Nataka niwashtaki Barclays

Ozzie

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
3,222
1,225
Ninatafuta wakili yoyote mzuri atakayeweza nisaidia kusimamia kesi dhidi ya Barclays Bank.

Nikiwa kama mwajiriwa wa serikali nilichukua mkopo Barclays mwaka 2012 kama Premier member.

Baadaye nikanunua mkopo husika kwa kutoa thamani halisi waliyoandika kwamba ndiyo napaswa kulipa ili kumaliza deni (wakiweka na early settlement charges).

Cha kushangaza baada ya kulipa, naona akaunti bado inaonesha kwamba ninadaiwa kiasi fulani, na kwa bahati mbaya hawa watu wamekuwa wakiendelea kukata kila pesa inusapo kwenye akaunti husika.

Nimejaribu kuwasiliana na hawa jamaa, lakini naona wanaleta mzaha na pesa za watu. Wanaishia kufowadiana email tu, lakini hawafanyi lolote. Hawajui pesa hata ikiwa ni shilingi ni kubwa sana kama si yako na hujui mwenzako kaipataje.

Niko ughaibuni, lakini wiki mbili zijazo narudi Tanzania, ninatafuta mwanasheria atakayenisaidia kuwapa adabu. Hata kama itakuwa hasara kwangu, lakini ilete heshima.

Advocate mchapakazi naomba ni PM please.
 

saimon111

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
1,726
2,000
Hii case imekaa vizuri sana, ningekusimamia sema kwa position niliyopo saiv sitaweza.....kuna advocate mmoja ni mzuri ngoja nikutumie digits zake
 

kuku87

JF-Expert Member
Mar 3, 2013
1,221
1,500
Mwajiri wako ndo inabidi asimamishe hayo makato nitafute kwa kunipm nikuonganishe na manager muhusika wa mikopo ya taasisi yko
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom