Natamani kumuoa ila.,.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natamani kumuoa ila.,....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kopuko, Feb 8, 2012.

 1. kopuko

  kopuko Senior Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Habari wakubwa wenzangu wa jukwaa hili,,,natumai tu wazima wote wa afya njema..
  nakuja katika jukwaa hili nikitumaini kupata msaada na ushauri kutoka kwenu mana najua kuna watu wengi humu na waliopitia changamoto nyingi pengine hata kama yangu.

  mi ni kijana mwenye makamu ya kutosha tu kuwa na familia,nimeajiriwa na nimejiajiri pia shughuli zangu binafsi zinazo nipa tu kipato cha kutosha japo si sana,kwa hilo nzweza kusema kuwa nimefanikiwa kupata vyote kasoro mwenzi wa maisha tu.

  Labda nijaribu kudokeza historia yangu ya mapenzi ki ufupi pengine itatoa mwanga,,nimeshapita kwenye mahusiano mengi tu ya kutosha,nimefanya uhuni wote na mwingi tu lakini nimekuwa na bahati mbaya ya kukutana na wadada ambao wengi wao ni "wife materia" japo na machakaramu walikuwepo wengi tu..but hawa naowaita ma wife material sikutokea kuwajali wala kujua umuhimu wao,,niliwatenda kuwachanganya na kuwavunja mioyo japo wapo pia walionivunja moyo mimi kwa namna moja au nyingine kwa kunitenda..

  kilichonisukuma kutaka ushauri toka kwenu ni kuwa kila ni lalapo na niamkapo neno kuoa laniijia kichwani,but wa kumuoa simpati,ni kama mwaka nw najaribu kutafuta but kila ninaye mpata sioni kama ametimiza vigezo au kama tunarandana tunaishia kupoteza muda na kuwaambia ukweli waendelee na maisha yao mana mi natafuta mwenzi wa maisha..

  kuna huyu binti mmoja mabaye mara kadhaa ameniijia kwenye fikra,nikajitosa kumwambia ukweli na dhamira yangu bila kujali ya kutaka kuoa na kuwa ni yeye ndiye naye ona ananifaa,,huyu binti miaka kadhaa ya nyuma kama 9 iliyopita aliwahi kuwa mpenzi wangu japo hatukudumu sana,ila tuna vitu vingi sana in common,,tatizo linalokuja ni kuwa anadai ananipenda ila ana mpnz wake amabye hajwahi mtamkia kitu kama hicho,,tunakuwa tukichat mara nyingi tu vizuri but nakuwa na mashaka kama nikifanya sogea nikae kwake itakuwa jambo jema,,yani nikomae mpka nimng'oe jamaa,na kwa kuwa jamaa simjui pia so ni inakuwa ngumu kupigana na adui usiye mjua..

  mkiwa kama marafiki zangu wa humu,naomba mnisaidie mana mpka najihisi nina gundu,,labda wale wanawake wasio kuwa na hatia sas laana yao ndo yanifata sa hv,,pia nawazaga labda sijajichanganya vya kutosha,,mara nyingine nasema labda sijawasilisha swala langu vizuri kwa Mungu au pengine wa kwangu bado hajaumbwa ndo maana.
  ila cha kushangaza magube gube ndo yanajitokeza kila siku

  naombeni ushauri wapendwa cha kufanya wajameni

  natanguliza asante.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  what goes around comes around.

  Anyway siwezi kuhukumu kwa historia yako ya kimapenzi.
  Kinachohusu katika ndoa ni upendo.
  Huyo dada yuko tayari kwa sogea tukae hadi umng'oe jamaa aliyepo?

  Isije akakusogeza, ukakaa afu wewe ukawa small house tu huku ukipoteza muda wa kutafuta wa kuishi naye.

  Be careful
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  wanasema KARMA IS A BITCH........

  vyovyote vile matendo yako yanakurudia......

  ushauri wangu kwako ni kuwa ndo hailazimishwi kwa kukomaa na mtu eti hadi kieleweke....

  hebu jaribu kuacha kutafuta mchumba kama mwaka mzima hivi na ikibidi ufanye maombi....

  halafu watafute wale wooote ulio wakosea zamani ukaombe msamaha au kuondoa 'black cloud' kati yenu....

  jisafishe kwanza kwa sala na kukaa mbali na uzinzi.....na jifunze kuwa kawaida hivi.....
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mng'oe na wewe uje kung'olewa.

  Kama mtu anakupenda kwanini akupe kazi ya kumng'oa jamaa? Si amuache na kuja kwako? Kesho na kesho kutwa akirudi akakuchukulia mke kwakua huyo mke alitoka huko kwa nguvu utamlilia nani?

  Kua makini mwenzio asije akakubaliwa nae baadae kwa kisingizio kama hicho hicho "nna mume wangu ila simpendi/hanivutii kama wewe".
   
 5. kopuko

  kopuko Senior Member

  #5
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kongosho kwa hilo sina uhakika nalo,mana la moyoni mwa mtu ni giza nene,,pia tatizo jingine yupo mbali na mimi,mkoani so ni ngumu kujua baadhi ya mambo
   
 6. kopuko

  kopuko Senior Member

  #6
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  nakuunga mkono swala la kujisafisha na maombi pia aisee
   
 7. kopuko

  kopuko Senior Member

  #7
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  lizzy unalosema ni kweli,but hapa kuna tatizo la distance,hili linafanya ugumu wa kujua status ya uimara ya mapenzi yao,,but nakubaliana moja kwa moja na wewe
   
 8. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  mmh, mzee una bonge la history kiasi kwamba ni bora ungeamua kubaki single tu... halafu mapenzi ya siku hizi bwana, watu hawakupi a clear-cut position, kind of sitaki nataka; yaani mtu anakuachia ka-space ka kupumua (eti nakupenda but nina mpenzi wangu) ili ukijishughulisha kidogo umpate
   
 9. U

  Utamu Member

  #9
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  the boss we unataka mwenzio asipone mwaka mzima
  alafu Mungu anasaidia wanaojisaidia
   
 10. U

  Utamu Member

  #10
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana,ila pia waweza deal na hao magube gube
  wakati mwingine wanaweza kufaa kutegemea na wewe utakavyowaweka
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  wewe utamu ni mwanaume au mwanamke?

  kukaa mwaka mbona sio kazi?
  watu wanakaa miaka...
   
 12. kopuko

  kopuko Senior Member

  #12
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kwa hiyo wanishauri nioe gube gube?
   
 13. kopuko

  kopuko Senior Member

  #13
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hapo ndo nami napojipa moyo wakati mwingine,labda ni pozi tu ila ananipenda ki ukweli kwa upande mwingine
   
 14. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  ulishapiga teke bahati.....

  Anza upya tafuta mwenza mpya
   
 15. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280
  May be na wewe sio Hazibendi material.. maana wanawake wanavyopenda kuolewa afu wewe huoni..,
  By th way, What goes... What comes...
   
 16. Going Concern

  Going Concern JF-Expert Member

  #16
  Feb 8, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 935
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  mwanamke akipenda anapenda kweli, siwezi kukuhukumu kwa kuwaumiza wadada wa watu myb ulikua ni ujana. ila amini usiamini ogopa sana kumuhumiza mtu nafsi yake in future, you will pay it.......

  tatizo la vijana wengi tukiwa tunatafuta mchumba factor kubwa tunayo. consider Mara nyingi ni je? kifaa nachotaka weka ndani ni chaukweli? jamaa zangu wata appreciate? mi naamini wanawake kuna wanawake wengi tu ambao ni wife material ila boys ndo tunamatatizo!!!! tafuta mwanamke unayezani unaweza fanya nae maisha then funga ndoa, dnt care what others are just thinking about you.....ila lazima ukawaombe msamaha wale wote uliowaumiza nafsi zao unless mambo yako yataenda ovyo daima...
   
 17. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #17
  Feb 8, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwani we "nakupenda lakini nna mpenzi wangu" unaitafsiri vipi?
   
 18. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #18
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  could be true i see; huenda anakupima pumzi huyo, ukichacharika kidogo tu unaanua ngoma
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Feb 8, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  njimjoib bj bk kkjkbibvhjhbkonob.k
   
 20. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #20
  Feb 8, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Alafu wewe......?
   
Loading...