Natamani Dr. Slaa aje aniambie haya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natamani Dr. Slaa aje aniambie haya!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JingalaFalsafa, Apr 29, 2012.

 1. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Tukishampa nchi 2015 (japo tunaweza hata kesho), atawafanyaje watu hawa!

  Wenye majumba ya thamani hali jirani zao wanalala nje!
  Wenye kumiliki magari makali hali jirani zao hawana uwezo wa kununua hata ndala!
  Wenye kulimbikiza fedha benki hali jirani alala njaa?
  Wenye kuishi Masaki na Osterbay hali kuna wa Tandale na Manzese!
  Wenye kuona ni haki kuzunguka misuru ya magari hali hospitali zetu hazina gari za wagonjwa, na shule na walimu wake hoi kwa mazingira yaliyokosa vitendea kazi.
  Wenye kuhodhi aridhi kubwa kwa manufaa ya watoto wao!
  Wageni wanaochota rasilimali zetu hali twabaki kapuku!
  Wenye kula na kusaza hali jirani na watoto wake wanashindia uji!
  Uwepo wa high class mahosptalini na kule kwetu sie.
  Uwepo wa special schools hali na St. Kayumba zetu.
  Hata uwepo wa Dar na Mwanza hali kuna Lindi na Singida.
  Na mengine kama hayo yaashiriayo UBINAFSI.

  Mungu wetu anaita!
   
 2. Y

  Yabisi Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  maswali mazuri
   
 3. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Wakati wa kampeni haujafika tuliza kipila muda wa kampen ukianza atafunguka usimsababishie Offside ya kijinga!
   
 4. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mkuu, kosa si kuwa na utajiri bali kosa ni njia ulizozitumia kuupata huo utajiri ni halali?
   
 5. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Tumwombe Mungu 2015 tufike salama ili tukishuhudie kiama cha mafisadi.
   
 6. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  ...Mawazo ya Kimaskini...

  ...Kila mwananchi ana haki ya kumiliki pesa, ardhi, majumba, kupata huduma za hospitali na shule za kiwango akipendacho ilmuradi havunja sheria, suala la kuwasaidia maskini wanaomzunguka ni hiari yake na katu hawezi kulazimishwa kufanya hivyo...
   
 7. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  ...Ukiondoa viongozi wachache wa sasa wanaokula kupitia mfumo wa kiserikali na viongozi wapya watakaopata mchongo wa kula serikali baada ya uongozi kubadilika, kwa asilimia kubwa safu ya wenye kufaidi maisha,kwa mantiki ya matajiri, itabakia vilevile kwa sababu utajiri kwa mtu ni skills, na kwa yeyote aliye na skills hizo pesa zitamfuata tu, kuendelea kusubiri ni dalili za kutokuwa na uwezo huo...
   
 8. papason

  papason JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  labda mbinguni tuu ndo hautakutana na hayo matatizo
   
 9. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Mungu wetu ametuumba na kutuwekea msingi mkuu wa namna ya kuishi, yaani UTU, ambao upo nafsini mwa kila mtu..., na kutouishi ni sawa na kujisaliti na kujinafiki mwenyewe, umejikataa kabla ya kukataliwa na jamii. Katika mantiki ya UTU, maisha ni hatua, hakuna UHALALI wa kuwa na hatua ya 5, kwa wenye 0 au 1, ukishapata 1 ni haki na wajibu wako kumsaidia jirani yako kuifikia hiyo moja, akishaifikia tafuta ya 2 sasa. Yaani kusiwe na 2 kama hakuna 1 na 1, au 3 kama hakuna 2 na 2. Najua kuwa mimi na wewe ni vigumu kushuhudia hili, lakini tusiache kusimika misingi ya kufikia hili, na mifupa yetu aridhini, italoweshwa kwa maji ya mito ya machozi ya furaha kutoka machoni mwa watoto au vitukuu vyetu, na hiyo ndiyo upendo wetu wa dhati kwao, na ndio kuishi hata baada ya kifo chetu. Tusijidanganye na mnazoziita haki za binadamu, zimekosa mantiki. Je, ni haki kushindanishwa kiwete na mzima katika mbio, au kumuacha msituni ajitetee? Hatuoni huko? Mtu makini huongozwa na mantiki na si mifumo iliyowekwa kwa maslahi ya watu fulani, MANTIKI huweza kubadilisha mfumo, lakini si mfumo kwa mantiki. Tukisema muda bado, kutakuwa ndio kushindwa kwetu, wajukuu wetu watakumbwa na haya haya ya leo, labda wao waje kuwafanyia wajukuu zao na lawama ziwe juu yetu. Maisha ni furaha, kama haipo basi ni upuuzi, na hakuna furaha ya mtu ila watu! SI SAHIHI KUNGOJA, NA TUANZE KUISIMIKA SASA, hata kwa mahubiri kabla ya nguvu!
  Labda mimi jinga, niongozeni kwa hoja, msitukane jamani wanaafrika wenzangu wa Tanzania.
  Mungu wetu anaita!
   
