Natamani Magufuli aamuru tuanze kuchimba Uranium.

Kiberiti Kidogo

JF-Expert Member
Jan 14, 2017
575
917
Ukweli ni kwamba nchi yoyote duniani iliyoendelea kiuchumi imepitia au imo katika uchimbaji,uchenjuaji na utumiaji wa madini ya Uranium. Nchi hizo zilianzisha shughuli hiyo bila amri ya nguzo yoyote. Tz tuna uranium lukuki. Magufuli amuru na sisi tuanze uchimbaji wa madini hayo ili na sisi tujikwamue kiuchumi kama wenzetu. Ukweli ni kwamba hata matatizo kama ajira, nishati yatapungua...masuala ya viwanda yataimarika na ndipo tutakapoanza kupiga bao kwenye uchumi wa viwanda. Tz tuna malighafi nyingi sana. Ona Japan, German, south Africa, america wako mbali. Magufuli hebu yatazame haya madini kwa jicho la tatu. Na kingine cha muhimu mkuu masuala ya kuagiza silaha nje ya nchi hayatakuwepo hii itatupa heshima kubwa hata kwa mataifa chokozi kama Malawi, Rwanda, Burundi, Uganda, USA, na Somalia. Vijana wako wapo uwezo wanao. Bilali mwenyewe pale anaelimu ya Nuclear makini mzee wa watu haitumii. Mkuu tinakuomba sana amuru madini haya tuanze kuyafanyia mchakato. Naimani suala la Umeme wa luku, luku!? Halitakuwepo. Sijui symbion na wenzie watasubiri mkuu. Suala la gas na mafuta kama vipo tuchimbe na kuhifadhi tutatumia badae. Saizi tukomae na Uranium. Asante Boss.
 
Uranium inafanyiwa exploration tangu 2007 Mkuju River, ndani ya pori tengefu la Selou huko Namtumbo Ruvuma.
Japo gharama za kufanya hayo unayoyataka nina uhakika hatuwezi kuzimudu lakini pia kasome madhara ya madini ya urani ulete mrejesho.
 
Gharama zake ni kubaa sana.... kwa sasa hatutaweza kuimudu kama nchi. Instead nchi ijenge uchumi wake kwanza
 
Dah napata wasiwasi kama uranium inaweza kuwa mkombozi wetu kwa sababu tuna vitu tele sana vya kuupandisha uchumi wetu ila hakuna kubwa lililofanyika ni kona kona nyingi sana.

Kama Tanzanite, dhahabu,Almasi, utalii, bandari, uvuvi, na mengineyo lukuki yameshindwa kupangwa vyema ili kumkomboa mtanzania vipi uranium iwe mkombozi wetu.

Kichwa kinakataa....mimi naona tuyaache kwanza hakuna lolote hata tukiyachimba tutakuwa vilevile tu, tatizo ni sisi sio rasilimali
 
Uranium inafanyiwa exploration tangu 2007 Mkuju River, ndani ya pori tengefu la Selou huko Namtumbo Ruvuma.
Japo gharama za kufanya hayo unayoyataka nina uhakika hatuwezi kuzimudu lakini pia kasome madhara ya madini ya urani ulete mrejesho.
Uranium unazani inamadhara gani? Husiwe mwanasiasa. Uranium ina madhara gani na ikiwa katika hali gani?
 
Madini mengine tuliyowapa wazungu watuchimbie yametunufaisha vipi?
Madini mengine mkuu kama yapi? Unataka kuitaja dhahabu?! Au tanzanite?! Unajua matumizi makubwa ya dhahabu au tanzanite?! Hivi unajua gram moja ya uranium inaweza kufanya nini duniani?
 
Naimani kabisa elimu ya kikoloni inatutisha hadi sasa!? Angalieni nchi ambazo zinamkiza america na zilizompita uingereza katika utajiri zote zina mambo yao binafsi. Ila sisi tumemeza elimu za mataifa ya magharibi. Why? Madini ya uranium yapo Tanzania for years now? People drill wells and drink water within uranium deposits. Umewahi sikia wamepata matatizo? Tuache uwoga. Magufuli tuingie kwenye mchakato huo na sisi twende mbele.
 
Ahaa.kwa sababu umeona Kim kadinda.ukachukulia rahisi.hayo madini hayachimbwi ovyo ovyo.vinginevyo vikwazo vinakuhusu.rejea ya Iran.
 
Waliopinga vikwazo wote ndowalioshinda kimaisha. Kwann Japan, south Africa, Israel, America, German wanavinuuu. NK nae anavyo? Unazani uranium inaugumu gani? Kwa taarifa yako dhahabu ni ngumu kuipata kuliko uranium.
 
Uranium
Very tricky mineral
Sio rahisi kama unavyochukulia
Kiuchumi, kimazingira, kisiasa yatatuumiza

Nistick zaid kisiasa. Uranium ni "political mineral" kuichimba kwake kunaweza kuzua mengi sana. "Cold War Politics" zinahusiana sana na uranium,

Labda mteja awe U.S.A otherwise tunaingia kwenye mgogoro wa western vs eastern. Wajuz watafafanua zaidi
 
Uranium unazani inamadhara gani? Husiwe mwanasiasa. Uranium ina madhara gani na ikiwa katika hali gani?
INA madhara ya kiafya mfano unaweza pata saratani ya ini,matatizo ya mapafu,ubongo hadi uzazi....
Athari nyingine ni ya mazingiraaaa Elewa uchimbaji wa uranium unachkuaa sehemu kubwa sana ya ardhi ....pia
Na uchimbaji mfano ukiisha ardhi hyo huwezi Tumia tena
Uranium syo kazi rahisi unavyofikiriaaaa

Ova
 
Madini mengine tuliyowapa wazungu watuchimbie yametunufaisha vipi?

Kweli kabisa!
More money, sometimes equals more problems!

Zaidi, chimba madini umalize; kisha utajua mbona nchi zingine hazijaanza kuchimba kwao ilhali waligundua kitambo sana kuhusu uwepo wa madini hayo....
 
Sasa usipotaja dhahabu au tanzanite au almasi utatatja madini yapi?

Unajua kabla ya kuanza kuchimba madini hayo tulikuwa na hazina ya kiasi gani, na hazina hiyo ilitufanya tuwe wenye hazina kubwa nambari ngapi duniani?

Je unajua kuwa tanzanite inapatikana wapi pekee?

Ukiweza kutafakari hayo yote kwa ufasaha bila shaka utanielewa katika hili la Uranium.

Madini mengine mkuu kama yapi? Unataka kuitaja dhahabu?! Au tanzanite?! Unajua matumizi makubwa ya dhahabu au tanzanite?! Hivi unajua gram moja ya uranium inaweza kufanya nini duniani?
 
Back
Top Bottom