SoC04 Serikali itoe "Graduate Loan" kwa maendeleo ya wahitimu wa Vyuo Vikuu na ukuzaji wa Uchumi wa Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

Bando la wiki

JF-Expert Member
May 23, 2023
355
974
Kwa upekee kabisa nipende kutoa pongezi zangu za dhati kwa uongozi wa JF kwa kutuletea jukwaa hili.

Nirudi kwenye mada tajwa hapo juu kuhusu Serikali kutoa mkopo kwa wahitimu wa vyuo vikuu ujulikanao kama "GRADUATES LOAN" ili kuboresha uchumi wao binafsi na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.
Wote ni mashahidi namna kwa hivi kipindi cha karibuni idadi ya wahitimu wa vyuo vikuu inavyoongezeka kupita idadi ya ajira zilizopo katika nchi yetu.

Embu tuangalie Ripoti ya Taasisi ya Utafiti na kupunguza Umaskini Tanzania ( REPOA) ya mwaka 2019, inasema, VYUO vyetu Kwa ujumla wake, vinatoa wahitimu Milioni Moja 1,000,000 Kila mwaka ukilinganisha na nafasi 250,000 zitolewazo na Serikali Kila mwaka.

Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) katika Ripoti yake ya mwaka 2017/2018, inaonyesha kuwa ajira katika sekta binafsi ilishuka Kutoka nafasi 239,017 kutoka 2016/2017 Hadi ajira 137,054 mwaka 2017/2018.

Kwa ripoti hizo tunaona namna kama taifa tulivyo na hali mbaya kwa vijana wetu wahitimu wa vyuo vikuu kwa ukosefu mkubwa wa ajira unao wakabili.
Vijana wanachuo wote wawapo vyuoni, mategemeo yao mkubwa ni kupata ajira haraka sana baada ya kuhitimu masomo yao. Lakini baada ya kumaliza vyuo, mategemeo hayo hubadilika kutokana na hali halisi waikutayo mitaani "HAKUNA NAFASI YA KAZI HAPA"

Madhila yawakutayo wahitimu wa vyuo vikuu mtaani kwenye harakati zao za kujitafutia maisha.
  1. Dharau; wahitimu wa vyuo vikuu ambao bado hawajajipata mtaani wanadharauliwa hadi na watoto wa darasa la saba. Kila anachojaribu kukifanya jamii hadi wana familia wake wanamdharau kwa kuona kwa elimu yake kubwa hastahili kuwa hivyo alivyo au hapo alipo.
  2. Ukosefu wa ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu hasa mabinti wa kike hulazimishwa NGONO zembe kama Rushwa juu ya kupata ajira mahali hapo.
  3. Watoto wa mitaani kuongezeka katika jamii kwa sababu ya hiyo ngono zembe kwa mabinti wahitimu wa vyuo vikuu wanapolazimishwa kutoa rushwa hiyo ili wapate ajira. Mwisho wa siku wanajikuta wamedanganywa na hivyo kujikuta wamebaki kuwa wazazi pekee yao maarufu kama Single Mothers.
  4. Watoto wa mitaani pia kuongezeka kutokana na upande wa wahitimu vijana wa kiume kwa kuamini baada ya kumaliza vyuo vikuu watapata ajira kwa muda mfupi tu hivyo wanaendeleza mahusiano ya kingono kwa kuamini watapata ajira na mambo yaende sawa. Lakini wanajikuta hakuna ajira na majukumu ya kifamilia yanazidi kuongezeka hivyo vijana hao huishia kurumbana kwenye mahusiano yao na mwisho wanaamua kuwatelekezea mabinti hao mtoto/watoto wao.
  5. Ongezeko la msongo wa mawazo kwa wahitimu hao na mwisho kujikuta wengi wao wanadumbukia kwenye uraibu wa madawa ya kulevya na pombe kali. Wakishadumbukia kwenye madawa ya kulevya wanajikuta wanapoteza matumaini na hivyo kuanza kutengwa na jamii.
  6. Ongezeko la wizi na matendo ya kiarifu nchini. Hii ni hatari ya serikali kuwaacha hawa wahitimu kujipambania wenyewe kujitafutia riziki. Kwa kuwa hakuna ajira na wao kama wanadamu wanamaitaji yao hivyo hujikuta wameingia kwenye makundi ya wezi na majambazi kwa ajili ya kujitafutia mkate wao wa kila siku.
Kwa hali yoyote wahitimu wa vyuo vikuu wanapaswa kuangaliwa kwa jicho la kipekee.
Ukuaji wa Uchumi wa taifa lolote duniani unategemea kwa kiasi kikubwa uchapakazi wa vijana wa taifa hilo. Tanzania tuna idadi kubwa sana ya vijana hao ambao wengi wao hawatumiwi ipasavyo katika kukuza uchumi wa nchi.
Serikali kwa kutoa mkopo wa biashara na ubunifu kwa vijana wahitimu wa vyuo vikuu utakaokuwa ukijulikana kama Graduate Loan tunategemea kuleta mapinduzi makubwa ya kijamii na kiuchumi kwa vijana wetu hawa wahitimu.

