Huyu jamaa walikuwa na kundi lao yeye Nate Dogg na wenzake Snoop Dogg na Warren G liitwalo
213 ambalo waliimba nyimbo chache na kabla hawajamaliza hata
Album ya kwanza, Waren G alikuja kumtambulisha Snoop Dogg kwa kaka yake wa kufikia ambaye ni Dr. wa Music aendaye kwa jina la Dr. Dre. Huyu jamaa akiwa mmoja ya waanzilishi wa G-Funky, ndiye aliyekuwa producer mkuu wa Death Raw Record.
Dr. Dre kabla ya hapo, alikuwa chini ya producer na Rapper mwingine ajulikanaye kama Eazy E. Huyu jamaa alikuwa Gangsta fulani na alikuwa akiwazurumu sana wanamusic wengine na kuwalazimisha kufanya kazi kwake mara akishakusajili na ukitaka kukimbia, anatishia au hata kukuuwa. Akina Dre walikuja kuondoka baada ya kupata Mlinzi mwingine mwenye jina la Suge Knight.
Walipomkimbia, jamaa aliimba wimbo kuwatukana na akapaka sana ila Dre akamjibu na wimbo huu chini ambao unamuonyesha huyo Eazy-E ambaye sasa ni marehemu na alikufa kwa AIDS. Huu wimbo ni
DIRTY please. Eve kwenye wimbo wa "Let me blow your mind", anaimba Eazy come, Eazy Go..... ni majumlisho ya kumcheka huyu jamaa Eazy-E.
Dr. Dre akiwa Death Raw Record, ndipo alipoanza kulijenga kundi zima na hii Style yake ya G-Funky ambayo ilianza kupata sifa na umaarufu mkubwa sana na kupendwa dunia nzima hadi leo hii tunapoandika. Humo ndani wakaanza kuja wanamuziki wengine wenye ujuzi wa hali ya juu. Upigani wa kinanda ambacho hasa ndiyo kilikuwa kinaleta radha kwenye G-Funky (G ni Gangsta) ambacho kilikuwa mwanzo kinapigwa na jamaa aitwaye D.O.C. Tatizo dogo la D.O.C. ni kuwa hakuwa mpigaji kinanda mzuri ila alijua kuzitunga BIT nzuri sana za kianda.
Hii hali ilikuja kumalizika na D.R.R ikawa full mara alipoingia Mr. Piano Man aka SCOTT STORCH. Myahudi huyu aliyetokea Canada, kwa kweli alikuwa akilipiga kinanda hadi unakubali. Ukisikia nyimbo nyingi za miaka ya 90 ya Dr. Dre, ni jamaa ndiye alikuwa anapiga kinanda hizo sauti zote nzuri nzuri unazisikia kama EVe-Let me blow your mind, 50-Cents-Candy Shop, Outter Contoll, In da club........, Learn Back-Fat Joe etc.
Ukiangalia hapo juu, utaona kuwa kundi la DRR lilikuwa limekamilika kweli ila kulikuwa kuna tatizo kidogo - RISASI NJE NJE.
Warren G aliwatambulisha wenzake kwa kaka yake Dr.Dre ambaye ndiyo alikuwa na SAY kubwa sana kwenye kundi. Cha ajambu ni kuwa kaka yake aliwachukua Marehemu Nate Dogg na Snoop Doggy na kumwacha mdogo wake. Wengi wanadai kuwa ni kutokana na hizo risasi nje nje ndiyo akamuacha mdogo wake pembeni ili kumlinda na unyama wote unaofanyika kwenye kwenye mchanyato wa Miziki an Ujambazi.
Huu ulikuja kujulikana ukweli mara Suge Knight kugeuka kuwa mbogo na kuwafanyia unyama wenzake. Tupac alipigwa risasi akawa kaondoka na wengine wote wakaikimbia DRR na kwenda mbali sana kujificha huku wakiacha mali zao zote. Snoopy alikimbilia kwa baba yake Lil Romeo aka Master P. Dre aliomba tu ruhusa ajitoe na kuanza kujenga himaya yake upya.
Katika misukosuko hiyo yote, Warren G hakuguswa kabisa na Suge Knight. Pamoja na kuwa hakuwa kwenye kundi kwa kuandikishwa, amekuwa akipata ushirikiano mkubwa sana kwa wana kundi wa DRR na baadaye kwa Himaya mpya ya Dr. Dre.
Marehemu Nate Dogg katika maisha yake alibaki kuwa pembeni mwa Dr. Dre huku akishirikiana na wanamuziki wote walioko kwenye Himaya yake. Nakumbuka kwa mara ya kwanza kumwona akiimba wimbo wa REGULATE LIVE wakiwa na Warren G. Siku hiyo walimkaribisha Snoop atese na wimbo wake wa "What's my name...." Snoop akatokea akiwa kwenye sehemu walizokaa watu (Kama sikosei ilikuwa ni music award) na kusema "Samahani, leo hii mie sintaimba maana nimewaletea Dogg wengine muwaone....." Hapo ndipo dunia nzima ikawaona LIVE Nate na Warren G wakitesa na huo wimbo. Warren G kama Rapper na Nate kama mwimbaji, walikosha roho za watu saaana na ule wimbo nakumbuka ulitesa kwenye chart dunia nzima.
Siyo siri kuwa Snoop Doggy alikuja kuwa juu sana kulinganisha na wenzake. Ila bado mwishoni alikuja na kuwaunganisha wenzie na wakamalizia album yao ya THE HARD WAY. Haikuuzwa sana ila wimbo wa Groupie Love ulipendwa na wengi na hadi leo wengi wanaupenda sana na mie nikiwa mmoja wao. RIP NATE DOGG. Video/nyimbo zake mbili ninazozipenda ukiachia wimbo wa Regulate naziweka kwenye ujumbe mwingine.