Natangaza rasmi kumuunga mkono JK

Natangaza rasmi kumuunga mkono JK

Hivi wasaidizi wakikuangusha kwanini usiwaondoe? Kwanini uongozi wakapewa kishkaji na sio uwezo wa utendaji.
Unasema yeye JK anaipenda nchi saana, LINGANISHA UTAJIRI WA FAMILIA YEKE IKIWA NI PAMOJA NA RIZ1 kabla baba yake hajawa raisi na wa sasa hivi utapata jibu.
Hivi mmiliki wa Richmond ni nani? Tutajua yote 2015. Wewe subiri!
Tulimpenda sana JK, lakini uwezo wake wa kuongoza nchi ni mdogo.

Wewe ni kati ya wale waliompigia kura 2005, muunge mkono mpaka mwisho kaka.
 
Nashindwa nakuelimisha vipi wakati huwezi kuona vitu vidogo vidogo, mfano wasaidizi wake kawachagua yeye, wengi sana wabovu kweli bado unaamini yeye yuko fit?

Ama wewe ni mnafiki au upeo finyu sana, please msaidie kwa kumwambia ukweli

kaka nina upeo wa kutosha, ila ungejua maana ya wana mtandao usingenilaumu au kumulau mkulu, jamaa walimzunguka.
 
Hivi hao wasaidizi wake wanao muangusha ameletewa kutoka Jehanamu na Shetani?
Kama yeye (JK) mwenyewe ndiye aliyewachagua single handed (PM, Mawaziri, PS, Wakurugenzi
CJ, AG, Speaker, RCs, DCs) etc anashindwaje kuwadhibiti/kuwawajibisha kama kweli ndiyo wanao
muangusha?

This is a lame excuse, I'm sorry I can't buy it, try something else.
 
Samahanini nimeona kama amependekezwa mkapa awe mbunge then pm?!! Au sijaona vizuri? Mi huwa na shangaa asa, huyu mkapa alivokua kiongozi amejineemesha kweli kweli, migodi, jet, radar alafu bado tu tumuweke? Then Mkapa ni katili apelekwa ICC kwanza kabla ya upm

chiluba kumbuka 7 x 70
 
siyo siri wenye matatizo ni watumishi wa serikali na ndio wamechangia kudorora kwa uchumi wetu kutokana na uchu na tamaa zao mbaya ipo siku wananchi wataamua kugawana nao hizo mali ndo hapo watakapo lia na kusaga meno si mnakumbuka shamba la balali watu walivyojitwalia mazao yake ipo siku tuuu stay tuned lazima tugawane umasikini!!!!

hata mimi naunga mkono, kama wamezichukua kinyume na sheria wakati ukifika tutazigawana,
 
Ametumia Uhuru wake wa kutoa maoni kama wewe unavyoamini Regardless Lowasa na JK wote wawili hawana sifa za kuwa Marais wa nchi hii.
Tanzania tunahitaji King Cobra wetu kama Michael Sata ambaye atasafisha ufisadi wote nchi hii. Lowasa na JK wote ni mafisadi na wana mikono michafu hakuna mwenye ubavu wa kuleta uadilifu.

Tukumbuke kuwa hata ukiwa mchapa kazi kwa viwango gani lakini kama ni mla rushwa na fisadi wewe hufai, unatakiwa uazishe kampuni zako binafsi kama alivyofanya Mzee Mengi na Bakhresa, hawa wote ni mafisadi ila kwa sababu wanaendesha biashara zao binafsi sisi hatuna maneno nao.

Asante kwa kumjibu maana wengine wanatumia masaburi kufikiria!
 
Bwana Ta Kamugisha,Tatizo hapa ni kansa ya mfumo wa naizesheni uliotapakaa ndani ya uongozi wa Tanzania(unakumbuka nguvu ya Tsunami?). Na kwa bahati mbaya sana Rais ndio Kaizari wetu, ndiye final say kwa Kila jambo. Nani anasaini certificate ya kuongeza posho za wabunge?Nani anateuwa IGP? DPP? PCCB,Mwanasheria Mkuu? Wakuu wa Mikoa/Wilaya? Wakurugenzi? ect? Hatuna mifumo inayojitegemea na inayoweza kujisahihisha na kujiangalia yenyewe. Mifumo hii ilikufa tangu enzi za Mwalimu. Madaraka yote yalikuwa centralized na hivyo kufanya uraisi wa kifalme,na kwa maana hiyo maamuzi yote ya msingi. Hivyo kwa bahati mbaya(nasema kwa bahati mbaya kwa sababu hipaswi kuwa hiyvo) JK ndio mwenye wajibu mkuu wa kuhakihikisha mtumbwi unaelekea kunakotakiwa mpaka hapo mifumo yetu itakapobadilikia. Ndiye mkurugenzi mkuu wa Tanzania na kazi yake ni kuwapata Key Performance Areas hao mameneja wake(Wasaidizi) na kama hawa-perform anawaachisha kazi. Na kama JK halijuwi hili basi hafai kuwa Rais. Hivyo tatizo kuu la serikali yetu kuto-perform ni JK. Aidha naizesheni imemwelemea,uwezo wake ni mdogo, hajali(maana anajuwa nguvu alizokuwa nazo ni kubwa na hamna anayeweza kumfanya chochote) au serikali yake inaendeshwa na waliomweka madarakani(kumbuka nguvu ya Tsunami haikuwa ni nguvu ya umma ila fedha na vyombo vya habari vilitumika kuwatengenezea wananchi nguvu ya umma. Na hivyo kikombe cha uwajibikaji kwa Tanzania hawezi kukiepuka,lazima akinywe

Pm na makinda wamekurupuka, jamaa hajasaini, alisema watumie busara wao wakalopoka! waonyeshe walaka aliosaini jk juu ya kupanda kwa posho.
 
