Natangaza kuchukua jimbo tarajiwa la Kahama mjini

Mimi nina kadegree kangu na ndie diwan wa kata ya masama west 2015 na kama mungu akiona inafaa ntakua m/kiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai. Vijana tuamke ndo muda wetu huu!! CDM damu!
 
Umeshawahi kuwa hata Kiranja au Monitor darasani? Ushauri wangu jiimarishe zaidi katika taaluma yako hata kwa 10 years ndipo uwaze kuja katika siasa za kugombea Ubunge!
 
Asante mkuu kwa marekebisho,lakini kuhusu swala la chama mkuu ni CDM .Matatizo nlisema nitaendelea kuyaelezea mbeleni ikiwa pamoja na mipango yangu yote

Go Go Go Kamanda usirudi nyuma kitendo cha kusema tiketi yako ni ya pande ipi Mungu Yu pamoja na wewe!
 
ilo jimbo nasikia kila aliyetangaza kugombea 2015 alikwenda na maji RIP kanumba na wengineo
 
Mkuu km ni CDM naunga mkono hoja. Make Mzee Lemebeli kachoka lkn yuko pale kwa ajili ya kulinda maslahi ya chama chake zaidi kuliko kuwatumikia wananchi
 
Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa mwisho hapa muhimbili, nalitamani na ninatamani sana kuwatumikia wananchi wenzangu wa kahama. Kilichonisukuma sana ni kuona rasilimali nyingi tulizonazo wana wa Kahama ni aibu maisha tunayoishi tukiendelea kutembelea barabara za vumbi ,ugumu wa maisha ukituandama kiasi cha kutishia amani ya wananchi na migodi pia kwa sababu naona ujambazi na matukio ya ajabu yamezidi.

Lakini pia kama kijana nimefikia uamuzi huu kwa kundi la vijana wenzangu likihangaika bila ajira .Pia kilimo chetu maarufu cha pamba na mpunga vinazidi kufifia kwa sababu ya sera mbovu za viongozi wetu walioamua kutufanya maskini kwa makusudi.

nitaendelea kutoa maelezo mengi sana kuhusiana na huu uamuzi ,Pia Wana KHM wenzangu mliomo jamvini endeleeni kunishauri kadri muwezavyo

NAWASILISHA

Kwenye Bold, hayo ni matamshi ya uongo yaliyozoeleka. Kama unatamani kuwatumikia wananchi unaweza kuwatumikia hata sasa, sio lazima uwe mbunge. Sema Unatamani kuwa Mbunge .... Period
 
Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa mwisho hapa muhimbili, nalitamani na ninatamani sana kuwatumikia wananchi wenzangu wa kahama. Kilichonisukuma sana ni kuona rasilimali nyingi tulizonazo wana wa Kahama ni aibu maisha tunayoishi tukiendelea kutembelea barabara za vumbi ,ugumu wa maisha ukituandama kiasi cha kutishia amani ya wananchi na migodi pia kwa sababu naona ujambazi na matukio ya ajabu yamezidi.

Lakini pia kama kijana nimefikia uamuzi huu kwa kundi la vijana wenzangu likihangaika bila ajira .Pia kilimo chetu maarufu cha pamba na mpunga vinazidi kufifia kwa sababu ya sera mbovu za viongozi wetu walioamua kutufanya maskini kwa makusudi.

nitaendelea kutoa maelezo mengi sana kuhusiana na huu uamuzi ,Pia Wana KHM wenzangu mliomo jamvini endeleeni kunishauri kadri muwezavyo

NAWASILISHA

HIKI NI KILIO CHA WAPENDA MAENDELEO WOTE!. Wenye nia ya kugombea udiwani na ubunge kupitia cdm wajitokeze sasa ili waandae kata na majimbo yote ya uchaguzi. Nasi tuanze kupima uadilifu wao!
 
Kijana umeonesha nia nzuri ya kutaka kuongoza jimbo la Kahama...
Sisi kama wana CDM tunahitaji kuona kwanza umekitumikia chama kwa kiasi na muda gani? Tunao vijana wengi hapa Kahama ambao wamepambana katika kueneza sera za chama na kuimarisha chama..

Sidhani kama wewe uko hata kwenye kundi la wapambanaji ndani ya jimbo la kahama... Jenga Chama kwanza kuliko kukimbilia madaraka maana uko shule na hujawa na muda wa kutosha kutumikia CHADEMA.

Peoples Power!!!!!
 
Hakuna njia bora ya kuwatumikia watu kama kufanya ajira nyinginezo zaidi ya uanasiasa. Siasa za baada ya 2015 hazitakuwa lelemama kama unavyodhania. Zipo njia nyingi za kuwasaidia wana Kahama zaidi ya kuwa mwanasiasa. Unaweza kweli ukagombea ukashinda kama akina Mkosamali na Silinde, lakini mbeleni inaweza ikakuachia kovu baya hasa utakaposhindwa kuyafikia matarajio ya watu. Halafu ujue, ubunge wa miaka ijayo, itakuwa ni nadra sana mbunge kudumu zaidi ya vipindi viwili.

