Natamani kuifunga jela mifupa yake

X-Paster!
Endelea kutumwagia maelezo humu....tupo tunaokuelewa...pia wapo wasiokuelewa!
Naamin hilo walijua!
Nashukuru sana ndugu yangu na wale wengine kwa kuliona ilo, japokuwa wapo wanao chukia kweli inapowekwa adharani.
 
Ya nne..1,2,3,4 nadhani unajua nne inaandikwaje..kwi kwi..nne tena za kueleweka tu sio za madrasa. Shukran za pekee kwa mama yangu aliyehakikisha sikanyagi madrasa maana ningeishia kua zuzu kama wewe.

Wewe inaonekana hzo degree zako hazijakusaidia,mbona unakuwa mdini sana? Nasema hv maana kwenye hoja zako za hapa umekuwa na kashfa kwa jamii ya kiislamu,ebu twambie kwann?
 
Wewe inaonekana hzo degree zako hazijakusaidia,mbona unakuwa mdini sana? Nasema hv maana kwenye hoja zako za hapa umekuwa na kashfa kwa jamii ya kiislamu,ebu twambie kwann?
Mkuu hao ndio watetezi wa sera za Nyerere, hawana hoja zaidi ya kusingizia udini na zaidi ya hapo kuvurumisha matusi, na uku wakijiona kuwa wao ni mahodari sana wa kupinga hoja.

Wacha tuwasubiri...!
 
kaazi kwelikweli

wengine wapo kwenye mchakato wa kumfanya mtakatifu, wengine wanataka kumfukua na kumfunga jela
 
mbona mnamtoe mwezetu kwenye maelezo yake ya awali?
Sisi africans sijui tukoje?
Tumuungeni mkono maelezo yake ili akimaliza ndio tumuelewe zaidi...kupinga pinga tuuuu!!!
Kama kipindi cha mzee MA.k.w.a.iya channel kumi.Je tutafika?
 
mbona mnamtoe mwezetu kwenye maelezo yake ya awali?
Sisi africans sijui tukoje?
Tumuungeni mkono maelezo yake ili akimaliza ndio tumuelewe zaidi...kupinga pinga tuuuu!!!
Kama kipindi cha mzee MA.k.w.a.iya channel kumi.

AHAAA umenichekesha sana hapo kwenye mzee Makwaia, maana yeye anawaita wageni kisha yeye ndio anakuwa msemaji mkuu na ndio anayewawekea maneno aliyewaalika
 
Twambie basi mjahidina mwenzako mwinyi na kilaza mwenzake jk wametusiadia nn ktk nchi hii?
Tatizo lenu vijana wa sasa mnakosa hoja, ila kejeri mmeweka mbele...!

Hapo mmoja umemruka, au habari za Mkapa uzitaki?
 
hivi mwalimu mzuri akikufundisha na wewe ukawa mwisho ni kosa lake?

Ni nini hakutuonya kuhusu EL na JK???

kama uko fair utajua kwamba alituambia tusiwachague sie tukashangilia boyzIImen

tunavuna tulichopanda
Asiyesikia la mkuu huvunjika guu,leo tunayajutia matendo yetu.
 
