Natamani hata kunywa sumu, mapenzi jamani...

Natamani hata kunywa sumu, mapenzi jamani...

jack 1

Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
61
Reaction score
63
mimi ni msichana wa miaka 26, naishi arusha nilikua na mchuchumba wangu ambae tumedum nae kwa miaka 2 na kupanga mambo mengi ya kuoana wote tumepanga nyumba moja japo kila mmoja anakaa chumbani kwake dec nilisafiri kwenda likizo nyumbani mwanza nimerudi jan 10 nimekuta kaanzisha mahusiano na dada jirani tena tumepanga nae nyumba moja nifanyeje wana JF yaani wanapika na kupakua yule dada ananiwekee nyimbo za mafumbo. taarabu, mpaka nakosa ham ya kuishi nilipomtaka nimuulize mchumba wangu imekuaje maana hatukukosana kabisa hataki kupokea cm yangu ananisalimia tu basi nampenda sana jamani naumia nashindwa niongee na nani anisaidie mimi niende wp jaman haaa kwel dunia haina huruma
 
oi! Hilo ni jambo la kumshukuru Mungu upo na uhai hadi mida hii na tena 2pa kule ishishi maisha yako fanya yale yaliyo sahihi nani amekudanganya ulizaliwa kwa ajili ya mtu fulani hapa duniani......tena ikibidi mpe time yake chukua time yako yeye mwenyewe atajiongeza mda kifika kuwa aliacha gold akakimbilia mawe tena mawe ya kutu..... Mapenzi ndo yalivyo jaribu kuyaona maisha ni zaidi ya hapo ulipofikia kuna level zaidi na zaidi ambazo unapaswa uzivuke soon so dont stack on one level
 
Piga moyo konde na usonge mbele,kwani kuvunjika kwa mahusiano yenu sio mwisho wa maisha,mshukuru Mungu kakuonesha mapema aina ya mwanaume uliyekuwanae,mwanaume anashindwa kuvumilia hata mwezi mmoja hakufai. Waswahili wanasema pindi ukizaliwa unaambiwa wapo sio yupo kwa hiyo vumilia aliyekupangia Mungu bado hujakutana naye.
Ikiwezekana hama kwenye hiyo nyumba tafuta chumba kwingine.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Wacha bana....hivyo.eeeh.....

Well.....pole sana shosti......hivi maisha yalivyo matamu namna hii.....raha zote hizi za dunia......umefikia kuwaza kunywa sumu.......uwiiiii.....God forbid......toa kabisa hayo mawazo.......huyo sio mwisho wa maisha yako.......tupa kule.....hama hapo..........
Vuta ngoma mpya.......simple........

Mapenzi kizungumkuti r.i.p mleta thread kajilaze bana peponi kuna bata zaidi.
 
acha ujinga, unywe sumu kisa mchumba?ufe kwa hasara ya nani kama sio wazazi wako, achana nae mpotezee, watu wanaachwa na waume wamefunga ndoa na watoto wanao sembuse boyfriend. ukiona hasira sana labda uhame nyumba maana wanawake wa hivyo ni hatari, kesho akiona huyo mchumba kakuangalia atahisi anataka kurudi kwako anaweza kukudhuru. Jaribu kuwa mbali nao endelea na maisha yako utapata anae kupenda na kukuheshimu. kama ni mcha Mungu tulia katika kuabudu na kumtumaini Mungu utashinda. Ni mapito tu hayo.
 
Dunia sio mbaya walimwengu ndio hawana maana.., wewe achana nae na hama hapo endelea na maisha yako, utapata anayekujali..

Kumbuka, Nobody is worth your tears (let alone your life) and if someone is.., he wont make you cry..
 
mimi ni msichana wa miaka 26, naishi arusha nilikua na mchuchumba wangu ambae tumedum nae kwa miaka 2 na kupanga mambo mengi ya kuoana wote tumepanga nyumba moja japo kila mmoja anakaa chumbani kwake dec nilisafiri kwenda likizo nyumbani mwanza nimerudi jan 10 nimekuta kaanzisha mahusiano na dada jirani tena tumepanga nae nyumba moja nifanyeje wana JF yaani wanapika na kupakua yule dada ananiwekee nyimbo za mafumbo. taarabu, mpaka nakosa ham ya kuishi nilipomtaka nimuulize mchumba wangu imekuaje maana hatukukosana kabisa hataki kupokea cm yangu ananisalimia tu basi nampenda sana jamani naumia nashindwa niongee na nani anisaidie mimi niende wp jaman haaa kwel dunia haina huruma
Pole sana kwa iko kiza cha mapenzi maana unasalimiwa lakini simu haipokelewi
 
Omba Mungu kifo kisikukute kwenye bata

Sasa bora ipi......? Kikujie kwenye bata........au kikujie ukiwa umeachwa na mpenzi.......? Think Cocro.......think twice.......
 
Hama hiyo nyumba ina mikosi la sivyo utakuwa unalia kila siku na tatizo la kutaka kujiua litatimia iwapo utazidi kuwepo hapo nyumbani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom