Nategemea kupeleka hii Hoja yangu binafsi Bunge la August 2013 kuhusu Ajira kwa Vijana

...hoja yako ina tofauti gani na hoja ya Dr.Kigwangala iliyopitishwa(in context)?.......kama umeona hoja yako ina tofauti na ya mwenzako niliyemtaja..kwanini hukuongezea unayoona yana tofauti kwenye hoja ile ambayo ililenga kushughulikia matatizo ya vijana?.........waambie viongozi wako washughulikie implementation ya hoja zilizopitishwa kuwahusu vijana....maana ziko......unachofanya hapa ni unaa tu wa kujaribu kuwaonyesha vijana kuwa unafanya kazi....baada ya kusutwa na jimbo lako.....you still have some time to work for your people though...kama utaacha siasa za taka....
 
Serikali legelege watumwa wake nao wengi wao ni legelege na ngoja fagio laja hakika 2015 siyo mbali kwani hakika tuna MUNGU aliyehai.
 
hahahahaha thats funny kwa kweli....hoja ni nzuri sana, tatizo je ita tekelezeka? je serekali ina hela za kuwalipa hao vijana?...kwani serekali haijui kuwa tatizo la kukosekana kwa ajira kwa vijana na lina ongezeka?...HIZI NI SIASA TU..mfano mzuri ni tatizo la MAJI ubungo, pia mkumbushe mkuu tunasubiri SANA tena kwa hamu list of shame ya wauza UNGA.
 
76001_520488124671683_609135472_n.jpg

Habari vijana wenzangu,

Nategemea kupeleka HOJA BINAFSI BUNGE LA 26 AUGUST 2013 KUHUSU AJIRA KWA VIJANA.
HINTS,
× Kuitaka Serikali iitishe sensa ya wahitimu wote wa fani zote na ifanye uchambuzi wa ikama ya utumishi katika wizara, idara, mikoa, halmashauri- serikali za mitaa, na mashirika yake ya Umma. Lengo ni kujua idadi ya wahitimu wasio na kazi na nafasi zilizowazi.

Utafiti wangu ni kwamba KWA UPANDE WA SERIKALI;
(A) KILA OFISI ya serikali INASHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE ipasavyo KWA AJILI YA UPUNGUFU WA WATUMISHI, HAKUNA OFISI IMETIMIA WATUMISHI

(B) KUNA WATU WENGI SANA WANAKAIMU NAFASI MPK WENGENE WANAKAIMU NAFASI ZILIZOKUWA ZINAKAIMIWA yaani KAIMU KAIMU AFISA UTUMISHI NK NA NAFASI YAKE HIVYO HIZI NI tatu nafasi kwa mtu mmoja

(C) KUNA WATU wanapewa ajira za mikataba na WANAONGEZEWA MIKATABA KWA KIGEZO KUWA HAKUNA MTU ANAYEWEZA KUZIBA NAFASI HIYO au hakuna mwenye uzoefu. KWA UPANDE WA PILI SASA WA WAHITIMU;
(1) KILA MTAA KUNA KIJANA AU VIJANA WAHITIMU WANA MIAKA 2 HADI 5 HAWANA KAZI WANAZUNGUKA NA BAHASHA MPAKA SOLI ZA VIATU ZINAKWENDA UPANDE
(2) KILA MTAA VIJANA WAPO WAKIOMBA KAZI WANAAMBIWA HAWANA UZOEFU wa 2 or 3 yrs, Au anayetakiwa awe na 4yrs experience hata katika ngazi za ofisa wa ngazi za kuanzia ilihali hakuna chuo kinafundisha uzoefu
(3) Vijana wapo na diploma hawajulikani walipo kwa Serikali na wamekaa miaka 2 hadi 5 na diploma zao wanasubiri kazi. kipindi ambacho angewezeshwa kwenda shule angeshavuka diploma na degree angekuwa hata na master.

Kufuatia hali hii:
(i) vijana wanaitwa bomu ili hali VIJANA NI NGUVU KAZI YA TAIFA
(ii) Vijana wana stress, wamekata tamaa hawaoni future na wengine wanahasira sana
(iii) Vijana wahitimu wanatunzwa na wazee ambao hawakwenda shule hivyo kuwa mzigo kwa wazazi.

Lengo ni kuitaka serikali ikishajua idadi ya wahitimu na ikama yake cos ofisi ziko wazi mlioko ofisini mkisema ukweli msiogope mabosi wenu mtakiri hili
(1) Serikali ifanye re allocation ya vijana kwenye nafasi za kazi kufuatana na ujuzi wao,
(2) Serikali ianze kufanya attachment kwa vijana wapate uzoefu maofisini na hata kuwalipa half a saraly of a full employed officer ili kuondokana na tatizo la kukosa uzoefu kwa kijana aombapo kazi.
(3) Vijana wawe tayari kujitolea kulipwa hata half a saraly ili wapate uzoefu
(4) Uwezo wa kazi na marks za kwenye vyeti ni vitu viwili tofauti, serikali ikiwa attach ofisini vijana itajua uwezo wao itaacha kuongezea wastaafu mikataba kwa vigezo kuwa hakuna mwenye uwezo wa kuziba nafasi hiyo
(5) Serikali ibane matumizi yake ili itenge fedha ya kuendeleza wahitimu. Mtu mwenye diploma kusubiri kazi miaka 5 ni kipindi angeweza kuwa na degree na masters yake. Baadhi sehemu za kukata matumizi ya serikali bila kuathiri kazi za serikali ni kwenye magari na mafuta ya magari.

Unakuta bosi anakaa bunju halafu dreva gongolamboto halafu ofisi posta, au bosi kiluvya dreva mbagala ofisi posta kila siku trip hizo, pia training nje ya nchi kwa mtu mwenye 59yrs nakutumia milions and milions zisitishwe ili tuandae generetion ya kupokea majukumu. Pia serikali ikishajua waliopo pia iandae projection ya tunakoelekea in three to five yrs hali itakuwaje na serikali inampango gani. Sababu maisha bora yanaletwa na KAZI.

SERIKALI IKISHAJUA IWEKE BAJETI AMA YA GUARANTEE AU YA KUFUFUA VIWANDA VYOTE VILIVYO LABOUR INTENSIVE ili kuchukua vijana wahitimu na wa mtaani. SENSA HII SIO GHARAMA NI KUWATANGAZIA TU WAHITIMU WAKAJIANDIKISHE KTK OFISI ILIOKARIBU AU KUPELEKA CV kwa DC the cv zinachambuliwa.

This is a rough idear. You can add or improve. VIjanaaaaaaaa, itikieni NGUVU KAZI YA TAIFA.

Ndugu Mwigulu,

Hoja kama hoja haina neno. Ni nzuri tu. Ila inapwaya kama itatokea CCM. Nitakupa sababu:

1. CCM bado indaiwa ahadi ya kutengeza ajira milioni moja mliyoahidi katika ilani yenu ya uchaguzi. Nikichukua viajira mnavyotumia kujitetea vya bodaboda, hatufiki hata robo ya lengo. Sasa ni aibu kama umegundua ndani ya serikali na idara zake kuna nafasi kibao ziko wazi halafu umefahamu kuwa kuna wasomi wengi mtaani halafu mpaka leo hujaripoti kwa mwenyekiti wako wa chama ili muone namna ya kuitekeleza hiyo "ajira 1,000,000"! Hakuna haja ya kupoteza muda wa bunge hilo linaweza kushughulikiwa kama mna lengo la dhati la kutekeleza ahadi na sera zenu. Ila naona harufu ya uleule mtindo wa CCM ya kutafuta pa kuiba na kula. Hapo mtapoteza muda bungeni, ambapo mtakuja na kutengeneza kamati au tume ya kutafiti halafu mje na matokeo ambayo hayatatangazwa hadharani. Hapo nnachoona ni maandalizi ya kuchezea kodi za Watoka jasho wa nchi hii bila sababu ya msingi.

2.Serikali kufanya haihitaji kuambiwa na bunge. Mpaka sasa ilipaswa kujua ina nani kwenye payroll na haina wangapi! Mpaka kufikia hapa kumeshafanyika tafiti nyingi sana ndani ya nchi hii ambazo hazijasababisha mabadiliko zaidi ya kupotea kwa fedha na kulitia hasara taifa. Kumeshaundwa tume kibao za kuchunguza matatizo na ubadhirifu wa mali za umma mara kibao na hakuna kilichotekelezwa mpaka leo. Wewe mwenyewe unajua jinsi mlivyofeli kama wabunge, kushughulikia kashfa za Dowans na Richmond, wizi wa kwenye Rada na Meremeta kati ya nyingi nyingine. Nafikiri kwa sasa tumechoka siasa. Tumechoka kusikiliza vikao vya bunge visivyo na tija. Tunataka MABADILIKO! Nadhani badala ya kupeleka hoja binafsi ya aina hiyo peleka hoja binafsi ya kufufua utekelezaji wa mapendekezo ya kamati teule za bunge na tume mbalimbali, ikiwemo ya Mwakyembe. Hakuna sifa kwenye kukimbilia mbele wakati ulikotoka bado hujamaliza. Ni ujuha na kutofikiria.

3.Hoja yako inamezwa na kasoro kubwa ya kufikiria kuwaajiri vijana serikalini zaidi. Somo zima la ajira haliishii kuajiriwa serikalini. Ni somo pana sana ambalo lingekuwa na ufanisi kama msisitizo ungekuwa namna ya kuwaambukiza vijana kufahamu na kupenda kujiajiri badala ya kuajiriwa. Unaweza usinielewe haraka, lakini ninafikiri kijana akijiajiri na akaweza (kama atawezeshwa kwa utaalamu na mtaji) ni wazi ataweza na yeye kutoa ajira kwa wenzake hata kama ni indirect au hata kama ni kwa watu wawili. Hii itasaidia hata wale ambao hawatakujaajiriwa serikalini wawe na cha kufanya.

4.Sioni nia ya dhati ya kutatua tatizo la ajira kwa vijana. Mpaka sasa tayari kuna vijana wengi walioamua kujiajiri kwa kulima na biashara ndogondogo. Lakini bado wanakutana na vipingamizi vya kukosa masoko na kusakamwa na mgambo kila kukicha. Ili uone na wewe kuwa hakuna nia ya dhati angalia jinsi mlivyowapeleka vijana Machinga Complex, mnataka wafanye biashara na walipe ushuru! Mnafikiri ni nani atapenda kuhangaika kupanda ghorofa wakati kuna wafanya biashara kibao kenye soko la nje pale chini? Ni kwa nini mara zote mnaona ni sifa kuwakamata machinga kwa kuwa wamethubutu kuanza biashara badala ya kuja na njia mbadala ya kuwatafutia sehemu na kuweka visababishi vya wao kufanikiwa? Mbona sioni katika program za ujenzi za serikali sehemu ambapo walau kuna maono ya kuwasaidia kujihifadhi na kufanya kazi vizuri? Kwa wale wanaolima, ni kwa nini hamfikirii kuwasaidia kutafuta masoko ya nje na kusimamia bei kwa masoko ya ndani? Zaidi sana mimi nashangaa jinsi seriakli inavyokuja na mikakati ya kuwazuia wasiuze mazao Rwanda , Uganda , Kenya nk. Mbona wakati wa kulima hamuonekani kujali? Mbona hamsaidii kusimamia bei nzuri ya mazao kwa wakulima mpaka wanalanguliwa kinyonyaji kabisa? Badala yake mnaona ni dhambi wakulima kuuuza mazao kwenye soko linalowafaidisha! Serikali yenu ni ya ajabu sana. Mnawezaje kuhubiri "Kilimo kwanza" wakati you have no Idea masoko yakoje? Hebu tuwe na nia ya dhati katika kutatua tatizo. tuache siasa everywhere everyday!