 10. C

  Complex number JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 28, 2012
  Messages: 219
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Hisia zako kali,umemaanisha unachokitetea,inaonesha una nia na dhati na usawa katika jamii,keep it up.LAKINI,Je turudi katika misingi ya ujamaa?
   
 11. K

  Kiboko Yenu JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ukimaliza kachukue posho yako kinondoni
   
 12. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Maswali yako yote niliyo highlight hayana maana wala mashiko kwa Tanzania ya leo na Yeyote atakayeenda huko amefilisika kisiasa. Ulichotakiwa kuongezea ili maswali yako yawe relevant ni kuwa 'Wenye kuwa na vitu hivyo kwa kuvipata kwa njia zisizo halali'

  Nafikiri tusitishie kuadhibu hard working ili kuwa please wengine cha muhimu ni kuweka mazingira ya kila mtu kufikia vitu hivyo provided atafanya kazi kwa bidii. Lets fight for lifting up everybody not bringing down the lawful success.

   
 13. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Nakupa 'like' kama mia tano hivi. Unajua muanzisha thread yawezekana ni mpambanaji mzuri ila anasahau kuwa CDM hawana chuki na mtu yeyote. Naomba kumwambia huyu jamaa pamoja mie sio msemaji wa CDM kuwa; tunategemea wale wa masaki na o'bay watakaa walipokuwa allocated kisheria, waliopata utajiri kihalali au kwa njia zinazokubaka hawatabugudhiwa ila kiufupi maslahi ya nchi na wanyonge yatawekwa mbele. Yasipofanyika haya una uhuru wa kuchagua chama au mtu yeyote after 2015. Karibu sana.
   
 14. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Kama ndiyo mantiki iliyomo nafsini mwet, basi hatuna budi kuanza kuisimika hiyo, japo ni sawa kwa afukiaye mbegu ya mkangazi kuvuna mbao, lakini tumaini analo si kama yule aliyeacha, hata isipoota wapo watakaona umuhimu wa ulichotaka kufanya, watafanya wajukuu wao watavuna mbao, huko ndiko kuishi hata baada ya kifo chako. Nyerere alisema "...ujamaa ni imani....", tukiihubiri inavyostahili, watoto wetu wataiishi. Tupindue nafsi zetu, kwani hata siku moja haiwezi kutokea afrika ikawekeza magharibi, NEVER. Sasa kwanini tung'ang'anie kupinga ukweli? Ndoto gani tunazoota, au ndio bora liende tu hali tunachezewa sharubu? Mpumbavu ni yule anayefananisha thamani ya maisha yake, na yale ya taifa zima!
  Nimemtaja Dr. Slaa, kama mtu anayeweza kunielewa na mwenye ushawishi mkubwa kwa watu, kati ya wanaogombea nafasi ya kutuongaza katika hiyo furaha. Sina maana tofauti Kiboko Yenu, labda unifikirie tena, ila utakuwa unanionea ukiamini hvyo, japo siogopi. Ndicho nachoamini, upeo wangu umeona hilo nafsini mwangu, ndio MANTIKI KUU NAFSINI MWANGU, UTU!
  Sisi tulishazikwa kaburi na tumeshaoza, tuwafikirie watoto wetu wajao nao wasifukiwe hai kama sisi. Mungu wetu anaita, umoja na kuthubutu ndiyo nguvu yetu, yu tayari kutushindia.
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Usisahau kumuuliza na haya:

   
 16. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  haswaa! kwa jinsi nilivyomsoma mtoa uzi naona anataka dr aanzishe jihad dhidi ya wenye mali hata kama wamejinyima na kujituma kuzipata!!
   
 17. K

  KISAKA MORIS JF-Expert Member

  #17
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uko sahihi laki,ni tatizo lako umeshindwa kuelewa shida si mtu kumiliki vitu hivyo shida ni njia anazotumia kujimilikishia vitu hivyo,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,kama mtu anaweza kumiliki mali kihalalia ni vizuri sana na tunataka taifa la aina hiyo lakini kama ni njia za wizi kama wafanyavyo wengi ndiyo wanatakiwa wasakwe....
   
 18. Y

  Yasser5 JF-Expert Member

  #18
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hapa pokoje wadau
   
 19. kombati

  kombati Member

  #19
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  watajichimbia chini hawa wala nchi maana hawataweza kuhimili hasira za wananchi ambazo mpaka sasa zimeshaanza kuvuja
   
Loading...