Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,889
- 828,475
Najua na natambua jinsi mambo haya yalivyo tayari. Nilishajiandaa kitambo
Sihitaji changamoto zaidi.. Eeh mola wangu nisaidie🙏🏿
Nipe jioni laini, tamu kama chokoleti.
Nipe usiku tulivu na usingizi mnono kama wa mtoto
Nipe ndoto nzuri ili usiku wangu uonekane umevaliwa kama pamba ama sufi nyeupe sana💖
Kukipambazuka, kiza kupotea na mwanga kuchukua hatamu
Tucheke hadi tutoe machozi, pamoja na wale wanaotufanya tuonekane rahisi kutupenda.
Nataka kupumua hewani mwa kila mahali nilipowahi kuota kutengeneza kumbukumbu.
Ingawa magumu yangu yameniumba, kwa njia nzuri na zenye uchungu nitakazoshukuru milele, nataka siku zangu ziwe kamili na zenye upendo.
Nataka kuwa mtu asiye na umbo, mtu anayetembea na kuhama bila wasiwasi.
Unajua Siku zingine mimi hunywa maji. Yale halisi na ya asili
Lakini Wengine, husema hayo sio maji bali ni kimiminika yumbishi😀
Yote mawili ni kweli.
Wote wawili ni mimi... Mm yea maji na mnywa kimiminika yumbishi
Matoleo yangu yote ni ya kweli na muhimu.
Mimi ni nani nisipotambulika na ni kuheshimiwa.? Kupendwa? Kujaliwa hisia zangu za ndani?🤔
Ningependa kuwa marafiki wazuri kwa uchache kuliko kuwa na marafiki wengi unaowachukulia kama ndugu lakini wao mioyoni mwao wanakuchukulia kama mshindani.
Ningependa kukubali watu wengi kuliko kukubaliwa na watu wengi.
Nataka kuwa mtu ambaye wengine wanajua ni salama kumgeukia, kumwamini na kumtegemea
Kuna upole ndani yangu ambao haukuwapo hapo kwanza.. Upole wa hua na si ukimya wa kifutu
Upole wangu uwe nguvu yangu kuu. Kiroho na kimwili..
Ili usiwe mgumu kwa mambo yaleyale yaliyokusudiwa kukuvunja moyo,💪🏿
Hilo ndilo ninalojivunia zaidi.
Kea njia hii kila mtu karibu nami anapata nuru yangu💡.
Kwa njia hii sote tunaangaza. Na dunia itakuwa sehemu salama zaidi kwa kila kipumuacho na chenye uhai!
Mjoli wenu
Jr™ 15.02. 2026