Natamani kuchana vyeti!

Pole sana. Yaan kuna walio kazini wanatamani kujiajiri, and vice versa.
Inaeza kua umepangiwa kua mjasiria mali, pambana na hyo chanel kwa moyo wote, ipo sku utaangalia nyuma utasema bora kweli sikuajiriwa. Trust me.
 
Dada, hapo ulipofikia siyo pazuri.
Nakushauri BADILI KUFIKIRI KWAKO. Kuna vitu ambavyo ni adui wa kusonga mbele
~kulaumu
~kunung'unika
~kulalamika
~n.k
Hivi vyote hufanyika kwa njia ya MAWAZO/KUFIKIRI.
Na matokeo yake huleta kujiona hufai, kukata tamaa na kuvunjika moyo.

Anza kujiwazia mema tangu sasa
~kuwa elimu uliyopata inatosha kukuwezesha kufanya vitu mbalimbali hata bila ya kuajiriwa.
 
Mwombe Mungu tu usikate tamaa utashinda
 
Usikate Tamaa, Jaribu katika mashirika ya kimataifa, kama UNDP
 
Nimecheka kama mazuri vile saiz naingalia hard copy angu ya CV imejaa had vumbi kwenye droo.. Inauma na inakatisha tamaa...mpaka nimezila...na mtaa mgumu...nilijua nipo peke angu daaah!!!!
 
mmh! inaudhi na kukera kama mtu maisha yako uliwekeza sana kwenye elimu ili baadae ikulipe lakini expectation inakuwa siyo kabisa! ila amini ipo siku MWENYEZI MUNGU atasema yes!! amini hivyo
 
Pole,,mpendwa uskate tamaa Mungu Ni mwema atakusaidia,,hata mm nilipata changamoto KAMA yako TENA zaid ya mwaka Na nusu nikaja nikapata NGO .japo najitolea ila naamini one day yes.usikate tamaa mpendwa
 


Waweza anagalia opportunities nyingine hata nje ya nchi, ili bando unalotumia jaribu kuangalia na kuomba nje ya nchi unaweza kupata kazi. tafuta kazi au omba kusoma Zaidi ili uongeze ujuzi na competence yako. Hakuna kukata tamaa pambana.
 
Sasa kama hata kuitwa interview huitwi,itakua cv yako hujaipangilia poa.
 
km vyeti havikusaidii tafuta kitakacho kusaidia...fanya biashara simple yeyote tatizo unalimit akili yako kufikiria upate mmoja na ndo ubaya wa elimu sasa jaribu kufikiria km huna elimu kila siku fikiria maisha km huna elimu ndani ya mwezi uje uniambie umepata akili gani
 
Watu wanatamani kuacha kazi wajiajiri,wewe unatamani kuajiliriwa? Hatari sana
 
Pole ndugu. Kata tamaa ya kuchana vyeti hivyo maana sio mzigo kukaa navyo. Ukijituma sawasawa katika shughuli za shamba baadae ukipata kazi utagundua kuwa hizi kazi bana ni utanashati tu. Kama mshahara hata haufiki tar 10 lini utakuwa tajiri kwa kuajiriwa. Utanielewa vizuri siku ukiipata hiyo kazi na kupokea huo mshahara ndo utanielea. Halafu huwezi niambia tu kuwa una wito na kazi hiyo. Nothing like that and if it is there it is just a temporary feeling
 
Mungu yup



Mungu yupo naanasikia kilio chako dada yangu endelea kumuomba utafanikiwa tuu.
 
Anza hapo ulipo mkuu. Kwani community development ni mpaka ukae ofisini kama kweli una mapenzi na profession yako basi mimi nakushauri uanze hapo hapo kwenye shughuli zako unazofanya sasa
 
I feel sorry for you. But Have a little faith God will make a way.
 
Wacha nichangie hapa

Mkuu pole sana kwa hali uliyonayo.

Ila mimi naamin pia hyo ndo njia yako ya kutoka financially.

Kama unaweza kufanya kilimo cha mahindi na kufuga kuku relax madam.

Implement tu hizo project zako kitaalam zaid na utaona matunda

Yamkin Mwenyezi Mungu hajakupangia kaz yes hajakupangia na huwez kulazimisha. Fanya kilicho ndani ya uwezo wako

Sijui kwann watu wengi tunapenda kuwa watumwa kuwa mfanyakazi au mtumishi wewe ni mtumwa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…