x pastor akili anayo sanaaa tu'kuna kitu nmeona humu watu wengi wamekimbilia elimu cjui kusoma bure''lakin anachosema x pastor ni kweli nyerere alikosea formation yule''hakutakiwa kukimbilia kwa rusians kipindi kile angepima maji''kipindi vita baridi inatambaa duniani'mataifa makubwa yanauza sera zao''hakutakiwa kabisa kuvamia sera za watu wa mashariki'mzee alichemka mungu amlaze mahari pema kwa sababu kuna watu karne fulani walimuona hero''lakini sisi hapa sasa hvi tunaona alitokota kimtindo''mfano hai tunaona sasa hvi nchi karibu zote za mashariki zilitetereka ktk karne ya 20 na mpaka kuingia 21 ndio znajikongoja kukimbizana sawa na nchi za magharibi'mfano'Rusia,china kati ya mataifa makubwa ambayo BABU YETU alizichagua kupiga nazo dili zilikuwa hoiii ktk karne zile''china imefufuka miaka10 iliyopita na sera zao hawakuziuza kama wanavyouza watu wa magharibi'wenye ubongo mtakuwa mnanielewa nazungumzia nn''alichagua mataifa ambayo sera za usisi na ardhi yetu siyo dili enzi za ambazo wengine wanafikiria kuifanya dunia kuwa kijiji'sa sijui walikuwa wana wazimu ama vipi!!! X PASTOR anasema BABU alimrushia goma MZEE RUKSA Ahangaike nalo nae mzee ruksa cjui alikosa muda wa kusoma vitabu au kuangalia chumi za watu wa magharibi hili abadili formation!!! siwalahumu sana sababu inawezekana walikosa muda au moyo wa dhati hatujui sababu kila mtu na moyo wake!!!basi alivyoondoka babu ruksa na ile sera yake angalau yule mzee alifanya kidogo japo team yake haikuwa nzuri''sababu walichakachua kipindi kibaya''nchi haikufikia kiwango cha kuiibia mabilioni ya hela wakati changa''akajisahau mzee wa watu watu wakaongezeka,uchumi haukotosha kuongeza kiasi cha watu kama hawa waliopo sasa hvi''zkakosekana hela za kuhamasisha uzazi wa mpango,kilimo bora,na mwenendo mzima wa sera za kibepari'wakajifnya kujenga vighorofa viwili vitatu vya kuzugia'nadhani wenyewe mnaona mji kama dar es salaam kua vighorofa cjui vingapi kwa ajiri ya makazi''cjui walisahau kwamba sera za kibepari zinasema 92% wanaishi mjini basi siye imekuwa kinyume 98% ndio wamelikalia ardhi hawajui hata wafanyie nn??basi jamaa wakajisahu pale miaka ikaenda wakaruhusu watu wazijue sera za kibepari kabla hawajajipanga vzuri''na wakasahu kwamba ukuaji wa uchumi wa kibepari wa kileo hautaki majitu mengi kabla haujakomaa mijamaa ikazaliana''wakatuzaa na sisi wengiii mpaka wakashindwa kujenga madarasa,hospital na vyuo vya kutosha hili waendane sambamba na sera mpya'cku zkapita dunia ikawa inaendelea kwa kila baada ya miezi6 sasa cyo miaka100 ya karne zileee au 10 ya karne ya20 kasi ikawazidi wakruhusu watu wajue mambo mengi'wakajua kuandamana,wakajua kususa kugoma kufanya kazi wakati nchi yao haijafika popote''na viongozi wao wakaiba kweli kuogopa kurudi kwenye umasikini walioukuta enzi za babu''masikini marehemu najua tutakutana tu babu''basi wakaiba wakrindana hawakujua kwamba hii cyo sisi tu hata ndugu zao wamo''muda ukapita BABU akajifia masikini huku vijana wake wakifurahi kwa sabbu alikuwa anawazogoa mara kwa mara'kwa sababu walishaanza kuota mapembe hafu wakaona babu alikuwa anzingua tu'walisahu kwamba uko uingereza na marekani ye ndio aliwapeleka'babu akaondoka masikini katuachia ukiwa''MI namkubali X pastor ana akili sna unajua kuna watu humu wanaishi ktk zile sera za ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKTI wakati sasa hvi watu wanafanya kazi kama timu ka archieve''Ukichemka unaambiwa tu''sasa hvi hamna nabii wote tunafanya kazi tulipe kodi hili tujenge barabara,shule,hospital,chakula kingi.
 
Wewe inaonekana hzo degree zako hazijakusaidia,mbona unakuwa mdini sana? Nasema hv maana kwenye hoja zako za hapa umekuwa na kashfa kwa jamii ya kiislamu,ebu twambie kwann?

Una ushahidi ? usitafute mabwana humu ebo
 
Mkuu hao ndio watetezi wa sera za Nyerere, hawana hoja zaidi ya kusingizia udini na zaidi ya hapo kuvurumisha matusi, na uku wakijiona kuwa wao ni mahodari sana wa kupinga hoja.

Wacha tuwasubiri...!

Wewe umeshathibishia umma huu kuwa uko mentally weak and spineless..hamna utachosema watu serious wakakusikiza watakusikiza hao hao wenzako wene utapiamlo wa akili kama wewe.
 