Wewe ni kati ya wale waliompigia kura 2005, muunge mkono mpaka mwisho kaka.

Ni kweli 2005 nilimuunga mkono, lakini akachemsha ndio mana 2010 sikumuunga mkono. Wewe huoni 2005 alipata 80% na 2010 akapata 62% tena kwa kuchakachua. Tena nasikitika kumuunga mkono mwaka 2005
 
Mimi hata sielewi mnazungumzia nini jamani. Nilikuwa nje ya Dar Mwezi mzima na nusu niliacha kilo ya mchele shs 1800 nimekuta 2500. Nataka mabadiliko ya haraka, mambo ya kuunga mkono hayasaidii ndugu yangu.

bora urudi ulikotoka ukawe mkulima, inaonyesha mjini upawezi, wahachie wazawa wa huo mji rudi kwenu
 
Upole uko katika kuongoza nchi tu au hata katika mambo mengine ya kimjini mjini? Maana isiwe katika mambo ya msingi mtu unakuwa mpole ila kwenye mambo ya kipuuzi unaamua kukomaa na mtu mpaka unamkomesha

Ameanzia kwa hao wengine wanafuata.
 
Ulichoandika na ulichoamua kutangaza vinapingana. Kama rais anateua msaidizi halaf msaidizi anaboronga waziwazi na unashindwa kumwajibisha si wewe ndio mwenye matatizo? Kwaufupi ulichoamua ni uamuzi unaoongozwa na njaa kama kibonde

nitake radhi we nusumfu ahaa nimekosea nusumutu, huwezi kunifananisha na kibonde! sina njaa kama unavyonifikiria, ninazo za kunitosha mm na familia yangu ndo maana cjakufuata kukuomba msaada? hacha umasaburi wako.
 
Nani anayetakiwa kuchukua maamuzi magumu kama wateule wake hawaeleweki?
Kuna criteria zaidi ya hiyo moja kumpima kiongozi
Teh teh teh

Jk haitatokea kuwa bora hata siku moja.

kaka umeamua kuchukua nafasi ya marehem shekhe yahaya ya kutabiri!
 
Hamna lolote, Every system should have responsible person on top..for our country the president is the last person..if things are not well he is responsible, if things are well he is also responsible. usimlaumu yoyote, amepewa power over all people and even over the law...he has to use it, unless he will be useless if he can't use his power. Sipendi visingizio hata siku moja..

una uhakika na usemacho?
 
Hivi wasaidizi wakikuangusha kwanini usiwaondoe? Kwanini uongozi wakapewa kishkaji na sio uwezo wa utendaji.
Unasema yeye JK anaipenda nchi saana, LINGANISHA UTAJIRI WA FAMILIA YEKE IKIWA NI PAMOJA NA RIZ1 kabla baba yake hajawa raisi na wa sasa hivi utapata jibu.
Hivi mmiliki wa Richmond ni nani? Tutajua yote 2015. Wewe subiri!
Tulimpenda sana JK, lakini uwezo wake wa kuongoza nchi ni mdogo.

kama uwezo wake wa kuongoza ni mdogo ndo maana namshauri avunje baraza lake la mawaziri ili aweke watakao msaidia si hawa waliopo wazee wa posho
 
Mapungufu ya Jk yanaanzia katika kuchagua watu wabovu hivyo hawezi kukwepa uozo wowote wanaoufanya.

Viongozi wa wizara ya afya hawstahili kujiuzulu bali kufukuzwa, udhaifu wa JK nikuchukua muda mrefu kuchukua uamuzi huo ili angala madakatari waweze kuwa tayari kukaa katika meza ya majadiliano.

Ni wakati huu wa uongozi wa JK kama Mwenyekiti ndipo kila mtu kageuka msamaji wa chama, sasa unafikiri nani wa kubeba lawama kama sio Mwenyekiti mwenyewe? Mbona zamani haikuwa hivyo?

Hapo ndipo utabini udhaifu wa JK wako ambao sisi watoe tumeshaubaini, kama atweaa hilo ulilopendekeza hataweza kwani yeye hutaka kumpendeza kila mtu akiwepo na wakati hawapo huwasema vibaya mbele ya wengine

Haya ndio wote ambao tumepoteza imani naye ulitegemea kutoka kwake mwaka kuaniza 2005 lakini badala yake aktumia uswahiba kuwaweka watu madarakani, matokeo yake ndio haya unayolamikia hata wewe. Sasa nani wa kulaumiwa?

Watendaji wake aliowachagua kwa kuwaamini then wanamwangusha na si yeye wa kulaumiwa
 
Hivi hao wasaidizi wake wanao muangusha ameletewa kutoka Jehanamu na Shetani?
Kama yeye (JK) mwenyewe ndiye aliyewachagua single handed (PM, Mawaziri, PS, Wakurugenzi
CJ, AG, Speaker, RCs, DCs) etc anashindwaje kuwadhibiti/kuwawajibisha kama kweli ndiyo wanao
muangusha?

This is a lame excuse, I'm sorry I can't buy it, try something else.

Mbona anawawajibisha? mfano jairo, lowassa.
 
Ni kweli 2005 nilimuunga mkono, lakini akachemsha ndio mana 2010 sikumuunga mkono. Wewe huoni 2005 alipata 80% na 2010 akapata 62% tena kwa kuchakachua. Tena nasikitika kumuunga mkono mwaka 2005

Majuto uja baada ya tendo
 
Umekiri kuwa jk amepoteza mvuto. Mahali umechemka ni hapo unapompa ushauri. Jamaa ni mwoga, hana uwezo wa kuwapiga chini hata mabalozi wa nyumba 10.
 
Back
Top Bottom