Natamani kuwafunda lakini?

Natamani kuwafunda lakini?

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Habari zenu wanajamvi wenzangu humu mjengoni

Nimekaa nimetafakari, nimejiuliza na kujijibu mwenyewe ila nimeshindwa kupata jibu
litakaloniwezesha kukidhi haja ya moyo wangu. Niliyoyaona humu ulimwenguni
yamenifanya nione maajabu na kama sio mazingaombwe hivi ndugu zangu
rafiki zangu wa moyoni hasa ninyi WANAUME makaka zetu.


kwanini mmekuwa ni WAVIVU, MSIOJIJALI na KUWAJALI WENGINE yani mtu
mzima na wala si kipande cha mtu anajijali yeye kuliko mazingira yaliyomzunguka.
Yani hii kitu imenikera sana na nimeona leo niwaseme na kama yuko anatakayefuata
ushauri wangu atapona kama yeye ni sikio la kufa wala halisikii dawa yoyote ya uponyaji
hataponyeka.

Wewe unapenda kwenda na wakati kwa nje lakini kwa ndani umeoza? Kwanini
mnakuwa hivi na kwanini mnajiendekeza kirahisi rahisi na mnasema kuwa wanawake
ndo wachafu wakati nyie wenyewe mmeoza, mnanuka na mnatisha kabisa. samahani
kama kuna mtu anapata picha ya uhalisia wake hapa, ila niko kuwafunda muachane
na tabia hii mbaya, HEBU JALI AFYA YAKO, MAZINGIRA UNAYOISHI NA KUWAJALI WENGINE
Nawapenda nawatakia afya njema na mbarikiwe na kuzidishiwa maradufu
 
Ni kama sijakusoma vile

Kujali mazingira akiaje!!!Kutupa taka Ovyo
Usafi wa mwili au !!!!!!!!


body cleanness but it look like cleanness in general from hair to pubic hair,toe nails,bedroom,muchoo,musuruwali,
Musafi mugeneral
 
Kuna kitu siwezi kukubaliana na wewe kamwe hii ya kusema wanaume ni wachafu. Ukikuta mwanaume ni mchafu jua moja kwa moja mkewe ni mchafu haswa. Mwanamke wajibu wake ni kuhakikisha usafi wa mume. familia na mazingira. Mwanaume wajibu wake ni kuhakikisha kuwa kipato cha kuweza kumudu mahitaji kipo. hii kauli yako naipinga kwa nguvu zangu zote. Siyo kwa kuwa nina mwanaume ninayempenda sana hapana. Kauli imekaa vibaya kama kuvunjiana heshima. pia naona jinsi wanawake mnavyosahau wajibu wenu. More respects to all men.
 
wewe unayejali mazingira wafunze basi...
 
Hii thinking yako ya mwaka 47 hata siikubali. Kwa hiyo mwanamke kazi yake ni kukaa tu na kuhakikisha usafi wa mumewe! 24/7? Umenikumbusha libinamu langu flani mkewe alikuwaga analifuga ile mbaya. Halinunui hata sukari nyumbani wala kulipa ada ya shule, na still mkewe anamnunjlia nguo ili 'asimuaibishe'. Sasa hivi mkewe kamsusa yuko kama senema!

Haya na wanaume wasiooa wenye miaka 30 watafanyiwa usafi wa kitanda na mama zao? Na hata kama ni mke usipate kasafari kwa mwezi ulaya jkirudi unakuta mtu anaishi kama nguruwe? Hata kama usafi unafanyiwa sio kutupa ovyo basi! Manners!
Kuna kitu siwezi kukubaliana na wewe kamwe hii ya kusema wanaume ni wachafu. Ukikuta mwanaume ni mchafu jua moja kwa moja mkewe ni mchafu haswa. Mwanamke wajibu wake ni kuhakikisha usafi wa mume. familia na mazingira. Mwanaume wajibu wake ni kuhakikisha kuwa kipato cha kuweza kumudu mahitaji kipo. hii kauli yako naipinga kwa nguvu zangu zote. Siyo kwa kuwa nina mwanaume ninayempenda sana hapana. Kauli imekaa vibaya kama kuvunjiana heshima. pia naona jinsi wanawake mnavyosahau wajibu wenu. More respects to all men.
 
Si kwa sababu huwa wanawake hawasemi! Mie nna pua sensitive sana na napenda organisation. Kuna wanaume wananuka sijui vitu gani wallah! Yaani hata kama ni ofisini unamvumilia tu ila unatamani kushika pua!
Hii makitu kama sijaisoma vile???

Sijawahi sikia mwanaume mchafu zaidi ya kusikia yule mwanamke mchafu hamjali mumewe
 
Si kwa sababu huwa wanawake hawasemi! Mie nna pua sensitive sana na napenda organisation. Kuna wanaume wananuka sijui vitu gani wallah! Yaani hata kama ni ofisini unamvumilia tu ila unatamani kushika pua!

Mmh wanawake mnavihoja kwelkwl, ila abt dis nadhan t relies 2 personal awareness na c kusema Kwamba flani z responsible 4 nastic outluk ya sombody zaid zaid kwa sababu za ku avoid kuabika pia wyf au husband anaweza take over juu ya usaf wa mwenzie.
Abt mazingira km mtoa Uzi anavyo insist nadhan Mara nyingi nje ya fance za majumba ye2 wengi wana Ile spirit ya kuamini kua Labda Yule flani atasafisha na inakua hivyohivyo pande zote at da mazingira ya mtaa yanakua xo nast
 
ninamaanisha hivi angalia hii picha utaelewa Cleaning-Out-Home.jpgcleaning tiv.jpg
Ni kama sijakusoma vile

Kujali mazingira akiaje!!!Kutupa taka Ovyo
Usafi wa mwili au !!!!!!!!
 
asante kwa kunisaidia kumwambia huyo mdada maaana naona hajanielewa vizuri pale juu
body cleanness but it look like cleanness in general from hair to pubic hair,toe nails,bedroom,muchoo,musuruwali,
Musafi mugeneral
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom