Natangaza rasmi kuanza utabiri

Natangaza rasmi kuanza utabiri

Habari za mchana!

Jamani mida ya saa tano niliona thread inayohusu tukio la uvamizi katika chuo cha sebastian korowa Tanga ambapo majambazi wamevamia na kumuua mlinzi pamoja na kufanya uharibifu wa mali na kupora vitu vya thamani.Kama habari hii ni ya kweli basi natangaza rasmi kuanza utabiri naomba watu wa vyombo vya usalama mlioko humu siku ambayo nikayotoa utabiri humu kuhusu matokeo ya uharifu mchukue tahadhali kwenye maeneo muhimu kuanzia siku inayofuata kwani ndani ya wiki moja hilo tukio litatokea kwani kuna baadhi ya matukio ambayo hua yatafanyika usiku ambao nimeota,siku ya pili yake au ndani ya siku thelasini kuanzia siku inayofuata.

Lakini hua inategemea ukubwa wa tukio yaani kama tukio kubwa sana hua linatokea baada ya mwezi au mwezi,kwa matukio madogo hua yatafanyika usiku,siku inayofuata au ndani ya wiki ya siku inayofuata.Ndoto niliyoiota ambayo naihusisha na tukio hili nalielezea kama ifuatavyo;Juzi usiku wa kuamkia jana niliota ndoto tofauti lakini kubwa ambayo ilichukua mda mwingi ilikua hivi.

Niko eneo fulani ambalo lina vyumba vingi vingi ghafla magaidi wakavamia na kuanza kufanya uharibifu na miongoni mwa mambo ya uharibifu yaliyofanywa na hao magaidi ni kuchoma moto baadhi ya vyumba watu wakawa wanakimbizana huku na kule ili wajiokoe.Kwabahati mbaya polisi wakaja baadae kidogo lakini baada ya mda yakatokea majibizano ya risasi kati ya polisi na hayo magaidi.

Miongoni mwa vitu nilivyoona vimeharibiwa ni gari na mimi nilikua miongoni mwa watu ambao wapo katika tukio wanahangaika ili risasi zisiziwazuru lakini kwabahati nzuri nilisalimika.Yale magaidi yalivyotokomea watu pamoja na polisi wakawa wanazunguka kuangalia vitu vilivyoharibiwa.

Baada ya hapo nikaingia kwenye ndoto nyingine ambayo ilikua ni fupi kidogo ambayo ilikua inaonyesha mtu mmoja ambaye ndio alikua kiongozi wa wale magaidi ananikimbiza na alivyokua ananikaribia namtia vitasa vya kufa mtu lakini nikimaliza nikawa nakimbia nae kwaubishi akawa ananifuata mpaka kuna mda nikawa napaa ili asinishike lakini na yeye akawa anapaa ananifuata ili anizuru lakini mara ya mwisho nikampa vitasa vya mwana ukomo tukiwa kwenye njia panda fulani baada ya vitasa kumkolea akaelekea njia ya kushoto na mimi nikaelekea njia inayoeleke kulia lakini hilo jicho aliokua ananiangalia anaweza kuja tena kwenye ndoto kulipiza kisasi maana vitasa vya mwisho vilivyomfanya aamue kusepa asiporudi basi itakua amefia huke ambapo ameelekea.

NB;simlazimishi mtu kuamini na mimi sio mtu ambaye amekimbia shule au mtu ambaye amechanganyikiwa kwakukosa kazi kutokana na uhakiki wa watumishi hewa unaoendelea kwani nina kazi na kazini nikiingia saa kumi na mbili tu nawasha kiyoyozi peke yangu hakuna mtu ambaye ananichafulia hewa yaani bonge la ofisi.Kinachonifurahisha ni kwamba hata hapa kazini nilipo ni kukamilika kwa moja ya ndoto niliyoota,actually am proud of myself.

Kesho inshaalah ntaelezea ndoto moja miongoni mwa nne nilizoota kuhusu Rais wetu lakini nawaombeni tumuombe sana ili mungu amuepushie.Katika ndoto nne nilizoota kuhusu huyu kiongozi wetu yaani kuanzia mchakato katika chama chake mpaka kua Rais tatu zimeshakamilika bado moja ambayo hata mimi sitaki itoke
Aisee tukishirikiana kufanya collaboration itakuwa POA mnk na mm siyo haba kuona yajayoo na yataka vyo kuwa
 
Daah! Jamaa noma sana. Hongera sana.

Ila umeniacha hoi na hiyo bonge la offisi lenye kiyoyozi unalokaa mwenyewe , najaribu ku imagine. But all in all , wewe ni Noma sana

Respect..
jmaa nimecheka Sana
 
Kwenye ndoto yako ya magu kufariki,kwenye ndoto pia uliota ugonjwa ndo ulimuondoa?
 
Aise kumbe movie hazidanganyi ni vitu vinavyotokea kwenye maisha halisi
 
JF wangefanya mahojiano naye kwa ndoto zote alizoota for branding purpose.
 
Back
Top Bottom