Majumuisho:

Nadhani ni vema tukajikita kusimamia utekelezaji wa yale yaliyokwishapitishwa na kuamuliwa zamani kwanza. Wananchi tumechoshwa na hadithi za Serikali za miaka nenda rudi na tume kibao zisizotoa matokeo hadharani, wala kutekeleza yale mapendekezo yaliyowahi kutolewa na tume hizo na yaliyoamuliwa na bunge na kamati mbalimbali. Tekelezeni hayo kwanza halafu tuje na mapya!.Ni wakati wa kufuatilia Mapendekezo ya tume na kamati mbalimbali yaliyokwishatolewa. Hakuna haja ya kuongeza kazi mpya ili hali zile tulizokwishazianza hazina dalili ya kufanikiwa!

Ndugu Mwigulu, Peleka hoja binafsi ya kufufua yale yote yaliyoamuliwa bungeni na yaliyotokana na tume kama za kina Mwakyembe ambayo hayajatekelezwa mpaka leo. Hilo la ajira, kamshauri Mwenyekiti wako wa chama taifa namna ya kuliingiza kwenye zile ajira milioni moja,..ilani halali ya chama chako ambayo haihitaji bunge. Inahitaji kutekelezwa tu. Naamini ndugu mwenyekiti atafurahi na kukupongeza sana!
 
Hivi mwenye kiu ya maji huwa anapita na kupiga mbiu kwa watu kwamba jamani nina kiuuuu!!!La hasha anachofanya ni kutafuta maji na kutii kiu yake. Maana yangu ni kwamba kwa nafasi uliyonayo kwenye chama chako unajua wapi pa kwenda na nani wa kumuona ili kama kweli na kwa moyo wa dhati una nia hiyo liweze kufanyika.
 
Ndugu Mwigulu Nchemba inaonekana unayo hoja nzuri tatizo unashindwa kuiandika katika mtiririko unaoeleweka. Mfafute John Mnyika akufundishe jinsi ya kuandika hoja binafsi. Hata mwishoni mwa hoja sijaona ukiandika kwa kufuata muongozo wa kuwasilisha hoja yaani 'Mh Spika naomba kuwasilisha' sasa nashindwa kuelewa hoja hii unaiwasilisha kwenye mkutano wa vijana au kwenye Bunge? Maana umeweka chorus inayoitikiwa na vijana.

Nakala: Matola, Pasco, Kimbunga, Arushaone, Invisible, Mungi, Alfred Yegella, Crashwise, etc

dogo kuwa unasoma uzi hadi mwisho. chini kabisa mwigulu kaandika "this is a rough idea. you can add or improve...." ni mfano wa atakacho kiwasilisha bungeni. maandalizi yanaendelea yakisubiri mchango wako pia
 
Ingawa umeanza vibaya, unaelekea kuzuri. Haya ndo masuala ya msingi ya kujadili. Si kila siku Nitakifuta chadema, mara ooh...bra bra bra. Nilikuwa nakushangaa siku zote.
 
Mh Lissu aliposema majaji wa mikataba, wewe Mwigulu na wabunge wenzako wa CCM pamoja na Mwenyekiti wako, mlimtukana matusi ya nguoni. Leo hii kama kawaida yako Mr. Copycat unarudia yaleyale uliyopinga. Hauoni kama wewe ni kichaa
 
Una kila sifa ya kuwa kiongozi wa nchi na sio jimbo tena, Mungu akupe uhai na afya ili uwezo wako huo uliotukuka uweze kulisaidia taifa kwa urefu na mapana yake.

Binafsi nimependa hoja yako na itakuwa na manufaa makubwa kwa vijana endapo bunge letu tukufu litaridhia kuijadili na kuiunga mkono.

TUNAPOSEMA VIJANA, TUNAKUWA TUNAONGELEA MOYO WA TAIFA LETU, KUWEZA KWAO NDIO KUWEZA KWA TANZANIA.

Pumba hizi bin uhalo.
 
Ha ha ha nmecheka sana leo kumbe Hamy-Dada ndo Mwigulu-mzee unapost,ku comment na ku like Mwenyewe ,we noma umevunja record ya JF-Na hizi ndo sifa unazitaka kwa hii comment ya HAMY-D?lols

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Naona umeanza kuelewa unachopaswa kukifanya kama mwakilishi wa kundi linalo tawala na si mpinzani.pia achana na siasa za uhasama,zaidi ujikite na mahitaji ya Watanzania unao wawakilisha.
Hilo la vijana ujikite pia kuangalia walioathirika na madawa ya kulevya maana wengi wameathirika na wanaangamia huku ma dealer wakiendelea kuneemeka.Tutalaumiwa na vizazi vijavyo.
Nakutakia kazi njema katika ujenzi wa Taifa.
 
Mimi nashauri seriklali ianzishe miradi mbali mbali ambayo itatoa ajira kwa vijana wa taiofa letu.

Kuna miradi mingi ya zamani iliyokufa ambayo ilikuwa inatoa ajira kama vile Relwe, Rtc, NMC , viwanda mbali mbali . nk
Kama serikali ikiweza kufufua hii miradi tatizo la ajira litaweza kupungua kwa asilimia 30
 
76001_520488124671683_609135472_n.jpg

Habari vijana wenzangu,

Nategemea kupeleka HOJA BINAFSI BUNGE LA 26 AUGUST 2013 KUHUSU AJIRA KWA VIJANA.
HINTS,
× Kuitaka Serikali iitishe sensa ya wahitimu wote wa fani zote na ifanye uchambuzi wa ikama ya utumishi katika wizara, idara, mikoa, halmashauri- serikali za mitaa, na mashirika yake ya Umma. Lengo ni kujua idadi ya wahitimu wasio na kazi na nafasi zilizowazi.

Utafiti wangu ni kwamba KWA UPANDE WA SERIKALI;
(A) KILA OFISI ya serikali INASHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE ipasavyo KWA AJILI YA UPUNGUFU WA WATUMISHI, HAKUNA OFISI IMETIMIA WATUMISHI (so what)

(B) KUNA WATU WENGI SANA WANAKAIMU NAFASI (ume-establish hili vipi; kwa nini kukaimu kunatawala?) MPK WENGENE WANAKAIMU NAFASI ZILIZOKUWA ZINAKAIMIWA yaani KAIMU KAIMU AFISA UTUMISHI NK NA NAFASI YAKE HIVYO HIZI NI tatu nafasi kwa mtu mmoja

(C) KUNA WATU wanapewa ajira za mikataba na WANAONGEZEWA MIKATABA KWA KIGEZO KUWA HAKUNA MTU ANAYEWEZA KUZIBA NAFASI HIYO au hakuna mwenye uzoefu. KWA UPANDE WA PILI SASA WA WAHITIMU; (Sababu za ajira za mikataba ni zipi? Je, tunaweza kuwapata watumishi hawa bila mikataba?

(1) KILA MTAA KUNA KIJANA AU VIJANA WAHITIMU WANA MIAKA 2 HADI 5 HAWANA KAZI WANAZUNGUKA NA BAHASHA MPAKA SOLI ZA VIATU ZINAKWENDA UPANDE (bila shaka unao ushahidi wa kitakwimu wa taarifa hii)

(2) KILA MTAA VIJANA WAPO WAKIOMBA KAZI WANAAMBIWA HAWANA UZOEFU wa 2 or 3 yrs, Au anayetakiwa awe na 4yrs experience hata katika ngazi za ofisa wa ngazi za kuanzia ilihali hakuna chuo kinafundisha uzoefu ( nalifikiri unajua vema athari za free market economy Mwigulu?
(3) Vijana wapo na diploma hawajulikani walipo kwa Serikali na wamekaa miaka 2 hadi 5 na diploma zao wanasubiri kazi. kipindi ambacho angewezeshwa kwenda shule angeshavuka diploma na degree angekuwa hata na master (ni vijana wapi unaowazungumzia hapa, maana ni vijana wachache wanaobahatika kupata ufadhili/udhamini wa serikali. Kimsingi hoja hii itaingusha vibaya serikali ya CCM.)