Wewe umeshathibishia umma huu kuwa uko mentally weak and spineless..hamna utachosema watu serious wakakusikiza watakusikiza hao hao wenzako wene utapiamlo wa akili kama wewe.

Easy buddy, let's forgive him and move on cause he's not gonna change, he has some inferiority complex issues with Mwalimu.
 
Natamani Kuifunga Jela Mifupa yake.

Salaam ndugu zanguni wapendwa ndani ya jukwaa hili la JF, ni matumaini mpo na siha njema kabisa. Leo nami najikita kwenye jukwaa la ili. kwa machache ambayo yalikuwa yanapita kama taswira ya picha ya kutisha mbele ya macho yangu, kiasi yakwamba naogopa hata kulala, maana hilo jinamizi ninalo liona kila nikifumba macho linatisha kweli kweli.

Wengi watashtuka na kichwa cha makala haya, "Natamani Kuifunga Jela Mifupa yake." Naam ni kweli kabisa ndugu zanguni, natamani kweli na si uongo, kwani leo nimekaa na kutafakari mengi sana, haswa enzi zile za "Zidumu Fikra za Mwenyekiti wa..." Nakumbuka sana enzi zile ambazo ndio kwanza tumepata uhuru, enzi za matumaini mapya, enzi za kufurahia uhuru tulio upata toka kwa Mwingereza, aliyepewa dhamana ya kutuangalia mpaka pale tutapopata uwezo wa kujitawala, enzi za kujivunia utaifa wetu.

Ni dhahiri kuwa usiku ule wa Desemba 9, 1961 wakati ilipokuwa inashushwa bendera ya Mwingereza na kupandishwa ile ya Tanganyika, wengi walitokwa na machozi ya furaha kila aliyeshuhudia alikuwa na yakini kuwa ule ulikuwa ndio mwanzo wa maendeleo ya nchi yetu Tanganyika.

Maendeleo ambayo yangekuja kuonekana katika hali bora zaidi za kiuchumi kwa taifa na mtu mmoja mmoja, nyumba bora zaidi, kilimo cha kisasa zaidi, usafiri bora zaidi na juu ya hayo elimu bora zaidi na kwa wote.

Kwa kweli matumaini yetu yalikuwa makubwa sana, kiasi ya kwamba wengi walikuwa wakitokwa na machozi ya furaha na matumaini. Matumaini ambayo leo hii yamekuwa ni ndoto za Ali Nacha. Wengi watashangaa hivi leo X-Paster anataka kusema nini, mbona hatumuelewi? Ni kweli kabisa unaweza usinielewe, kwa sasa ila kama utatafakari na kuchambua maisha ya Mtanzania tangia kupata uhuru mpaka leo hii, basi utashindwa kutambua, wapi tulipotoka na wapi tunaelekea na wapi tumesimama.

Lahiti tungalijuwa kuwa Uhuru ule ungetuletea mashaka haya nina ukakika kabisa mashujaa wetu wasingetumia mali zao na muda wao kuondoa ubaguzi wa kikoloni na hata ingekuwa tumepewa uhuru bila ya harakati basi hakuna ambaye angesheherekea kama ilivyokuwa siku ile ya uhuru.

Nakumbuka sana, baada ya uhuru mwaka 1961 viongozi wa nchi yetu tukufu walifanya mengi kwa nia ya kuendeleza nchi hii. Hapa kuna machache niliyoweza kuyakumbuka baadhi ya hayo ni kama ifuatavyo:

1961 - Uhuru wa Tanganyika

1962- Jamhuri ya Tanganyika

1964 - Muungano Tanganyika na Zanzibar na kuzaliwa nchi mpya iliyokuja kujulikana kwa jina la Tanzania

1967 - Azimio la Arusha

1971 - Madaraka mikoani

1980's - Vita dhidi ya wahujumu Uchumi

Bila kusahau U.P.E, vijiji vya ujamaa, maduka ya kaya, elimu bure, kutaifisha majumba, mashamba n.k.

Kwa wakati ule nyimbo nyingi zilitungwa kupongeza kila hatua iliyochukuliwa. Kwa bahati nzuri miaka yote ya sitini na sabini iliwashuhudia Watanzania chini ya utamaduni wa kuheshimu na kuthamini sana viongozi wao, hivyo moyo wa uzalendo ulijitokeza wazi wazi.

