya Kremlin chini ya Vladimir Vladimirovich Putin ina kikosi ndani ya jeshi kitwacho Spetsnaz ambacho kazi yake kubwa ni kudhibiti wapinzani wa kisiasa na wanaharakati nchini Urusi, kikosi hiki kipo ndani ya shirika la Ujasusi la nchi hiyo la FSB japo kinaundwa zaidi na wanajeshi wa Red Army na hakitambuliwi kwa sheria yoyote ndani na nje ya Urusi.

Nchini Zanzibar kuanzia baada ya mapinduzi mpaka miaka ya 1980+, kulikuwa na kikosi kilichoitwa "viwavi jeshi" hiki kilikuwa ndani ya Idara ya Usalama Zanzibar (ZIS) kilichokuwa chini ya Kanali Seif Bakar, kazi kubwa ya kikosi hiki ilikuwa ni kuwashughulikia wale wote waliopinga ama kukosoa utawala wa Mzee Karume, kikosi hiki kilikuwa kimepata mafunzo ya hali ya juu toka Ujerumani Magharibi.

Kwa namna yoyote, hujuma, uhalifu dhidi ya ubinadamu na ama mauaji ya wanaharakati au wanasiasa ndani ya taifa lolote hayafanywi na mashirika au idara kama taasisi zilizopo kisheria, bali hufanywa na vikosi vya namna hiyo vinavyofanya kazi chini ya amri za kirais (presidential decrees).

Wakati huo katika nchi za Magharibi kama Nchini Marekani, Rais amepewa kinga yakutoshitakiwa kufuatia shughuli za oparesheni za kijasusi zinazofanywa na CIA kwa manufaa ya taifa la Marekani na hata zisizo na manufaa kwa taifa. Kinga hiyo huitwa, AMRI No 12333 (Executive Order No 12333) ya mwaka 1947 ambapo mwaka 2008, ilifanyiwa marekebisho.

Mwaka 1974 hadi 1976, kwenye mapendekezo ya taarifu huru ya tume ya Agranat , ambapo aliyekuwa Waziri Mkuu Israel Bwana Yitzhak Rabin alimteua Jenerali Rehavam Zeevi kuwa mshauri wake, katika mambo ya usalama na ujasusi. Vile vile, Zeevi akawa mshauri wa Waziri Mkuu katika masuala ya vita dhidi ya ugaidi ndani na nje ya Israeli, na akawa pia mwambata wa Mkurugenzi wa Usalama Jeshini, na vile vile, akawa afisa maalumu wa kumtaarifu Waziri Mkuu, juu ya tofauti za kimawazo, zilizokuwa zikijitokeza katika idara na vitengo vya usalama na ujasusi.

Katika maoni yake ya jumla, Jenerali Rehavam alisema, ni udhihirisho uliowazi kuwa uamuzi na matakwa ya vitengo vya siri vya ofisi ya Waziri Mkuu visivyotambuliwa na katiba wala sheria, vina nguvu kuliko mamlaka zilizopo kisheria (akimaanisha mkurugenzi wa Kidon ananguvu kuliko wa Mossad). Hii ilikuwa ni katika kuonya utendaji kazi wa chombo hicho ambapo wakurugenzi wote huripoti kwa bosi mmoja ambaye ni Waziri Mkuu.

Sikufundishi kuelewa, nakufundisha kufikiri maili milioni...

Na Yericko Nyerere

NB

Mods acheni kuvuruga uzi huu, hii sio hoja yakujibu bali ni yatafakuri na kama kuna maoni yabaki kwenye sehemu yake ya maoni....
 
Mnakimbilia sana utamaduni wa magharibi tujenge nchi yetu na maneno mepesi ya kueleweka Kwa hadhira pana

Yericko wew ni mwandishi mzuri sana tabia yako ya kuipenda sana marekani na kuitolea mifana huo ni utumwa wa fikira

Kule twitter umepost habari za kitabu cha fire and fury sasa nikuulize tu maudhui ya kitabu hicho yanamsaidia nn mkulima wa korosho au wananchi wa kawaida wanaoishi Kwa mlo mmoja na pengine Kwa kutegemea ruzuku kutoka Kwa wahisani ndugu na jamaa

Badilikeni

Kijana msomi kama wewe unapaswa kumulika matatizo ya taifa lako na kuyasemea wazi Kwa hadhira bila kumung' unya maneno

Mossad inamsaidia nn mamantilie anaehangaishwa na mgambo wa jiji ?
 
Na Tanzania kipo kinaitwa Panya Road.... Noma sana natamani ningekuwa moja ya hiki kikundi napenda sana kula damu za watu.....
 
Mnakimbilia sana utamaduni wa magharibi tujenge nchi yetu na maneno mepesi ya kueleweka Kwa hadhira pana

Yericko wew ni mwandishi mzuri sana tabia yako ya kuipenda sana marekani na kuitolea mifana huo ni utumwa wa fikira

Kule twitter umepost habari za kitabu cha fire and fury sasa nikuulize tu maudhui ya kitabu hicho yanamsaidia nn mkulima wa korosho au wananchi wa kawaida wanaoishi Kwa mlo mmoja na pengine Kwa kutegemea ruzuku kutoka Kwa wahisani ndugu na jamaa

Badilikeni

Kijana msomi kama wewe unapaswa kumulika matatizo ya taifa lako na kuyasemea wazi Kwa hadhira bila kumung' unya maneno

Mossad inamsaidia nn mamantilie anaehangaishwa na mgambo wa jiji ?
Hayo mambo ya kumsaidia mwananchi wa kawaida uandike wewe.Usimpe jukumu hilo Yericko
 
Kwahiyo ile ya Oysterbay Eagle Wing House inawakilisha National Intelligence au State Intelligence Mkuu Yericko Nyerere? Nasubiri majibu yako nikitambua kuwa hauna mshindani katika haya masuala ya Kijasusi humu JF nzima na umetukuka kabisa kwa Ujasusi.
 
Mnakimbilia sana utamaduni wa magharibi tujenge nchi yetu na maneno mepesi ya kueleweka Kwa hadhira pana

Yericko wew ni mwandishi mzuri sana tabia yako ya kuipenda sana marekani na kuitolea mifana huo ni utumwa wa fikira

Kule twitter umepost habari za kitabu cha fire and fury sasa nikuulize tu maudhui ya kitabu hicho yanamsaidia nn mkulima wa korosho au wananchi wa kawaida wanaoishi Kwa mlo mmoja na pengine Kwa kutegemea ruzuku kutoka Kwa wahisani ndugu na jamaa

Badilikeni

Kijana msomi kama wewe unapaswa kumulika matatizo ya taifa lako na kuyasemea wazi Kwa hadhira bila kumung' unya maneno

Mossad inamsaidia nn mamantilie anaehangaishwa na mgambo wa jiji ?

Mkuu huyo Yericko ameshaandika mengi sana yanayoihusu hii nchi, je yamefanyiwa kazi? Kuliko aendelee kupaka rangi upepo na wakati ana kipaji si ni bora aandike kuhakikisha kipaji chake hakipotei. Halafu ukiona Yericko hafanyi unavyotaka wewe, basi wewe andika kuisifa Tanzania na kuelimisha hao wakulima wa korosho na vijana wengine wa kitanzania.
 
Back
Top Bottom