Masharti na vigezo vya mkopo huu kwa wahitimu wa vyuo vikuu.
  1. Ili muhitimu wa chuo kikuu aupate mkopo huu ni lazima awe amekaa nyumbani zaidi ya mwaka mmoja baada ya kuhitimu chuo. Hii inakuja ili kupunguza risk ya wahitimu wanaohisi bado wao wanaitaji kuajiriwa na hivyo mkopo huu kutoona thamani yake. Mkopo huu ni mahususi kwa wahitimu waliopigika mwaka mzima mtaani pasipo kupata mchongo wowote.
  2.  Mkopo huu ni kwa ajili ya kukuza biashara na uwekezaji wa wahitimu kutoka chuo kikuu hivyo mkopo huu utaenda kuwawezesha vijana katika eneo hilo tu la biashara na uwekezaji wa kibunifu.
  3. Mkopo huu uta range kuanzia wazo au biashara ya milioni 2 hadi million 10 pesa ya kitanzania.
  4. Mkopo huu utakuwa ukitoka kwa awamu ili ku assess utekelezaji wa wazo au mradi wa muhitimu huyo.
  5. Serikali kupitia BOT itatuma pesa hizo kwenye benki zetu maarufu kama CRDB, NMB, NBC na wao ndio watatumia utaratibu utakaokuwa umechakatwa vyema juu ya muhitimu gani anapata mkopo kutokana na wazo lake bora la biashara.
  6. Mkopo huu utakuwa na Grace period ya miezi sita hadi mwaka mmoja kwa muhitimu anaenza biashara. Haiwezekani grace period wawe wanakula tu wawekezaji wazungu kutoka nje huku sisi vijana wetu wazawa wakila msoto kwenye nchi yao wenyewe hili halikubaliki lazima kama taifa tuweke mazingira wezeshi kwa vijana wetu ili waumiliki uchumi wa nchi yao.
  7. Kwa maana hiyo kijana mkopaji kulingana na umuhimu wa wazo lake la biashara ataanza kurejesha mkopo huo baada ya miezi 6 au mwaka mmoja.
  8. Kwa mkopo huu lazima tuwajengee wahitimu hawa nidhamu na uchapakazi ulio tukuka juu ya mikopo hii. Kushindwa kulipa mkopo huo au kushindwa kuendeleza biashara yake, inaweza kupelekea mhitimu huyo kukaa rumande hata kipindi cha miezi 3 hadi 6. Lazima vijana wapambane wathamini dhamana ya mkopo huo kutoka serikalini.
  9. Vyeti original vya muhitimu vitapokelewa na kuchukuliwa na benki kama dhamana ya mkopo kwa muhitimu huyo wa chuo kikuu. Tunachukua vyeti kama dhamana ili kudhibiti mawazo ya wahitimu hawa kuwaza mambo mengi mengi kuhusu kuhajiriwa na hivyo kuvujisha pesa hizo kutoka serikalini.
  10. Dirisha la kutoa mikopo hiyo itakuwa januari ya kila mwaka huku kila mwisho wa mwaka desemba kunakuwa na sherehe za kupongeza vijana wahitimu waliokuza mtaji na biashara kutokana na mkopo huo waliopata kutoka serikalini.
  11. Kadi ya NIDA kila mwaka iwe inaboreshwa ili kuwa na taarifa kamili za kila raia wa Tanzania kuhusu hali yake ndoa, ajira, watoto, uhamisho n.k
  12. Ukamilifu wa taarifa hizo za NIDA zitasaidia kwenye utoaji wa mikopo hii kwa wahitimu kiasi kwamba itakuwa ngumu kwa mtu yeyote yule ambaye siye mhitimu kwa muda husika kupata mkopo huo.
  13. Mikopo mingine kwa vijana, walemavu na wanawake iendelee kutolewa kwa lengo maalum la biashara na uwekezaji pekee. Kama nchi tunataka kuona kila mtu anajishughulisha kwenye biashara inayomuingizia kipato.
  14. Graduates Loan, riba itakuwa ndogo haitazidi 8% baada ya miezi mitatu ili kuruhusu kijana huyu kuona thamani ya uwekezaji wake.
Vijana wa kitanzania hasa wahitimu wa vyuo vikuu lazima watengenezewe mazingira ya kuthaminiwa nchini mwao. Imefikia hatua leo hii wasomi wa chuo kikuu wanaona hata aibu kujitambulisha mtaani kwa sababu tu anahofu watu wakijua elimu yake wataanza kumtolea maneno ya kejeli.
Serikali haiwezi kusema haiwezi kutekeleza wazo hili kwa sababu ya ukosefu wa fedha! La hasha, kwani serikali ikiamua ku sacrifice matumizi yake makubwa ya anasa kama sherehe na kununuliana magari V8 kwa wakuu wa wilaya nadhani wazo hili linaweza kuanza kutekelezwa na vijana wetu wahitimu wa vyuo vikuu tukawa tumewaepusha na msongo wa mawazo juu ya hatima zao.
Sera ya vijana kufanya kazi (biashara na uzalishaji), serikali inabidi kusimamia hilo hata kwa lawama hii ni pamoja na kuwafukuza vijana wanaokaa vijiweni waende mashambani huko kufanya kazi za kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao kwa ajili yetu kama taifa na kwa ajili ya soko la kimataifa.