Hali hii ilijitokeza hasa pale wananchi walivyozitii hata amri ambazo bila shaka hata serikali iliona tabu kuzitekeleza, mfano kuanzishwa vijiji vya ujamaa, kutaifisha majumba, mashule na mashamba ya katani, pamba n.k.

Tuliambiwa na tukaamini kuwa Tanzania haiwezi kuwa huru hadi Afrika yote iwe huru. Serikali yetu tukufu ikiongozwa na fikra sahihi za mwenyekiti ilitumia kila uwezo uliokuwa nao kufikia lengo hili. FRELIMO, MPLA, ANC, SWAPO walifaidi sana msimamo wetu huu.

Tuliambiwa Idd Amin ni nduli anayetumiwa na mabwana zake ili kuzorotesha harakati za ukombozi wa Afrika. Tulikubali hili watu walitoa mali na roho zao kuikomboa ardhi yetu na kumpa adhabu kidogo ndani ya mipaka ya nchi yake.

Haya yalifanyika bila mtu yeyote kuhoji kwa vile wengi walidhani kufanya vile ni katika harakati zile zile za kutuletea maendeleo.

Wazalendo wale ambao enzi zile walijulikana kama Makabwela, yaani watu wa kipato cha chini, leo hii tunajulikana kwa jina la Walala Hoi, na haswa wanaoishi mikoani wanaweza zaidi kuona kile ninacho kizungumza... Si ajabu uko mikoani na haswa ukitembea siku ya soko au gulio ukamwona dalali akiuza kitanda cha kamba... karne hii.

Mimi bado najiuliza sababu ya huu umasikini ni nini haswa. Tulikuwa tunaambia kuwa ili nchi iendelee tunaitaji mambo manne, Ardhi, watu, siyasa safi na uongozi bora… Je hivi vyote kweli hatuna hata kimoja…!?

Nasema tena kwa sauti kubwa kabisa , serikali ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere haikuwa nzuri kwenye mipango ya uchumi, ni bora tungeendelea kutawaliwa na Mwingereza, kuliko serikali hii iliyo hasisiwa na Mwalimu Nyerere. Nadiriki kusema kuwa Wakoloni walikuwa bora kuliko Nyerere kwa mipango ya uchumi mizuri kwa ajili ya nchi hii. Hao wakoloni tulio waondoa ndio hao hao waliotuletea mazao mbali mbali ya kiuchumi, kama vile Pamba, Katani , Chai, Kahawa, Korosho na kadhaa wa kadhaa, na haya mazao yaliletwa ili kutegemeza uchumi wa nchi hii, na ni kweli waliona mbali, kwani mazao hayo mpaka leo hii ndio yanasaidia nchi yetu, lakini cha ajabu serikali iliua mashamba yote makubwa na hata hao wakulima wadogo wadogo wa mazao hayo, serikali haikuwajali.

Kipindi cha utawala wa Nyerere kwa kweli ni kipindi ambacho serikali yake ishindwa kuendesha uchumi wa nchi. Hata pale alipo amua kuanzisha Azimio la Arusha kama njia ya kujikwamua kiuchumi, bado hatukuona nafuu yoyote ile kwa mlalahoi, au makabwela. Na Kwa bahati nzuri mtoto yule aliyejulikana kwa jina la Azimio la Arusha alimfia mikononi kabla hata mzazi wake hajafariki. Hata ile siyasa ya Ujamaa na kujitegemea aliyopanga na wachumi wake uchwara, nayo ikapata ugonjwa wa kifaduro. Nayo akaishuhudia ikimfia mikononi.

Sera za ujamaa na kujitegemea kwa kweli hazikuwa sera nzuri hata kidogo. Na hata alipo ambiwa kuwa sera ni mbovu, badala ya kufuata ushauri wa kitaalam, yeye akatumia sura na maumbile yake akichanganya na uongozi wake na umahiri wa kuzungumza na kuvutia kuzitetea sera zake mbovu mpaka nchi ya Tanzania ikaangamia. Kusema kweli Mwalimu Nyerere alikuwa ni mahiri sana kwenye kutoa hotuba za kuvutia na zenye kuleta matumaini mazuri, maneno yake kwa kweli yalijaa ushawishi wa hali ya juu sana. Lakini ukija kwenye matendo ya zile hotuba nzuri hakuna hata kijiji kimoja cha maonyesho kuonyesha kuwa alifanikiwa kwenye sera zake. Hivi leo hakuna kijiji hata kimoja ambacho kinafahidika na sera zile za ujamaa na kujitegemea.