Kufuatia hali hii:
(i) vijana wanaitwa bomu ili hali VIJANA NI NGUVU KAZI YA TAIFA
(ii) Vijana wana stress, wamekata tamaa hawaoni future na wengine wanahasira sana
(iii) Vijana wahitimu wanatunzwa na wazee ambao hawakwenda shule hivyo kuwa mzigo kwa wazazi.

Lengo ni kuitaka serikali ikishajua idadi ya wahitimu na ikama yake cos ofisi ziko wazi mlioko ofisini mkisema ukweli msiogope mabosi wenu mtakiri hili
(1) Serikali ifanye re allocation ya vijana kwenye nafasi za kazi kufuatana na ujuzi wao,
(2) Serikali ianze kufanya attachment kwa vijana wapate uzoefu maofisini na hata kuwalipa half a saraly of a full employed officer ili kuondokana na tatizo la kukosa uzoefu kwa kijana aombapo kazi.
(3) Vijana wawe tayari kujitolea kulipwa hata half a saraly ili wapate uzoefu
(4) Uwezo wa kazi na marks za kwenye vyeti ni vitu viwili tofauti, serikali ikiwa attach ofisini vijana itajua uwezo wao itaacha kuongezea wastaafu mikataba kwa vigezo kuwa hakuna mwenye uwezo wa kuziba nafasi hiyo
(5) Serikali ibane matumizi yake ili itenge fedha ya kuendeleza wahitimu. Mtu mwenye diploma kusubiri kazi miaka 5 ni kipindi angeweza kuwa na degree na masters yake. Baadhi sehemu za kukata matumizi ya serikali bila kuathiri kazi za serikali ni kwenye magari na mafuta ya magari.

Unakuta bosi anakaa bunju halafu dreva gongolamboto halafu ofisi posta, au bosi kiluvya dreva mbagala ofisi posta kila siku trip hizo, pia training nje ya nchi kwa mtu mwenye 59yrs nakutumia milions and milions zisitishwe ili tuandae generetion ya kupokea majukumu. Pia serikali ikishajua waliopo pia iandae projection ya tunakoelekea in three to five yrs hali itakuwaje na serikali inampango gani. Sababu maisha bora yanaletwa na KAZI.

SERIKALI IKISHAJUA IWEKE BAJETI AMA YA GUARANTEE AU YA KUFUFUA VIWANDA VYOTE VILIVYO LABOUR INTENSIVE ili kuchukua vijana wahitimu na wa mtaani. SENSA HII SIO GHARAMA NI KUWATANGAZIA TU WAHITIMU WAKAJIANDIKISHE KTK OFISI ILIOKARIBU AU KUPELEKA CV kwa DC the cv zinachambuliwa.

This is a rough idear. You can add or improve. VIjanaaaaaaaa, itikieni NGUVU KAZI YA TAIFA.

Anyway, kimsingi nimeanza kuamini wanasema kuwa Mh Mwigulu ni kiongozi asiye na visheni. Kwa mfano hii hoja yako haioneshi kuwa tatizo la ajira kwa vijana ni linaanzia wapi, na hata suluhisho unalopendekeza halina uhusiano na tatizo unalozungumzia. Sio kwa vile tuna tatizo la ajira kwa vijana basi itoshe kupeleka hoja binafsi bungeni kupendekeza utatuzi wake, kwa nini basi usifanye utafiti makini kubaini tatizo hili ili tujue endapo tatizo la ajira ni:-

1.tatizo la mfumo wa ajira,
2. ama ni tatizo la sera ya vijana ama sera za ajira na kazi,
3. ama ni tatizo la kutojali kwa serikali
4. ama ni tatizo linalotengenezwa makusudi ili kuongeza pengo la wenye nacho dhidi ya wasio nacho kwa faida ya wenye nacho.