Vijana wasomi wa vyuo vikuu kuachwa bila kupewa ajira wala mtaji kutoka serikalini au kwa wanajamii kutakuja kuliangamiza taifa kwa staili hii;
  1. Ongezeko la wategemezi kwa vijana wenye nguvu za kufanya kazi.
  2. Uchumi wa nchi kudumaa kwa sababu rate ya Multiplier effect inatokea kwa kiasi kidogo sana maana kundi kubwa la vijana hawapati pesa kwa ajili ya kusukuma biashara kubwa kubwa na uwekezaji kwa ujumla.
  3. Machafuko na umwagaji damu mkubwa utatokea nchi hii kwa sababu wasomi hawa wanaona na inawauma sana namna pesa zinavyotafunwa na kundi la watu wachache waliojipa mamlaka ya kutawala wenzao kwa mgongo wa siasa.
Wanasiasa tusione vijana wasomi wa kitanzania ni wajinga sana kwa kuwa hawafiki hapo tulipo, tukumbuke kila jambo hubadilika kulingana na nyakati inaweza ikapigwa U-turn hapa watawala ndio wakawa watawaliwa na maisha yasiendelee kama tulivyotegemea. Hivyo naimiza usawa katika kuzitumia rasilimali za nchi yetu kwa kuwakopesha mitaji wahitimu wetu wa vyuo vikuu ili waweze kuzifikia ndoto zao za kiuchumi na kusaidia kukuza uchumi wa taifa letu kwa biashara na uwekezaji wao. Lakini pia tukumbuke hakuna mwekezaji kutoka nje atakae tuletea maendeleo tofauti na vijana wetu wasomi ambao faida katika biashara yao inawekezwa katika uchumi wetu hapa nchini.
 
Kwa hali yoyote wahitimu wa vyuo vikuu wanapaswa kuangaliwa kwa jicho la kipekee.
Ukuaji wa Uchumi wa taifa lolote duniani unategemea kwa kiasi kikubwa uchapakazi wa vijana wa taifa hilo.
Ni sawa kabisa, kazi tu.

Ili muhitimu wa chuo kikuu aupate mkopo huu ni lazima awe amekaa nyumbani zaidi ya mwaka mmoja baada ya kuhitimu chuo. Hii inakuja ili kupunguza risk ya wahitimu wanaohisi bado wao wanaitaji kuajiriwa na hivyo mkopo huu kutoona thamani yake. Mkopo huu ni mahususi kwa wahitimu waliopigika mwaka mzima mtaani pasipo kupata mchongo wowote.
Hahahaaaaaah😆, kwamba tuwe na uhakika kwamba kachapika na hajidanganyi tena kwamba ako na options kibao.

Kwa mkopo huu lazima tuwajengee wahitimu hawa nidhamu na uchapakazi ulio tukuka juu ya mikopo hii. Kushindwa kulipa mkopo huo au kushindwa kuendeleza biashara yake, inaweza kupelekea mhitimu huyo kukaa rumande hata kipindi cha miezi 3 hadi 6. Lazima vijana wapambane wathamini dhamana ya mkopo huo kutoka serikalini.
Afadhali umeweka kamfumo ka kuwawajibisha.

Dirisha la kutoa mikopo hiyo itakuwa januari ya kila mwaka huku kila mwisho wa mwaka desemba kunakuwa na sherehe za kupongeza vijana wahitimu waliokuza mtaji na biashara kutokana na mkopo huo waliopata kutoka serikalini.
Mi nnaona ni wazo zuri tu.
 
Back
Top Bottom