Nakumbuka aliyekuwa rais wa Kenya enzi hizo (Jomo Kenyatta) aliwahi kumwambia wanahabari kuwa "kama unataka watendaji wazuri katika sekta ya mbalimbali njoo Kenya na kama unataka wahutubiaji wazuri kila eneo liwe la siyasa, uchumi, biashara, kilimo n.k basi kwenda Tanzania kamwambie Nyerere akupe anao tele"

Ni kweli kwani ile siyasa ya ujamaa iliwaharibu sana viongozi wa taifa ili. Nyerere alitengeneza wahutubiaji wazuri si watendaji na wachapa kazi wazuri kwani karibia wote walipitia vyuo vya siyasa. Alipenda sana watu ambao kazi yao ni kuimba kwa nguvu hadi kufoka mate mdomoni kwa kusema "Zidumu fikra za mwenyekiti..." . Na wala sishangai maana hata leo na hata hao walio upande wa pili wenyewe wanajiita vyama vya upinzani wengi wanaiga tabia ya Nyerere ya kuwa wahutubiaji wazuri kuliko kuwa watendaji na wachapa kazi.

Na kwa kawaida sehemu yoyote ile maendeleo hayawezi kuja hivi hivi, lazima yafanyiwe kazi ili yapatikane. Kazi hiyo haitegemewi kufanywa na mwingine yoyote isipokuwa watawala na watawaliwa (serikali na raia).

Watawala ndio wenye jukumu la kupanga na kuratibu mipango na kutafuta njia za kusaidia utekelezaji wake ili watawaliwa waweze kufanya hayo ambayo yameshapangwa. lakini watawala wetu wale walikuwa kama wafalme, kazi yao ilikuwa kunyoosha vidole tu, bila kuonyesha mifano hai.

Mpaka leo hakuna ambaye anaweza kutuambia, ni ugonjwa gani uliotupata Watanzania, baada ya kutaifisha mashirika na mashamba. Tulikuwa na mashirika mengi tulio yaita ya Umma kama vile Viwanda vya nguo vya Urafiki, Sunguratex, Mwatex na kule Musoma pia kulikuwa na kiwanda cha nguo, ila sina uhakika kama bado kipo, tulikuwa na kiwanda cha kusindika nyama, Tanganyika Packers, kiwanda cha viatu kule Morogoro, na kile cha dar, pia kulikuwa na RTC na Ugawaji na mengine mengi. Yote haya leo ni marehemu na makaburi yake yashafutika kwenye ulimwengu wa Mtanzania.

Serikali yetu baada ya kutaifisha mashirika na makampuni na kukuta pesa nyingi kwenye hayo mashirika, wakaona bora kuanzisha vikundi vya sanaa vya mashirika ya umma. Vikundi ambavyo vilikuwa si vya uzalishaji mali, bali vilikuwa vinapata ruzuku kwa asilimia mia 100% kutoka kwenye hayo mashirika. Vikundi vingi kufikia mwishoni mwa miaka ya themanini 1980 vingi vilianza kudolola. Mashirika mengi yalianza kupungukiwa na uwezo wa kuviendesha vikundi hivyo kwa sababu nayo yalikuwa taabani kifedha.

Huwa najiuliza wakati mwingine, ni vipi bidhaa kama Pamba, Katani au bidhaa kutoka kwenye mashamba au makampuni ulio dhurumu, yaani umuuzie yule yule uliye mnyang'anya, hivi inaingia akilini kweli!?

Fikra zangu zika ambaa ambaa,mpaka zile enzi ambazo JKT walishirikiana sana na askari polisi kulinda viongozi na kukamata raiya, kisa wamemkuta na dawa ya meno au kipande cha sabuni ya mchubuo (tulikuwa tunaita sabuni ya pundamilia). Ukikamatwa na dozen moja ya sabuni ni muhujumu uchumi, hakuna ruhusa ya kuweka wakili wa kukutetea...!

