Natangaza kuchukua jimbo tarajiwa la Kahama mjini

muhas

Member
Apr 7, 2012
21
5
Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa mwisho hapa muhimbili, nalitamani na ninatamani sana kuwatumikia wananchi wenzangu wa kahama. Kilichonisukuma sana ni kuona rasilimali nyingi tulizonazo wana wa Kahama ni aibu maisha tunayoishi tukiendelea kutembelea barabara za vumbi ,ugumu wa maisha ukituandama kiasi cha kutishia amani ya wananchi na migodi pia kwa sababu naona ujambazi na matukio ya ajabu yamezidi.

Lakini pia kama kijana nimefikia uamuzi huu kwa kundi la vijana wenzangu likihangaika bila ajira .Pia kilimo chetu maarufu cha pamba na mpunga vinazidi kufifia kwa sababu ya sera mbovu za viongozi wetu walioamua kutufanya maskini kwa makusudi.

nitaendelea kutoa maelezo mengi sana kuhusiana na huu uamuzi ,Pia Wana KHM wenzangu mliomo jamvini endeleeni kunishauri kadri muwezavyo


NAWASILISHA
 
Ukiweka nukta anza na capital letter, na kwa ujumla jifundishe punctuation.

Nia yako ni njema, lkn hujasema utagombea kwa tiketi ya chama gani.

Pia umeainisha matatizo, lakini hujaeleza kuwa wewe kama kijana utayatatua vipi.

Vinginevyo nikutakie mafanikio mema.
 
we uctuzingue, ulipe kwanza kodi zetu tunazokulipia hapo, na kisha ukawatumikie hospitalini. kahama hawana madaktari wa kutosha, matatizo kwa wanawake na watoto ni makubwa halafu unataka ukawatumikie kivipi, shame on you, kafungue hata kahospitali pale tupia dawa na vipimo vya uhakika tutakuona wa maana
udaktari ni taaluma so katumikie wananchi kwa taaluma yako, ususahau kulejesha mkopo ili na wadogo zako wakope
 
kweli weee ni ngosha yani
mjini unasema "njini"
Ushauri
kazi ya udaktar na ualimu
kuanzi 2015 itakuwa kazi ya
heshima na nzuri sana

kikubwa kawafundishe wana kahama
mjini, ili watambue Chadema vizur kupitia M4C

V
SENGEREMA
 
Ukiweka tamaa mbele yote yatakushinda.
Kama ulitaka kuingia siasa mapema hii muhimbili umefata nini? Si ingetosha kusoma chuo cha diplomasia mahali fulani? Pili kuweza kusaidia wana kahama na tz kwa ujumla huhitaji kwanza kufikiria kulichukua jimbo. anyway nikutakie kila la heri katika azma yako
 
Ukiweka nukta anza na capital letter, na kwa ujumla jifundishe punctuation.

Nia yako ni njema, lkn hujasema utagombea kwa tiketi ya chama gani.

Pia umeainisha matatizo, lakini hujaeleza kuwa wewe kama kijana utayatatua vipi.

Vinginevyo nikutakie mafanikio mema.

:eek:hwell:kweli anatakiwa kufunguka vizuri kwan mpango mzima kwa sasa n cdm kwingineko ataula wa chuya kwa tamaa ya fisi
 
Jiweke bayana tuanze kukupima. Tupe jina lako kamili. Alaf hakikisha uraia wako, ukishaingia kwenye siasa unaweza kupata mshangao kuwa wewe ni mzambia.
 
Asante mkuu kwa marekebisho,lakini kuhusu swala la chama mkuu ni CDM .Matatizo nlisema nitaendelea kuyaelezea mbeleni ikiwa pamoja na mipango yangu yote
 
Kuna kundi kubwa la vijana ambalo linakuja kwa kasi kuchukua madaraka ngazi ya shina,mtaa, kitongoji, kijiji, kata,jimbo nk kupitia CDM viongozi wa CDM toeni mwelekeo (ELIMU) kwa kundi hili!!
 
Hongera mkuu tuko pamoja kamanda na adhima yako itimie!
Asante mkuu kwa marekebisho,lakini kuhusu swala la chama mkuu ni CDM .Matatizo nlisema nitaendelea kuyaelezea mbeleni ikiwa pamoja na mipango yangu yote
 
Yaani nakuona una tatizo kidogo,
Badala ya kufikiria zaidi kuendeleza FANI yako ulioichagua na kuisotea, eti unakimbilia SIASA,
Ndio ni haki yako ya msingi, lakini ungewatibu kwanza hao wana wa Kahama na wengine kwa miaka 10 hivi, ningekuelewa,
Nashindwa kukutofautisha na wachumia tumbo wengine, walioacha taaluma zao na kukimbilia maposho kwenye siasa
 
Back
Top Bottom