vexozanzhu
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 503
- 615
Binafsi nilikuwa simjui ila mitandao ilinifanya nijiulize nilisearch kama mwanzisha uzi ila hola....Zee la unga unataka nimueleze kivipi?
Nijaribu kumueleza km wenzangu?
Muuza madawa ya kulevya utamuelezeaje?
Ilibaki kidogo tu nianzishe Uzi
Ila Katika mambo sikuyafikiria ni watu wenye roho ya aina yako ambao wameegemea uvivu na kuacha kushughulika na maovu yao na kushughulika na maouvu ya watu
inawezekana hapo ulipo una kesi mbalimbali hatuzijui unashughulika na dhambi za Zingizi ambaye kwa watu wanamuombea Pepo. sijui watu unaoishi nao huko wanakuombea nini ingawa unaonekana mkereketwa
jiandae Kiongozi usihangaike na mwenzio keshafanya yake we tengeneza njia yako ya sasa na baadae
Kuna kasumba mbaya sana inayofanywa na watu wabaya wachache kwa kuwasema matajiri wengi vibaya wakishakufa jamii inayobaki inakazana na kubaki na maovu tu, ila juhudi za kazi hawataki kusema alifanya biashara usiku na mchana hawataki kusema, alisafiri alikaa bila kulala hawataki, aliajiri watu na kuwaongoza hawasemi, utasikia tu aliuza unga aliabudu shetani
wanasahu hata wenyewe wanafanya matendo hayohayo mengine mabaya na huku hata maskini hawawakumbuki
Kama kazi ya vipodozi isingempa utajiri kila mwanamnchi angefanya biashara ya vipodozi kama ni rahisi,ni strategy za soko ndo zinazotofautisha biashara moja na nyingine, inawezekana na wewe una duka lako la vipodozi hapo hujatoka ndo maana unaona wenzio Monsterz.
Hata darasani hamkuwa wa kwanza wote lazima kuna walioshika namba sababu ya namna yakufikiri kwa jinsi walivyoweza kujipanga.
Hata zama hizi za sasa ingawa hali ni ngumu kuna watu hawalali wanaumia wanafanya kazi, wanafanya projects, wanafanya biashara ndogo na kubwa,wanapitia shida za kodi,wanatapeliwa,hawakati tamaa, tena biashara wanaifanya kwa upendo kutoka moyoni kuisaidia jamii, halafu siku wakiondoka hapa duniani wanajitokeza watu wanaongea tu kirahisi wanavyojisikia juu ya maisha ya wenzao walioishi hapa duniani.
Mungu akusamehe tu Brother pengine ni roho ya wivu sababu bado hujawin.........
Toba haikuwekwa kwa maksudi yakufanya dhambi ila ni kwa mwenye hekima na uadilifu kutambua lililojema nakubadilika tungekuwa wema sana tungekaa peponi...kungekuwa hamna haja yakupita duniani sababu wote ni malaika.