Natangaza mgogoro na mamlaka ya hali ya hali ya hewa

Maseto

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
944
545
Nimekuwa nikifuatilia utabili wa mamlaka hii kwa muda sasa.kati ya tabiri zao 10,naweza kukadiria kuwa ni 2 tu huwa wanapatia.pengine niwashauri wataalam hawa kuachana na kutabiri badala yake wawe wanaelezea tu visababishi vya matukio ya hali ya hewa kama walivyokuwa wanafanya miaka iliyopita.kwa sasa nimeondoa heshima yangu kwao.
 
Ata babu yangu alikuwa accurate kuliko hawa jamaa plus elimu na mishahara juu!
 
Na wewe ndugu yangu kweli na utu uzima wako bado unawaamini watu hawa, yaani utabiri wao ni kama wa marehemu shehe Yahya ni wa kubahatisha yaani nashangaa hata hiyo elimu yao ni ya nini hasa.Walituahidi kuwa mvua za elninio zitaanza kunyesha Dar mwezi huu wa kumi sasa cha kushangaza yalitokea manyunyu tu.

Zifuatazo ni taasisi zikitangaza kitu usikubaliane nazo

TANESCO wakikuambia mgao wa umeme ni historia wewe nunua mishumaa kwa wingi weka ndani maana yake mgao ndo unaanza rasmi
POLICE wakikuambia kuwa tunafanya msako wa majambazi kwa hiyo wananchi muwe na amani wewe nyumba yako nunua vitasa na makufuli ya nguvu
TBC wakikuambia kuwa watatangaza live habari au tukio flan kama una safari yako wewe endelea utakutana na habari hiyo kwenye taarifa ya habari tena ikiwa imechakachuliwa
MAMLAKA YA HALI YA HEWA wakikuambia kuwa jua litawaka wewe nunua mwamvuli maana mvua inaweza ikanyesha tena kubwa na wakikuambia kuwa kuna mvua za elnino kama una shughuli yako wewe carry on tu maana hakuna hata tone la mvua litakalotokea zaidi ya mawingu mawingu
 
Wamejazana Vilaza tu mule ni bora kuwapotezea tu tuwaache wale tu mishahara na nyongeza kila mwaka wapewe nyingi tu
 
tunawalaumu tu je wana vifaa vya kisasa kuona mabadiliko ya hali ya hewa kama wana vya long time na huku kubadilika kwa tabia nchi basi tusitegemee chochote na hata kuwalaumu yaweza kuwa makosa.
 
Nimekuwa nikifuatilia utabili wa mamlaka hii kwa muda sasa.kati ya tabiri zao 10,naweza kukadiria kuwa ni 2 tu huwa wanapatia.pengine niwashauri wataalam hawa kuachana na kutabiri badala yake wawe wanaelezea tu visababishi vya matukio ya hali ya hewa kama walivyokuwa wanafanya miaka iliyopita.kwa sasa nimeondoa heshima yangu kwao.

Hawa jamaa hawana tofauti na wale jamaa waliotabiri kuwa mwisho wa dunia utakuwa tehere 21st May 2011 !!
Ilipofika siku hiyo, jamaa wakatangaza 'kuahirishwa' kwa mwisho wa dunia, mpaka pale itakapotangazwa tena baadaye !!!
 
hawa jamaa yawapasa wa angalie upya premises zao kabla ya kutoka na mahitimisho. Naamini wanatumia measurable quantities,ebu wazifanyie review maana lagging imekuwa kubwa.
 
tunawalaumu tu je wana vifaa vya kisasa kuona mabadiliko ya hali ya hewa kama wana vya long time na huku kubadilika kwa tabia nchi basi tusitegemee chochote na hata kuwalaumu yaweza kuwa makosa.

kama hawana vifaa na hicho wanachotabiri wana base wapi? Kama hawana vifaa ofisini wanafanya nini?
 
hawa jamaa yawapasa wa angalie upya premises zao kabla ya kutoka na mahitimisho. Naamini wanatumia measurable quantities,ebu wazifanyie review maana lagging imekuwa kubwa.

Cha msingi wanapata 'vit M'. Mambo ya kuhangaika na mahesabu ya Dr. Kyando hakuna anayejishughulisha nayo. Wengine wanatafakari chakula cha kuku kam kiepatikana. Maslahi ya jamii baadae.
 
Hawa jamaa wanabahatisha, kwako mleta maada,ume mind kwa nini mvua za elnino hazijanyesha wakati walitangaza hivyo au?
 
Back
Top Bottom