Nakumbuka ili kuangalia TV, mpaka kipindi cha sikukuu ya sabasaba kwenye banda la Yahaya Hussein, hii ni kwa wakazi wa jiji la DSM, Sijui uko mikoani hali ilikuwaje. Nakumbuka sana zile nyimbo za kina marehemu Mzee mzima Pepekale, Rechereau (tamka Rosherou) au Tabu Ley, Franco Luambo Makiadi Mzee wa o.k Jazz na wengine wengi.

Zaidi ya hapo kila kitu kilikuwa kwa foleni, nchi nzima shule za sekondari za kuhesabika kwa vidole vya mkono. Chuo kikuu kimoja tu, kama kimejaa basi, subiri mwakani au ndio basi tena. Ilifikia wakati hata ukiwa na gari zuri basi wewe ni bepari kila kitu kwa kibali, ukiona gari aina ya Benz basi hiyo ni mali ya Ikulu, watu binafsi si rahisi kumiliki gari kama hiyo yaani hata kuvaa suti ni ubepari. Nakumbuka mwaka mmoja aliyewahi kuwa naibu waziri mkuu salim Ahmed Salim, alikuwa Mtwara anahutubia wengi wa wale walio hudhuria walikuwa wamevaa majunia ya mbolea kama nguo.

Baada ya kutawala zaidi ya miaka ishirini na kushuhudia kila kitu kikishindwa na maji yapo shingoni, yanakaribia kuingia mdomoni, kiujanja ujanja na kiutu uzima akaamua kutoroka uongozi, ndio akamtupia Mwinyi maiti akitegemea miujiza ya kufufuliwa, alisha sahau kuwa enzi za wafu kufufuliwa zilisha pita... Akasingizia kuwa anan'gatuka mapema. Kumbe alikuwa ameshindwa kuendesha uchumi wa taifa ili.

Ndio maana leo hii kila nikikumbuka madhira ya utawala wake inanifanya nitamani kwamba mifupa yake ipelekwe gerezani. Kwani ni yeye aliyeasisi siyasa na sera mbovu dhidi ya taifa ili la Tanzania, na mpaka leo hatujainuka tena.

Mkuu X-PASTER, mara nyingi sana mitazamo yetu katika mijadala mbali mbali hapa jamvini huwa inashabihiana sana ukiondoa michache na hasa huu wa Baba wa Taifa. Mwalimu kama kiongozi na pia binadamu alikuwa na mapungufu yake mengi tu lakini kama kiongozi kaifanyia mazuri mengi Tanzania na Watanzania ukilinganisha mabaya aliyoyafanya akiwa madarakani. Pia kafanya mengi katika ukombozi wa ncchi za Afrika ambazo zilikuwa bado ziko chibi ya Wakoloni.

Mazuri aliyofanya Mwalimu kamwe hayatafikiwa na awamu zote tatu (Mwinyi, Mkapa na Kikwete) zilizo kuja nyuma yake mara baada ya kung'atuka madarakani mwaka 1985. Watanzania mbali mbali katika nchi za nje asilimia kubwa ya hao wanatokana na sera za Mwalimu za kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu bure kuanzia shule za msingi hadi chuo kikuu.

Sasa hakuna Azimio la Arusha na kutukuwepo kwake kumechangia kuibuka ufisadi wa kutisha unaofanywa na hadi Viongozi wa juu kabisa wakiwemo Marais, jee unaweza kuita hali ni bora kuliko ile tuliyokuwa nayo wakati wa Mwalimu?

Sasa hivi hakuna siasa ya ujamaa na kujitegemea je, unaweza kusema Watanzania walio wengi wanaishi maisha bora ukilinganisha na wakati wa sera za ujamaa na kujitegemea za Mwalimu?

Miye pamoja na kujua kwamba Mwalimu alikuwa na mapungufu mengi kama binadamu na kiongozi lakini naamini kabisa kaifanyia Tanzania na Afrika mazuri mengi ambayo yatakumbukwa na wengi kwa miaka mingi ijayo. Na hili la kuifunga mifupa ya Mwalimu, sijui alikukosea nini hadi ufikirie kitu kama hiki. Nakuomba umuache ili apumzike kwa amani. RIP Mwalimu.
 