Je, hudhani kuwa tatizo la ajira linachangia kushamiri kwa biashara ya madawa ya kulevya? Na nani anafaidika na biashara hiyo?

Mh. Mwigulu hoja yako hii imepwaya sana na inakuondolea sifa unazojimiminia ati wewe ni msomi na mchumi nambari moja. Ni dhahiri nimethibitisha kuwa huna visheni ya uongozi.
 
Yaani ukweli Mwigulu hilo suala halitekelezeki ni kutaka kutibu ugonjwa kwa pain killer,ni tatizo la sera mbovu za ccm ndo mzizi wake uliko,unataka kutatua ajira kwa vijana wakati mkuu wako wa nchi ajira 1000000 hata baada ya miaka 10 yote hajaweza!!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Assumption yako ni kwamba ukishajaza mapungufu yalipo katika ofisi za serekali utakuwa umepunguza unemployment rate ya vijana.Mi sikuelewi Lameck ni lini utaonesha a little bit of labor economics and macroeconomics even the premises. Before proposing something look whether it is replicable,relevant,sustainable,money value,efficiency and its effectiveness.I am regretting to value you anymore.
 
76001_520488124671683_609135472_n.jpg

Habari vijana wenzangu,

Nategemea kupeleka HOJA BINAFSI BUNGE LA 26 AUGUST 2013 KUHUSU AJIRA KWA VIJANA.
HINTS,
× Kuitaka Serikali iitishe sensa ya wahitimu wote wa fani zote na ifanye uchambuzi wa ikama ya utumishi katika wizara, idara, mikoa, halmashauri- serikali za mitaa, na mashirika yake ya Umma. Lengo ni kujua idadi ya wahitimu wasio na kazi na nafasi zilizowazi.

Utafiti wangu ni kwamba KWA UPANDE WA SERIKALI;
(A) KILA OFISI ya serikali INASHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE ipasavyo KWA AJILI YA UPUNGUFU WA WATUMISHI, HAKUNA OFISI IMETIMIA WATUMISHI

(B) KUNA WATU WENGI SANA WANAKAIMU NAFASI MPK WENGENE WANAKAIMU NAFASI ZILIZOKUWA ZINAKAIMIWA yaani KAIMU KAIMU AFISA UTUMISHI NK NA NAFASI YAKE HIVYO HIZI NI tatu nafasi kwa mtu mmoja

(C) KUNA WATU wanapewa ajira za mikataba na WANAONGEZEWA MIKATABA KWA KIGEZO KUWA HAKUNA MTU ANAYEWEZA KUZIBA NAFASI HIYO au hakuna mwenye uzoefu. KWA UPANDE WA PILI SASA WA WAHITIMU;
(1) KILA MTAA KUNA KIJANA AU VIJANA WAHITIMU WANA MIAKA 2 HADI 5 HAWANA KAZI WANAZUNGUKA NA BAHASHA MPAKA SOLI ZA VIATU ZINAKWENDA UPANDE
(2) KILA MTAA VIJANA WAPO WAKIOMBA KAZI WANAAMBIWA HAWANA UZOEFU wa 2 or 3 yrs, Au anayetakiwa awe na 4yrs experience hata katika ngazi za ofisa wa ngazi za kuanzia ilihali hakuna chuo kinafundisha uzoefu
(3) Vijana wapo na diploma hawajulikani walipo kwa Serikali na wamekaa miaka 2 hadi 5 na diploma zao wanasubiri kazi. kipindi ambacho angewezeshwa kwenda shule angeshavuka diploma na degree angekuwa hata na master.

Kufuatia hali hii:
(i) vijana wanaitwa bomu ili hali VIJANA NI NGUVU KAZI YA TAIFA
(ii) Vijana wana stress, wamekata tamaa hawaoni future na wengine wanahasira sana
(iii) Vijana wahitimu wanatunzwa na wazee ambao hawakwenda shule hivyo kuwa mzigo kwa wazazi.

