Natamani kila mtu aisome namba!

Natamani kila mtu aisome namba!

Kuna watu naona mnaamua kujiondoa uelewa. Hivi swali, kipindi kile si mlikuwa mnalalamika mifumo mibovu ya nchi? Sasa inarekebishwa tena hamtaki. Mfano huo wa waalimu, nyie ndiyo mlikuwa wa kwanza kuilamu serikali kuwa hilipi malimbikizo kumbe kulikuwa na udanganyifu mkubwa wa wafanyakazi hewa, na sasa serikali inarekebisha tena hamtaki, je nyie chandomo mnatoka sayari gani?
sasa hivi walimu wameshalipwa stahiki zao?
 
Walidhani wao mambo yatawanyookea, kumbe huyu waliye mkabidhi ufunguo Wa kugawa hewa anatunyima wote! Mbaya zaidi inafikia wakati hata wasaidizi wake Wa Katibu pia anawakatia pumzi!

hata walioimba haka kawimbo na wenyewe wanaisoma sarufii

Kuna watu naona mnaamua kujiondoa uelewa. Hivi swali, kipindi kile si mlikuwa mnalalamika mifumo mibovu ya nchi? Sasa inarekebishwa tena hamtaki. Mfano huo wa waalimu, nyie ndiyo mlikuwa wa kwanza kuilamu serikali kuwa hilipi malimbikizo kumbe kulikuwa na udanganyifu mkubwa wa wafanyakazi hewa, na sasa serikali inarekebisha tena hamtaki, je nyie chandomo mnatoka sayari gani?
kwahiyo walimu wamelipwa malimbikizi yao?
 
...hakuna atabaki salama...kama hata mwaka bado...!!na ukitaka upate utamu halisi wa hii hali,hesabu ni rahisi tu...chukua hali halisi iliyopo kwa sasa zidisha mara kumi (miaka ya utawala)= utamu halisi wa awamu ya tano
 
Kuna watu naona mnaamua kujiondoa uelewa. Hivi swali, kipindi kile si mlikuwa mnalalamika mifumo mibovu ya nchi? Sasa inarekebishwa tena hamtaki. Mfano huo wa waalimu, nyie ndiyo mlikuwa wa kwanza kuilamu serikali kuwa hilipi malimbikizo kumbe kulikuwa na udanganyifu mkubwa wa wafanyakazi hewa, na sasa serikali inarekebisha tena hamtaki, je nyie chandomo mnatoka sayari gani?
1,Mfumo ni nini?

2,Mfumo upi uliorekebishwa?
 
Habari wanajamvi!

Naam, Tunako elekea sasa kisiasa na kiuchumi ndiko hasa niliko kuwa naomba tufike! Ngoma kaipata kenge maji yote timbwitimbwili.Na bado.

Natamani kila mtu aisome namba.Walimu waisome namba, wauguzi waisome pia, wasanii waisome namba tena usiku na mchana, wale wanaojifanya kutaka kufanya usafi siku ya Ukuta waisome tena kwa herufi kubwa! Wakulima wazisome namba zoote ili wajue tulikuwa hatudanganyi kuwa kule ni walewale!!

Natamani aendelee hivihivi na asitokee mtu wa kumshauri.Natamani chama cha migomba waisome namba kwani wao walimpenda wenyewe bila shuruti. Napenda arudie tena kuwaudhi akina maalimu! Atuudhi wote! Natamani apige marfuku wanaume tusiongee mchana!! Aongee peke yake! Natamani kodi ipande mpaka peni tununue kwa shilingi Laki sita.

Natamani wanafunzi waisome namba mpaka wajute. Natamani wanawake waisome namba mpaka kujipaka mafuta iwe ni anasa!

Halafu uchaguzi ndio uje 2020.Tutakapo waambia chama kile ni walewale watatuelewa.Tutakapo waambia chama kile mkiwapa tena watatoa teuzi kwa ukanda watatuelewa. Tutakapo waambia wanavunja katiba watatuelewa.Tutakapo waambia kuwa wanavinyongo watatuelewa. Karibu 2020.
Tuisome mara ngapi tena
 
Tumeipendaaa wenyeweee (paampaaaa)
Chaguo letu milelee(pampaaaa)
Watavimba wapasuke(pampaaa)
Watajijua wenyewe (pampaaa)
Wacha waisome nambaaa eeeeh (WAISOME NAMBAAAAA)
Sisiemu mwele kwa mbeleeeeeee
Oooh mbelee kwa mbeleeee
 
Ndio jibu hilo?

Majibu yenu yamekaa vizuri sana,kuna yule DC aliulizwa maana ya demokrasia sikumbuki alijibu nini

Walewale
Kuna viumbe wengine tunao hapa JF kimawazo tu ila kiuhalisia wapo nje ya nchi wanafanya vibarua. Kisa cha mi kusema mhusika ni mbeba box alikuwa anasema mpaka sasa serikali haijafanya kitu, wakati tunajua serikali imejitahidi sana
 
Mmmh...hayo maombi huyo mwananchi yamenitisha ila tu nashangaa wimbi la watu kuichukia nchi inaongezeka hapa viongozi wa dini wanatakiwa sana
 
Kuna viumbe wengine tunao hapa JF kimawazo tu ila kiuhalisia wapo nje ya nchi wanafanya vibarua. Kisa cha mi kusema mhusika ni mbeba box alikuwa anasema mpaka sasa serikali haijafanya kitu, wakati tunajua serikali imejitahidi sana
Hizo ni fikra potofu

Uhalisia wa anachozungumza mtu huwa wazi

Ukiona ukwepaji wa maswali ujue hapo lilikua ni suala la kufikirika au lililosikiwa lisilo na evidence
 
Back
Top Bottom