Hata hivyo, sitaki kukukatisha tamaa, ukiona inafaa, timiza ndoto zako.
 
Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa mwisho hapa muhimbili, nalitamani na ninatamani sana kuwatumikia wananchi wenzangu wa kahama. Kilichonisukuma sana ni kuona rasilimali nyingi tulizonazo wana wa Kahama ni aibu maisha tunayoishi tukiendelea kutembelea barabara za vumbi ,ugumu wa maisha ukituandama kiasi cha kutishia amani ya wananchi na migodi pia kwa sababu naona ujambazi na matukio ya ajabu yamezidi.

Lakini pia kama kijana nimefikia uamuzi huu kwa kundi la vijana wenzangu likihangaika bila ajira .Pia kilimo chetu maarufu cha pamba na mpunga vinazidi kufifia kwa sababu ya sera mbovu za viongozi wetu walioamua kutufanya maskini kwa makusudi.

nitaendelea kutoa maelezo mengi sana kuhusiana na huu uamuzi ,Pia Wana KHM wenzangu mliomo jamvini endeleeni kunishauri kadri muwezavyo

NAWASILISHA
Endelea katika taaluma yako, hutoweza fanya lolote kama mbunge katika nchi hii zaidi ya kutetea maslahi yako. Hayo uliyo na ndoto nayo yanahitaji kujadiliwa na kukubaliwa bungeni, kupeleka hoja peke yake haitosaidia sana. Kuingia katika siasa kwa nia hiyo ni kujimaliza, ninachoweza kukushauri, endelea na taaluma yako, anzisha NGO ama Foundation itakayowasaidia hao unaotaka kuwasaidia kwa kuwaajili baadhi yao badala ya kutaka kuwasaidia mpaka uwe mwanasiasa ama mbunge. Huihitaji ubunge ama uwanasiasa kuleta maendeleo katika maeneo hayo, tumia ujuzi wako, washawishi vijana, anzisha NGO ama Foundation , tekeleza nia zako za maendeleo, UBUNGE AMA KUCHUKUA KAHAMA MJINI ACHANA NA MAWAZO HAYO. Ni ushauri pia mtazamo
 
Asante mkuu kwa marekebisho,lakini kuhusu swala la chama mkuu ni CDM .Matatizo nlisema nitaendelea kuyaelezea mbeleni ikiwa pamoja na mipango yangu yote

Ni vizuri maana kahama imeharibika tangu mgombea mamuluki kupitia CDM 2010. Lakini wapo vijana wanafanya vizuri ,ninachoogopa ni kuwa katika uchaguzi wa ccm hivi karibuni Bundi nao walipiga kura. Siuamini uchawi lakini kahama na siasa zake kuna mazingaombwe. Karibu tujenge chama na tumpate mgombea makini 2015
 
Kawatumikie Wanakahama kwanza kwa kuwatibu maana kule hakuna madaktari wa kutosha. Baada ya hapo watakuona kwa mema yako. Udaktari ni taalumu adhimu sana. Usijitumbukize kwenye siasa kwa wakati huu. Subiri kidogo
Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa mwisho hapa muhimbili, nalitamani na ninatamani sana kuwatumikia wananchi wenzangu wa kahama. Kilichonisukuma sana ni kuona rasilimali nyingi tulizonazo wana wa Kahama ni aibu maisha tunayoishi tukiendelea kutembelea barabara za vumbi ,ugumu wa maisha ukituandama kiasi cha kutishia amani ya wananchi na migodi pia kwa sababu naona ujambazi na matukio ya ajabu yamezidi.

Lakini pia kama kijana nimefikia uamuzi huu kwa kundi la vijana wenzangu likihangaika bila ajira .Pia kilimo chetu maarufu cha pamba na mpunga vinazidi kufifia kwa sababu ya sera mbovu za viongozi wetu walioamua kutufanya maskini kwa makusudi.

nitaendelea kutoa maelezo mengi sana kuhusiana na huu uamuzi ,Pia Wana KHM wenzangu mliomo jamvini endeleeni kunishauri kadri muwezavyo

NAWASILISHA
 
Naona kila kijana anayetoka Chuo Kikuu anakimbilia siasa, tunahitaji magari na majumba ya fasta fasta,. Mimi nadhani baada ya 2015 siasa haitakuwa na tija, najua Rais wangu Dr. Slaa atapunguza marupu rupu yasiyo na tija, bora imarisha kwanza fani yako
 
Kutumikia wananchi siyo lazima uwe mbunge/mwanasiasa. Kwa fani yako hiyo ya utabibu ni vizuri uwasaidie watz huko mahospitalini!
 
wazo lako ni zuri, kwani nchi inawategemea vijana kama wewe, na sehemu nzuri unayoweza tatua matatizo ya wanakahama ni kupitia siasa, haswa kwenye ubunge, lakini wosia wangu jipange vizuri, shule isije ota mbawa kwani hiyo ni muhas, msalimie kaaya
 
Back
Top Bottom