Usemayo ni kweli kaka, kuna baadhi ya mitazamo huwa tunakubaliana, ilo sikatai mkuu wangu. Lakini ili la Mchonga, wacha tu tutofautiane mitazamo as long as kila mmoja anaheshimu mtazamo wa mwingine, na hiyo ndio demokrasia au sio? Maana hii demokrasia hatukuipata enzi zile za zidumu fikra za Mwenyekiti wa ....!

Kuna sehemu niliwahi kuandika kuwa sikatai kuwa Kambarage alikuwa na mazuri yake (!?), ni kweli kwani alikuwa ni msemaji mzuri sana, na aliweza kuutetea uongo wake ufanane na ukweli. Huu uhuru wa vyombo vya habari, watu kukosoa serikali na hata hizi tovuti baraza, ingekuwa enzi za Kambarage, sote tungeishia jela au ulijui ilo?

Nasema tena Uhuru wa watu kutoa mawazo yao haukuwepo...! Wengi ambao walikuwa wanakerekwa na namna alivyokuwa akiongoza kama sio kutawala, walikuwa wanasemea uvunguni mwa vitanda vyao, hawakuthubutu kutamka adharani. Na wale waliothubutu, cha moto walikiona.

Nyerere aliwatisha viongozi waliokuwa chini yake na kuwafanya wamwabudu kama mungu wao. Wale viongozi ambao walisigana naye kama vile Mzee Oscar Kambona, na aliyewahi kuwa Katibu mkuu (secretary general) wa National Union of Tanganyika (NUTA) na baadae kuwa waziri wa kazi Mzee Michale Kamaliza (a polio victim), bila kumsahau mmoja wa wanawake jasiri na mwasisi wa Tanu Bibi Titi Mohammed, hao ni wachache ambao walikiona cha mtema kuni. (Bibi Titi Mohammed alihukumiwa kifungo cha maisha jela, akaja kusamehewa baada ya kutumikia kifungo kwa miaka miwili).

kwenye hii tuhuma alikuwepo pia Gray Likungu Mataka (Mwandishi wa habari), Capt Elia Dustan Lifa Chipaka na mdogo wake John Dustan Lifa Chipaka, Lt Alfred Philip Milinga, William Chacha aliyekuwa ubalozini nchini China na wengine tusio wakumbuka. Hivi kuna anaye juwa hatima yao ilikuwa nini...!? Kassim Hanga, aliye mrudisha Unguja, japokuwa alishauriwa asimrudishe kwa Karume, lakini kama kawaida yake, akamrejesha Unguja, na mwisho wake kila mtu anaujua.

Huyo Nyerere anaye tetewa Enzi ya ufalme wake, alipotaifisha mali za watu na kuzifanya zao, si ndio alikuwa editor -in-chief wa gazeti la Daily News, ambalo lilikuwa linajulikana kwa jina la The Standard kabla ya kufanywa mali ya serikali. (Kuna cha kujifunza hapa). Je nani anajua madhira gani yaliwapata hao wengine kina baba na mama kabwela!?

Huyo ndio Nyerere, Mfalme aliyeweza kutumia ufalme wake kuwanyamazisha wengine. Ila ukiwa Yusi ligi basi wewe umeula sana tu.

Leo hii waulize Watanzania kama wanajuwa chama kingine chochote kilichowahi kupigania uhuru wa nchi hii zaidi ya TAA (TANU). Hakuna atakaye kwambia, kama wapo wanao juwa basi ni wachache sana. Tanganyika ilikuwa nchi ya vyama vingi, lakini Nyerere alipokamata madaraka ya nchi ya Tanganyika vyama kama United Tanganyika Party (UTP), the African National Congress (ANC) na PDP, alivipiga marufuku kwa visingizio kuwa kazi ya kupigania uhuru imesha kwisha kwa hiyo hakuna haja ya kuwa na vyama vingine vya upinzani.

Nyerere mpaka anaondoka madarakani, raiya wengi kama si wote hali zao zilikuwa duni mno, kiasi cha kugeuza mipira ya magari kuwa viatu.

Je Watanzania atukupanga foleni kutwa na wakati mwingine kuweka makopo na mawe kwenye foleni, ili kupata robo kibaba ya unga wa njano (Nasikia kilikuwa chakula cha farasi na ngo'mbe uko Marekani), mchele, sukali, unga wa ngano, sabuni, dawa za meno, hizi ni baadhi ya bidhaa ambazo tulizibatiza jina na kuziita bidhaa adimu, tukivaa makata mbuga na kaniki na viroba vya magunia ya mbolea. Huku mabasi ya UDA yakifanya kazi kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 asubuhi na kuanzia tena saa 8 mchana hadi saa 12 jioni.

Kama ilikuwa unaishi Tandika na saa 12.30 jioni ikakukuta Kawe, ilikubidi uunge mkono Azimio la Arusha yaani utembee kwa miguu kurudi Nyumbani kwako.

Je hatukupigwa marufuku kuendesha magari siku za Jumamosi na Jumapili? Ili uendeshe gari siku hizo ilikuwa ni kwa kibali maalum (kwa wale walioweza kuvipata), kisa ilkiwa kunusuru kichele cha mafuta kilicho kuwa kimesalia kwenye akiba ya taifa.

Huwa napatwa na mchefuko wa tumbo, na kuhisi kutaka kukitoa chakula nilicho kula kama sio kutapika kabisa ninapowasikia watu wakisema kuwa Nyerere alileta amani Tanzania. Hivi hiyo amani aliileta kutoka wapi? Sikumbuki ni lini Watanzania tulipoteza amani yetu...! Tanzania ni nchi pekee ya Afrika ambayo amani yake haikuwahi kupotea hata siku moja. Nyerere alituogopesha sana na kutulisha ujinga na kutuimbisha nyimbo za kumsifia tu, watu wakapumbazwa, eti bila Nyerere nchi itaangamia... Naam tulimwita Mussa, si alitukomboa kutoka kwenye makucha ya Falao (Muingereza mkoloni).

Wapo watu wengine utawasikia eti Mchonga alituunganisha...! Agh! Hivi ni lini Watanganyika tuligawanyika, au jina Tanganyika, ndio kama kigezo kuwa Watanganyika tumetawanyika ndio tukaitwa Watanganyika?, au wana maanisha Kutuunganisha na Wazanzibar!? Watanganyika tulikwisha ungana kabla Nyerere hajaja mjini. Nadiriki kusema kuwa Lugha ya Kiswahili, dini za jadi na baadae Uislam na Ukristo, ndizo zilizo tuunganisha, na hatukuwahi kubaguana na ndio maana viongozi wa TAA na baadae TANU, ilikuwa rahisi sana kwao kupita kwenye majimbo ya Tanganyika na kueleza dhamira zao. Nyerere hakukutuunganisha kama wanavyotaka ulimwengu uelewe.

Ndio nasema japokuwa yeye ameshakufa, lakini ule mzimu (mfumo alio uwacha) bado unatawala platform nzima ya siasa za Tanzania, vyama vya siasa, wanasiasa wote, watawala na watawaliwa kwa maana ya vyama vinavyo jiita vya upinzani, vyote vimekumbwa na balaa la uongozi wake.

Mpaka leo Watanganyika wanashindwa kujikomboa kutoka kwenye makucha ya siasa zake zisizo tekelezeka.
 
Thank you in advance!
Nlikua bado kachanga enzi hizo! Humu kuna Milima c koko¤¤!.
 
Of course ndege wa wanaofanana huruka pamoja..
Walimu zangu walinfudisha kusikiliza na kutafakari kisha niulize.
Ukweli utabaki ni ukweli hata aje unaemtaka!.
Unapinga nini? Naona unapinga lakin hakuna maelezo ya hivyo wavipinga!.
 
Walimu zangu walinfudisha kusikiliza na kutafakari kisha niulize.
Ukweli utabaki ni ukweli hata aje unaemtaka!.
Unapinga nini? Naona unapinga lakin hakuna maelezo ya hivyo wavipinga!.
Wewe ndio walewale..fuatilia thread nlianza kuchangia wapi na mtiririko wa hoja uliendeje. natumai unajua kusoma na kuandika.
 
Back
Top Bottom