Lengo ni kuitaka serikali ikishajua idadi ya wahitimu na ikama yake cos ofisi ziko wazi mlioko ofisini mkisema ukweli msiogope mabosi wenu mtakiri hili
(1) Serikali ifanye re allocation ya vijana kwenye nafasi za kazi kufuatana na ujuzi wao,
(2) Serikali ianze kufanya attachment kwa vijana wapate uzoefu maofisini na hata kuwalipa half a saraly of a full employed officer ili kuondokana na tatizo la kukosa uzoefu kwa kijana aombapo kazi.
(3) Vijana wawe tayari kujitolea kulipwa hata half a saraly ili wapate uzoefu
(4) Uwezo wa kazi na marks za kwenye vyeti ni vitu viwili tofauti, serikali ikiwa attach ofisini vijana itajua uwezo wao itaacha kuongezea wastaafu mikataba kwa vigezo kuwa hakuna mwenye uwezo wa kuziba nafasi hiyo
(5) Serikali ibane matumizi yake ili itenge fedha ya kuendeleza wahitimu. Mtu mwenye diploma kusubiri kazi miaka 5 ni kipindi angeweza kuwa na degree na masters yake. Baadhi sehemu za kukata matumizi ya serikali bila kuathiri kazi za serikali ni kwenye magari na mafuta ya magari.

Unakuta bosi anakaa bunju halafu dreva gongolamboto halafu ofisi posta, au bosi kiluvya dreva mbagala ofisi posta kila siku trip hizo, pia training nje ya nchi kwa mtu mwenye 59yrs nakutumia milions and milions zisitishwe ili tuandae generetion ya kupokea majukumu. Pia serikali ikishajua waliopo pia iandae projection ya tunakoelekea in three to five yrs hali itakuwaje na serikali inampango gani. Sababu maisha bora yanaletwa na KAZI.

SERIKALI IKISHAJUA IWEKE BAJETI AMA YA GUARANTEE AU YA KUFUFUA VIWANDA VYOTE VILIVYO LABOUR INTENSIVE ili kuchukua vijana wahitimu na wa mtaani. SENSA HII SIO GHARAMA NI KUWATANGAZIA TU WAHITIMU WAKAJIANDIKISHE KTK OFISI ILIOKARIBU AU KUPELEKA CV kwa DC the cv zinachambuliwa.

This is a rough idear. You can add or improve. VIjanaaaaaaaa, itikieni NGUVU KAZI YA TAIFA.

Ndugu yangu Mwingulu,wazo lako ni zuri sana lakini halitekelezeki.Swala la Serikali kuitisha Sensa ndio umezidi kunichekesha zaidi na kuanza kuwa na wasiwasi na Mtaala wa Uchumi katika Vyuo vyetu maana Wachumi karibu wote mliopo kwenye siasa ni Matatizo matupu.
Nakushauri mjitahidi kudhibiti Mianya ya Ufujaji Fedha za Serikali na Mtimize Ahadi zenu za Uchaguzi kabla ya Kuanzisha kitu Kipya.Najua unataka kucheza Kete ya Kisiasa ili uonekane na Vijana kwamba unawatetea,Madhara yake ni Makubwa kwa sababu hakuna kitakachotekelezeka na hivyo kuiletea Serikali ya CCM aibu kwa Wapigakura.
 
usifikiri watanzania ni wajinga kama wewe. Unaandika post na kujipongeza mwenyewe. Damu za watanzania zitaendelea kukula tu. Haitafika 2015 utakuwa uko chali

-------- wewe huna lolote

una kila sifa ya kuwa kiongozi wa nchi na sio jimbo tena, mungu akupe uhai na afya ili uwezo wako huo uliotukuka uweze kulisaidia taifa kwa urefu na mapana yake.

Binafsi nimependa hoja yako na itakuwa na manufaa makubwa kwa vijana endapo bunge letu tukufu litaridhia kuijadili na kuiunga mkono.

Tunaposema vijana, tunakuwa tunaongelea moyo wa taifa letu, kuweza kwao ndio kuweza kwa tanzania.
 
Back
Top Bottom